The Chant of Savant

Thursday 18 August 2011

Tanzania ni sanaa sanaa hadi kiama


The Qatar Emiri Air Force plane through which nearly 140 animals from Tanzania were smuggled from the Kilimanjaro International Airport in November, 2010. (Guardian)


Baada ya kufumka kashfa ya usafirishaje haramu wa mamia ya wanyama kwenda Uarabuni yaliyofanywa na vigogo waliomo serikalini eti serikali inapiga marufuku usafirishaji wanyama nje! Yaani baada ya wao kusafirisha wanyama na kupata dola zao ndipo wanatuletea usanii wa kupiga marufuku usafirishaji wanyama! Hii ni sanaa maalum ya ufisadi na kujitoa kimasomaso. Je watanzania waathirika wako wapi?

Huwa napatwa na majonzi na mshangao kusikia watanzania wakimsifia rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi mwanzilishi wa ufisadi huu pale alipomleta brigedia Ali toka Falme za Kiarabu zama za kashfa ya uuzwaji wa Loliondo. Nani mara hii kawasahau majambazi wakubwa wakiongozwa na mkurugenzi wa wanyamapori wakati ule Muhidin Ndoranga? Nani kasahau kugundulika kwa njama za akina Zakhia Meghji na Seif Khatib waliokuwa wamejigawia miraba ya uwindaji?

Watanzania waguswe wapi ndipo wastuke na kufanya kweli? Kama wengine wameridhika sisi haturidhiki tutazidi kupiga kelele. Tunaamini kuna siku kitaeleweka. Je watanzania wameamua kutochukua hatua kutokana na ukweli kuwa kila mtanzania ni fisadi? Maana ufisadi sasa imekuwa sera na sheria vilivyobarikiwa na watawala na watawaliwa. Saa yetu ya UKOMBOZI itafika lini kufichua yanayofanyika NYUMA YA PAZIA? Mie sielewi. Kituko ni pale waziri mhusika na kashfa hii Ezekiel Maige kumsimamisha kazi mkurugenzi wa wanyamapori wakati naye ni mtuhumiwa na mhusika mkuu!
Kwa kituko hiki SOMA HAPA.

No comments: