Tuesday, 11 April 2017

Mpayukaji anapogeuka mwimbaji rap

makondaa

I vividly see it coming
Yes, it is truly coming
I can hear people fervidly yelling
Yes, I see them surreptitiously infuriated
The time is coming
When everything
Is going to be alarming
I see it coming
Yes, it is indeed coming
Bashite is packing
Yes, he will be soon going
 Mr Biggie must be thinking
To justice being done.
            Kwa wasiojua kitasha tusameheana. Kimsingi, kinachoongelewa ni kwamba ngome zitaanguka au kwa kinyasa ndoga ziyawa zawelale. Maana ngoma hii ilivyochefua na kutega wengi, nani alijua kuna ambao wangeramba matapishi yao na kuisifia na kudai wanaipenda wakati waliiponda?
Tokana na wengi kujiingiza kwenye mambo ya rap, nami kama Mpayukaji mtakatifu na mkuu nimeamua kutia timu lau nisikike hadi wahusika waipate kama siyo kunipata. Siogopi kufungwa hata kuzodolewa. Hapa lazima niangushe mistari lau ujumbe uwafikie wahusika. Guess what. Baada ya Nay wa Kutega kuwatega wakategeka, nami ameninasa kiasi cha kuvamia kunga kama si fani. Hapa lazima nifunge nyama ili farasi wafungiane nyama na nyangwa. Naweza kuonekana kijana wa zamani, ila bado ninayo mapya tena mapya kweli yanayowakonga roho wanene.
Japo si mpenzi wa ma-rap na marapu rapu tokana na kelele zake ukiachia mbali wanaoyatoa kuonekana kama hamnazo japo wanazo, huwa sipendi miziki hii. Lakini tokana na wimbo wa Wapo, nami nimejikuta nipo. Hivyo kuja na vimbwanga hivi uvisomavyo.
Ngoja nirejee wimbo ulionikuna kiasi cha kunisukuma kuvamia fani isiyo na wenyewe.
Naanza kushuka hivi:
A free hunk that’s never enjoyed freedom
Yes, it’s the hunk of doom
Vroom
 Acha niimbe kwa kimakonde
Nasema wapo
Wapo yes wapo
Tena wapo wapo
Wapo hapo hapo
Nasema wapo na kweli wapo
Wapo wanaoburuzwa
Sema wapo
Wapo wanaoburuza
Sema wapo
Wapo wanaojishebedua
Sema wapo
Wapo wanaoogopa kukosolewa
Sema wapo
Wapo wanaojua jua hata kama hawajui
Sema wapo
Wapo wanaobangaiza
Sema wapo
Tena wapo wateule
Sema wapo tu
Wapo wanaojigonga
Sema wapo
Wapo tena wengi
Wapo akina Bashiiit
Wapo tena sitawashit
            Kwa wasioinyaka, huu ni usawa wa kupenda rap. Mimi ni nani iwapo hata mzee M7 siku hizi ni rapper? Mimi ni nani nisiwape rap. Do you need more rap? Tell me. Do you need more rap?
            Naona yule anatikisa kichwa akidhani nafanya yote haya tokana na kanywaji au bangi.  Ushindwe. Kama hujaelewa somo basi umekwisha. Hujui kuwa baada ya jamaa wenye mabavu kutaka kila mchovu anyamaze, tumegundua namna ya kuwapa vipande vyao? Kama si rap, nani angewashikisha adabu akina Bashiit hadi wakajipiga mtama na kuramba matapishi yao? Ukisikia wapo wanaoramba matapishi na kujipiga ntama jua wapo? Nikisema wapo nawe jibu wapo.
Wapo walioanza kuharibikiwa, jibu wapo.
Wapo wanaochezea nafasi zao kwa kulinda makapi, sema wapo.
Wapo wanaojifanya miungu watu, sema wapo, wapo wanaojifanya wanajiamini wakati ni woga wa kawaida, sema wapo.
Wapo wanaofikiri kinyume, sema wapo.
Wapo walioghushi vyeti, sema wapo.
Wapo wakiulizwa  wanasingizia mihadarati, sema wapo.
Wapo akina Dav Bashite, sema wapo.
Wapo  waliojisahau, sema wapo.
Wapo wanaopinga kila kitu, sema wapo.
Wapo wanaochuuzana, sema wapo.
            Hebu tuache utani. Kwanini tusiwashauri wapingaji kugeukia rap ili hoja zao zisikike na kuheshimiwa. Maana baada ya kuona akina Rema wakipotezewa muda lupango, kuna haja ya kutafuta mbinu nyingine ya kupeleka ujumbe. Najaribu kupiga picha mzee Freeperson Mbhowe akiwa kwenye gwanda lake akila mic na mzee Sugu huku Joni wa Nyika na Tunda Lisssu wakimwaga vibwagizo kabla ya mzee Eddie Ewassa na Freddie Sumuye wakimwaga mistari ya kiutuuzima. Ngoma itanoga pale mzee wa Madevu kutoka mitaa ya Uondwe akimwaga vina kwa chati kabla ya mzee Ibra Pumba kumtungia mipasho ya kumpinga.
            Hebu jaribu kupiga picha dokta wa Majibu akimwaga vina kuwapasha mashakunaku kuwa wanapenda udaku na kujadili watu badala ya masuala akaishia kufanya hilo hilo analowashitakia wenzake. Kabla ya ngoma kutua piga picha bi nkubwa Sammie akisuluhisha kwa kumwaga vina vya kutaka kila mmoja aheshimiane na mwenzake huku brother Katelephone Aliyejaliwa akija na mistari ya Faru Joni kabla ya dokta wa Kusheini kuja na mistari dhidi ya jamaa mwenye madevu. Mwisho wa yote ni pale walevi wakatapoingia na mistari yao kusema wamechoshwa kuburuzwa na kutishwatishwa wakati kaya hii ni yetu sote bila kujali ukubwa wa cheo cha mlevi.
            Napiga picha walevi wakiimba
“Tunataka kaya yetu, tunataka.
Tunataka uhuru wetu, tunataka
Tunataka tuheshimiwe, tunataka.
Tunataka Bashite awajibishe, tunataka.
Tunataka haki na usawa, tunataka.
Tunataka walioghushi watumbuliwe, tunataka.
Tunataka makaburi yafukuliwe, tunataka
Tunataka tuyafunike wenyewe, tunataka.
Tunataka tunataka tunataka demokrasia na heshima, tunataka.
            Naona sauti imekauka hadi kuhitaji kanywaji. Lo! Hata kumbe sijapata majani lau nitulize kichwa na kuondoa mawazo yatokanayo na kadhia ya akina Bashite!
Chanzo: Tanzania Daima Jumatano kesho.

No comments: