The Chant of Savant

Tuesday 16 August 2011

Kwenda visiwani pasipoti tena!


Mbunge wa viti maalum, Mwanamrisho Taratibu Abama (CUF), hivi karibuni aliitaka serikali kurejesha utaratibu wa watu kutoka Tanzania Bara kuingia visiwani Zanzibar kwa paspoti ili kupunguza wimbi la ujambazi na mauaji linazidi kuongezea siku hadi siku.

Kauli hii ya kibaguzi na kashfa, licha ya kuwakasirisha na kuwasikitisha wenye akili, iliwashangaza wengi. Huyu mbunge anapata wapi jeuri ya kutoa matamko ya kibaguzi tena kwenye bunge la muungano? Nini mantiki ya Tanzania kupigana na kaburu kuondoa utawala wa kibaguzi kusini mwa Afrika yaani Apartheid? Je huyu mbunge anaijua historia ya taifa hili kwenye kupinga dhuluma naubaguzi? Kweli huyu mbunge ni mtanzania au wa kuja?

Ajabu, Abama alitoa kauli hii bungeni na bunge halikulaani ubaguzi na matusi haya kwa wananchi wote wa Bara akiwamo rais wa jamhuri ya Muungano. Pia hakuna mbunge aliyejitokeza kumuelimisha huyu mbunge ambaye uwezo wake wa kuelewa mambo ya kawaida achia mbali sheria unatia shaka. Ni hatari kwa mtu mwenye wadhifa wa ubunge kuwa na roho ya kibaguzi na hitimisho la jumla bila kuchelea nafasi yake. Kwanini Abama hataki kukubali ukweli kuwa kwenye nchi moja si rahisi wala haki watu wa upande mmoja kubeba pasipoti kuingia upande wa pili? Kwanini Abama hataki kukubali kuwa hata watu wa visiwani wanaweza kuwa tishio kwa mstakabali wa bara hasa ikizingatiwa kuwa wamejazana na kuzaliana bara kuliko hata Zanzibar? Hivi tukianza kuulizana nani ni nani katika nini kati ya bara na visiwani nani ataathirika hata kuadhirika ukiachia mbali kujua nani anamhitaji nani?

Kwanini Abama na wenye mawazo kama yake hawataki kusoma alama za wakati na kuuangalia ukweli kuwa bara imekuwa kimbilio la watu wengi wa visiwani wasio na pa kushika huko kwako? Kwanini ni halali kwa watu wa visiwani kuja bara, kufanya biashara na kuzaliana na kuneemeka lakini ikawa haramu hata kwa watu kiduchu wa bara walioko visiwani kuishi kama raia yoyote kwenye nchi yake?

Matamshi haya ya kijinga ya Abama yanathibitisha wazi kuwa hata uchomaji wa vibanda vya wafanya biashara toka bara una Baraka za baadhi ya wakubwa visiwani. Nani mara hii kasahau hotuba za chuki zilizokuwa zikiendeshwa na shehe mmoja aitwaye Azzan ambaye ukimtazama ni mwarabu kwa kila kitu? Mpuuzi huyu alikuwa akimtuhumu makamu wa rais Dk Gharib Bilal kuwa anataka kuigawa visiwani kwa bara. Kwa walioona alivyojibiwa kwenye jamii forum wachangiaji wakimtaka arejee kwao Oman akawagawe na kuwabagua huko watajua hasira walizo nazo wananchi dhidi ya ubaguzi huu. Ajabu mhusika hata akienda huko Oman hawatampokea zaidi ya kumuita Abdi yaani mtumwa wa kawaida! Watu wameshiba matunda ya muungano sasa wanaanza kuutapikia. Kama kuna watu wanauhitaji muungano zaidi si wengine bali visiwani. Maana bara nchi yenye ardhi kubwa na kila aina ya maliasili ahihitaji kijipande cha ardhi kisicholingana na hata baadhi ya wilaya zake ndogo. Hayo tuyaache. Ila tutahadharishe. Tukianza kuchokoana kama pweza wapo watakaoamsha hasira za akina Christopher Mtikila na kuanza kujilaumu. Kuna haja ya watawala wetu kuwakemea hata kuwatimua watu kama Abama ambao uwezo wao wa kufikiri unatia kila aina ya shaka.

Tukianza kuulizana asili yetu kuna wazanzibari ima watajikuta ni wamalawi, wacongoman, waarabu hata wahindi kiasi cha kutostahili kuishi hapo wanapopaona na kupaita kwao. Dhambi ya ubaguzi huwa haiachi kumg’ata mwenye kuitenda. Pia ni upofu na upogo kwa watu kuwekeza kwenye ubara na upwani. Maana kama tukianza changu kichungu chako kichungu tutaumbuana kiasi cha baadhi ya wenzetu kuathirika kabla yaw engine. Au ni kwa vile Abama ni mwanachama wa CUF chama ambacho siku zote kimekuwa na harakati za kichinichini za kuvunja muungano ili kiitawale Zanzibar?

Abama ni mbunge wa viti maalum ambaye hamwakilishi yoyote isipokuwa chama chake na tumbo lake. Hii ndiyo hasara ya kuwagawia watu ubunge kama ubuyu kwa kuangalia vyama na maslahi binafsi hata jinsia. Wabunge wa namna hii licha ya kutokuwa na uhalali na uwezo ni mzigo kwa walipa kodi. Wanakula bure kiasi cha kujipayukia watakavyo kwa vile wamefika pale kwa bahati. Nchi zenye demokrasia iliyokomaa hawana viti maalum bali mazingira sawia ya kuwania nafasi za uongozi.

Tumuulize Abama. Je wabara ndiyo wezi pekee duniani na wazanzibri malaika?
Je wazanzibari wanaoishi bara na kufanya mambo machafu nao waingie bara kwa paspoti?
Je wabara wakitaka wazanzibari wanunua visa ya kuishi bara wataona haki? Je mbunge ana habari kuwa bara inatunza kulisha na kwa kila wazanzibari wengi kuliko huko visiwani? Bila shaka mbunge, Abama yote haya sema ameamua kutafuta umaarufu naye ajulikane yupo bungeni. Si hilo, huyu mbunge anapaswa achunguzwe akili zake. Maana ukiangalia anavyofaidi marupurupu ya ubunge kwenye bunge la bara wakati huko kwao hatuna hata chembe ya mbunge, shurti awe ima ni mbaguzi mhafidhina au asiye na akili timamu. Tukianza kubaguana kwa tunakotoka, kuna watu wataiona dunia chungu kuliko hao wabara.

Okey wabara ni wezi. Na huo mpunga na ardhi vyao je? Kama wabara ni wezi kiasi cha kutishia usalama wa Zanzibar mbona mhusika anapata nafasi ya kuja bara kwenye bunge na kufaidi posho za makalio na kupayuka kama alivyofanya na asidhulike? Jamani tuache ulimbukeni wa kujiona bora kuliko wengine. Huu, licha ya kuwa ulimbukeni ni utoto na utovu wa nidhamu kuhukumu watu wa asili yao kama alivyofanya Abama. Hakika anapaswa kulaaniwa sin a waandishi wala watu binafsi tu bali bunge na serikali Au ni yale ya baniyani mbaya kiatu dawa? Au ni yale ya changu changu chako changu.Tujaribu kwa watu na wenye shukrani na kumbukumbu. Bila muungano Zanzibar itageuka Comoro nyingine. Na hao wabara mnaowachukia watakuja huko na mitutu ya bunduki kulinda amani mtakapoanza kupinduana kwa uhizbu afro na upemba na uzanzibari.

Hisia na mawazo mgando ya kubebeshana passports kwenye nchi moja hayawezi kutufikisha popote. Kama wapemba nao watataka wazanzibari wabebe passport kuingia Pemba kutokana na udogo wa kisiwa chao wazanzibari watasemaje?

Tuhitimishe kwa kumtaka Abama aombe msamaha huku bunge likimuonya hata kumshughulikia ipasavyo. Abama hafai kuwa hata mlinzi achia mbali mbunge kama ni mbaguzi kiasi hik
i.
Chanzo: Dira ya Mtanzania Agosti 16, 2011.


5 comments:

Miss K. said...

Ama kweli watu wengine huwa hawana fikra au labda ni upeo wao mdogo wa kufikiri.Swala la passport limepitwa na wakati na kama wanataka basi na wazanzibari nao wabebe. Huo ni ubaguzi kabisa kwanza watanzania wanaoenda Zanzibar sio kama wanalowea huko kama wao walivyojazana bara.Hivi wakisema kuwa kila mtu arudi kwao nani wataathirika zaidi? Wao wamejazana TZ bara wanakuja sijui kwa mitumbwi au majahazi bila passport. Huyu mbunge kakosa hoja ndo maana anakurupuka na kujiropokea.

Anonymous said...

Huyu mama hana maana. Sura yake kama mzaire vile. Inaonekana wazazi walikuwa watumwa na ana mawazo ya kitumwa.

Jaribu said...

Mimi sioni kwa nini hawa jamaa tunawang'ang'ania. Hamna chochote tunachopata isipokuwa maudhi tu. Mimi sielewi kwa nini wanajiona bora wakati hawana lolote. Ufukara wao ni sababu ya uzembe wao, na isingekua Bara ku-relieve population pressure wasingekuwa tofauti na Somalia. Wache waende tupumzike kusikia pumba za kila siku.

Anonymous said...

Mama lina sura mbaya kama mat...
Warudi kwao waone cha moto kama hawatatafunana kama wadudu.

Anonymous said...

Unastahili sifa Bi Abama tuweke pp ili tujuwe wezi ni nani?
na sio kuingia tuu kama kwenda iringa