The Chant of Savant

Wednesday 24 August 2011

Msekwa naye ni gamba


Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekuwa kwenye mikakati ya kuuaminisha umma kuwa kinaweza kurudisha hadhi yake. Moja ya mikakati ya kurejesha hadhi na imani ya chama ni kujivua gamba. Dhana hii ya kujivua gamba ilianzishwa baada ya CCM kubaini kuwa ufisadi ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya vigogo wake haufichiki wala kuweza kulindwa. Dhana hii imeishapata majeruhi ambapo aliyekuwa mbunge wa Igunga Rostam Aziz aliachia ngazi hivi karibuni huku watuhumiwa wenzake wawili Edward Lowassa na Andrew Chenge wakipewa mwezi mmoja kujivua gamba kabla ya kuvuliwa.

Ingawa CCM ima kwa maksudi au bahati mbaya ilikuja na majina matatu kati ya mengi yaliyoorodheshwa na wapinzani kule Mwemba Yanga ya Septemba 15, 2007. Wengi hadi sasa hawajajua vigezo vilivyotumika kuwalenga mafisadi watatu kati ya wengi. Hata hivyo, idadi ya mafisadi imekuwa ikiongezeka ingawa watajwa hawajashughulikiwa. Mnamo tarehe 17 Aprili 2011, Dk Wilibrod Slaa, Katibu mkuu wa CHADEMA ambaye ndiye aliyetaja kundi la kwanza la mafisadi, alipanua orodha ya mafisadi wa awali kwa kuongeza wengine wapya.

Yeye badala ya kuwa humu ndani kusikiliza bajeti ya wizara hii, amekuwa akihangaika huko kutafuta watu ili aende kuwakatia maeneo na kuyauza huku akisingizia Rais Kikwete ndiye ametoa amri ya kuuzwa kwa ardhi husika.

Ukichunguza kwa makini, mafisadi au magamba yanayoisumbua CCM si yale tu yaliyotajwa na Dk Slaa tu. Kwa mfano, makamu mwenyekiti wa CCM taifa Pius Msekwa hakuwahi kutajwa kwenye orodha mbili za mafisadi zilizotolewa na ufisadi ingawa anadaiwa kuwa amekuwa akifanya ufisadi tena kwa kiwango cha juu.

Hivi karibuni msemaji mkuu wa kambi ya upinzani kwa wizara ya Maliasili na Utalii, Peter Msigwa CHADEMA alinakiriwa na vyombo vya habari akimueleza Msekwa ifuatavyo:

"Kambi rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya Mwenyekiti huyu wa bodi mara moja kwa kukiuka mipaka ya majukumu yake, tunaahidi kuwa tupo tayari kuipa Serikali ushirikiano kuhusiana na tuhuma hizi,” Muhimu, hapa mwenyekiti anayezungumziwa ni Msekwa.

Shutuma za ufisadi dhidi ya Msekwa hazikutoka kwenye kambi ya upinzani tu bali hata kutoka chama chake kama alivyokaririwa Mbunge wa Ngorongoro, Kaika Terere (CCM) akisema kuwa Msekwa amekuwa akiitumia bodi kufanya mambo yenye mwenyewe ambayo ni kinyume cha taratibu za Bodi ya Ngorongoro.

Alisema Msekwa aliidhinisha ujenzi wa hoteli yenye hadhi ya nyota tano katika hifadhi ya Bonde la Ngorongoro ambapo hata wenyeji wa pale walikatwa kupitisha mifugo yao.

Telele alisema, "Rais gani anaweza kukubalina na uuzaji huu? Kama ni kweli amebariki, basi hatuwezi kukubaliana naye katika uamuzi wa kuharibu na kuiuza hifadhi ya Ngorongoro,"

Telele alitaka iundwe tume ya kuchunguza bodi ya Ngorongoro kutokana na mambo mengi yanayofanyika ambayo ni uvunjifu wa sehria na katiba.

Wengi wanangoja kuona CCM itamchukulia hatua gani kigogo wake huyu wa ngazi ya juu ambaye amewahi kushika nyadhifa nyingi ikiwemo ukatibu mkuu wa CCM, spika, uwaziri, ukuu wa mkoa na sasa umakamu mwenyekiti. Huyu si dagaa bali papa kwa viwango vya kitanzania. Ajabu ni kwamba ni huyu huyu Msekwa alikuwa akiwaita watuhumiwa wenzake kuwataka waachia ngazi yaani kujivua gamba kabla ya kuvuliwa. Je yeye atavuliwa lini? Bila CCM kujibu swali hili kwa kumshguhulikia mhusika, kelele zote za kujivua gamba zitaishia kuonekana kama danganya toto huku mchezo wa kulindana ukiendelea kama kawaida. Wengi wangetaka kuona Msekwa akivuliwa gamba hata kesho ili angalau haki ionekane imetendeka.

Pia, baada ya kufichuka kwa uchafu wake, Msekwa ameonekana mnafiki mbele ya jamii. Wengi wanashangaa alipata wapi ujasiri wa kuwataka wenzake waondoke au wajivue gamba wakati naye analo lake? Je ni kwa sababu yake yalikuwa hajafichuka? Je wako wangapi wanaoonekana kung’ara wakati ni wachafu kuliko hata wale wanaowanyoshea kidole?

Hata ukimwangalia rais Jakaya Kikwete ambaye alitajwa kushiriki na kunufaika na wizi wa EPA, utagundua kuwa hana udhu wa kumwajibisha yeyote. Je hii ndiyo sababu ya Kikwete kuchagua baadhi ya mafisadi na kuwaacha wengine? Je kwanini kulenga mafisadi watatu kati ya wengi waliomzunguka kama Msekwa? Je Msekwa anatuma na Kikwete kama alivyobainisha mbunge Telele kuwa huwa anasema ametumwa na rais? Mbona Kikwete hakanushi kama kweli auhusiki na ufisadi na hujuma hii?

Ukiachia orodha ya Dk Slaa, kuna magamba mengine mapya yaliyofichuka hivi karibuni. Hawa si wengine bali Idd Simba, Didas Massaburi. Hawa nao ni magamba yanayopaswa kuvuliwa haraka hasa ikizingatiwa walivyohujumu lililokuwa Shirika na Usafiri Dar es salaam (UDA).

Tuhitimishe kwa kuwahimiza wananchi wasiendelee kutoa nafasi kwa rais Kikwete kumaliza muda wake huku akiwa ndiye anashutumiwa kuwa kinara wa ufisadi hasa kwa kushiriki na kuwalinda. Wakati wa kumwambia Msekwa wazi wazi kuwa anapaswa kujivua au kuvuliwa gamba ni huu. Bila kufanya hivyo tutaendelea kuchezewa kana kwamba hatuna akili kama umma na jamii.

Chanzo: Tanzania Daima Agosti 24, 2011.

3 comments:

Anonymous said...

Watch nude girls on WebCam..
Sign-up now free.
[url=http://tinyurl.com/signup-free-cams][img]http://wm.mtree.com/images/banners/sm/sm_300x250_01.gif[/img][/url]

Anonymous said...

What a fuck is dog? Who wants to watch nude girls? Go watch your nude mother and sisters may be you will screw them then go watch your nude dad and give him a fuck.

Jaribu said...

At least naona jamaa wa CCM wanapita hapa kujihabarisha, ingawa inabidi wa-improve uandishi wao.