Saturday, 3 May 2014

Kingozi wa ANC wa kihindi anapowaambia wahindi kwenda India


Visvin Reddy , diwani wa zamani wa African Natinal Congress (ANC) nchini Afrika Kusini ametoa mpya kwa kuwataka wahindi wenzake wanaolalamikia serikali kufunga virago na kurejea kwao India kama wanadhani huko kuna maisha mazuri. Aliwaonya waache kujitenga na ubaguzi wachangamkie demokrasia badala ya kulalamika. Ameacha wengi wakizidi kulalamika kwa kuwapa ukweli ulio wazi kuwa maisha yao Afrika Kusini ni bora kuliko huko wanakodhani ni kwao. Je ni wenzetu wangapi wanaouona ukweli mchungu kama huu alioupasua Reddy? Je hali ya hawa wenzetu barani ikoje? Waliokuwa wanashangaa kuona jamaa hawa wanavyokimbilia Afrika na kwingineko kama wakimbizi wa kiuchumi wanaweza kupata picha halisi hapa. Matamshi haya ambayo yameonekana kuwa ya kibaguzi licha ya kuwaudhi wengi, yamekilazimisha chama cha ANC kujitenga na kada wake. Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.

No comments: