Wednesday, 18 May 2011

Dogo, acha kutishia watu wazima nyau

NI muciare Kristo ni muciare,
(ni mzaliwa mkombozi)
Ni muciare yaciaritwe itura lya Daudi (ni mzaliwa kazaliwa nyumbani kwa Daudi)
Ni muraika akyuga (Ni malaika asemaye hivyo)
Ni muciare muhonokyia witu (Kazaliwa mkombozi wetu)
Mutuhoyeri mututhaithaneri (Mwombezi na mtetezi)
Mengine utamalizia mwenyewe. Ni lugha gani? Not important so far.

Ngoja niimbe kwa lugha baba na mama ya lugha Afrikani, ambayo aihitaji tafsiri.

Ni fisadi Dogo, ni fisadi,
Ni fisadi kwa mgongo wa dingi,
Bilionea mtoka shuleni!

Ni fisadi kama baba yake
Ni fisadi kama mama yake nanihinoo
Ni fisadi hata akanushe vipi.

Ninininininhhhhi hiyo tena, pombe hizi siku moja zitanifunga.

Leo nina hasira nusu ya kulipuka kama bomu. Nina hasira ingawa mara nyingine huwa napafa furaha ya hasira. Upo hapo?

Fungua masikio usikie unabii huu kwa wadanganyika waliwao na kila fala kuanzia yule wa Kiajemi, kunyantuzu na kimeru ajiitaye morani wa Kimmasai.

Juzi nilicheka nusu kunonihino kwenye salawili. Wajue ni aje? Si baada ya huyu dogo tuseme mtoto wa nyoka ambaye naye ni nyoka kuanza kuleta nyodu kwa kutishia watu kuwa atawapeleka kwa pilato kwa kumvua gamba.

Kwanza nimwambie huyu bwana mdogo asiye na lolote zaidi ya kudandia mgongoni mwa dingi yake. Hawa anaowatisha ni watu wazima wasiotishiwa nyau. Wamemshinda dingi wake yeye kinyamkera mchanga aliyeko mberekoni atawaweza?

You know what? Baada ya Daktari Willy Silaha kudai kuwa Riz-One Kikwikwi ni bilionea, eti alijitutumua kuwa atampeleka kwa pilato asijue mafisadi na waliomuumba baba yake waliahidi hivyo na kuishia mitini!

Wako wapi wanasharia kama Nimrozi Mkononi, Endelea Chenga na mafisadi wenye nazo kama Eddie Ewassa ambaye alikubali yaishe huku watu kama Grey Mugonjoka eti wakitishia kumfikisha Silaha kwa pilato wasithubutu.

Dogo, dingi wako kafyata mkia itakuwa wewe yai! Kumbaff sana. Nasikia eti nawe ni mwanasharia. Kama ni wale wa chuo kikuu cha Manzese nakuonea huruma. Maana miprofwesa mingi pale imechanganyikiwa kiasi cha kuonea watu na kuwanyenyekea mafisadi.

Kama ulishinda mtihani wa sharia si kwa sababu you are competent. Indeed, so to speak, if I may and if all laws and rules are employed, you passed just because you are the son of the prezzo. Finito. Like or lick it. Shauri yako.

Najua you can not reciprocate to this as a quid pro quo knowingly that I am but a prof of juris. Jaribu niku-bang legally.

Kwanza dogo, inapaswa unishukuru kwa kukupa somo bure. Maana nikilinganisha somo ninalokupa wewe Dingi yako, mama yako hata hao ndugu zako na wapambe wa wao na kiasi nilichokuwa nikilipwa nilipokuwa nafundisha Chuo Kikuu cha Havard, naona kama nimekupenda sana.

Nikupe lau fununu. Dokta Willy Silaha na mchunaji sorry mchungaji wa kujipachika Kris Mtikisa ni al-shindikanaa kwa lugha za kitaalamu. Laiti
Pia ni vizuri ukafahamu kuwa wabongolalalanders wanajua ulivyo bilionea atokanaye na wizi. Wanajua kuwa hata mama yako ni bilionea.

Wanajua kuwa hata Freddie Ewassa ni bilionea. Wanajua nani ameiba nini, kiko wapi, kwa namna gani na anakula na nani. Unadhani kuwa hawajui? Lol! Wanajua kuwa utawala wa dingi yako umegeuka mali ya ukoo na kujuana.

Wanajua kuliko unavyojua na unavyodhani hawajui. sema. wananyamaza wakiacha historia baadaye ifanye vitu vyake.

Ama kweli ulaji tena wa dezo hulevya. Yaani mara hii umesahau yaliyowakuta akina Morinyo watoto wa Ben Makapu wa tunituni na nkewe mama Ana-tamaa! Ama kweli la kufa halisikii.

Kama historia ya Bongolalaland inakutia woga kwanini usisome ile ya Zaire ya Mobutu ambaye alijegeuza kila kitu yeye na watu wake akaja kufa kifo cha mbwa na kuzikwa kwa aibu tena kwa siri ughaibuni utadhani mbwa.

Kama anaona historia ya Mobutu ni ngumu kupata basi aende kwa Joe Makambale aliyevuliwa hivi karibuni ona anavyoanza kupotea utadhani hajawahi kuwapo!

Hata Dingi yako kuna siku atatokomea kama walivyotokomea wengine isipokuwa mzee Mchonga aliyeacha legacy inayong’ara.

Laiti Dogo angekuwa msomi lau wa kawaida na si kihiyo anayeitwa msomi, basi angefunga domo lake ili angoje njeo hapo baadaye ipitishe hukumu yake.

Hata kina Mubarak wa Kibaraak kule kwa Farao walikuwa na kiburi kama cha baba yake huku watoto wao kina Ala kumbe na Gamal wakijiona kama wasioguswa. Uliza. Sasa wako wapi? Wananyea debe bila huruma huku baba yao akingoja apatikane na hatia anyongwe kama mbwa kama alivyofanyiwa Saddam Hussein habithi wa mahabithi.

Nimalizie na semini endekezi ya wizi iliyofanyika hivi karibuni kule Idodomya. Nani anakumbuka rafiki yangu alivyokuwa akijiliza na kuwawekea mkwara wezi?

Wengi tunajiuliza bila majibu. Kama dingi mzima mwenye kaya unalia lia hao wa chini yako wafanye nini? Kwani hayo maulaji ni yanini kama siyo kuwatoa watu wanapoboa?

Hata hivyo tusishangae. Wapo wanaomuona kama mnafiki na msanii wa kawaida anayepiga mkwara ili muda wake uishe atimkie kizani.

Niwachekeshe. Juzi niliona video ya bi mkubwa Shari Njaa Kikuku akihutubia kule kwa Joji Kichaka! Du kumbe mtupu ung’eng’e haupandi. Alivyokuwa akitokwa jasho na lafudhi yake ya kimachinga huku akikosea maneno ya kimombo sina hamu. Wapelekeni wake zenu shule.

Nimalizie kwa kumuonya kuwa Dogo asipofunga domo lake tutamvua nguo na si magamba.

Kama amesomea taaluma yoyote mbona haifanyii kazi na anajificha nyuma ya umoja wa vitegemezi wa kiama cha baba yake.

Ngoja nisogee karibu na hili hekalu. Naona shangingi lile kama la Dogo. Huyu mlinzi naona hana heri nami acha nijikate kabla sijaitiwa mbwa wa Fanya Fyoko Ukome. Khalas kweisine.

3 comments:

Jaribu said...

Hata mimi nilimwona akitetemeka. Hata mmewe naye nilishawahi kumshuhudia akibangaiza bangaiza, "I am heah to sav the people of Tanzania." Wajifunze lugha au watumie wakalimani.

uswazi said...

haha haaaa, du! ebwana hii kali. Hata mimi nimeona video ile ya mamsap. kwa kweli angeongea kiswahili tu, halafu mtu mwingine atafsiri kimombo.

uswazi said...

haha haaaa, du! ebwana hii kali. Hata mimi nimeona video ile ya mamsap. kwa kweli angeongea kiswahili tu, halafu mtu mwingine atafsiri kimombo.