How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Sunday, 12 September 2010
Siku kunguni walipowanyima usingizi wakanada
Inaaminika kuwa kunguni ni adha na dalili za umaskini. Lakini hali si hivyo hapa Kanada ambapo kunguni wanaonekana kuwanyima usingizi wanasiasa kiasi cha kulalamika. Je hili lingetokea uswekeni wenye pesa zao wangesemaje? Tungeona ma-TX wa kutuhubiri juu ya usafi na mambo mengine kama hayo huku watawala wetu omba omba wakiomba misaada ya haraka kuteketeza balaa hili. Tungeambiwa huu ni ugonjwa wa maskini. Leo watasemaje jamaa zetu hawa? Maana kwa ujumla Kanada haina maskini kwa maana ya neno.
Michael Colle wa Chama cha Liberal alikuwa na haya ya kusema: "Inakatisha tamaa. Watu wananiambia kuwa hawawezi kulala na ni gharama na hawajui la kufanya na kipi kitawasaidia,"
Mamlaka za tiba za jiji la Toronto zimekiri kuelemewa na tatizo la kunguni. Kunguni jike, mdudu mwenye ukubwa wa milimeta sita asiyeruka ana uwezo wa kutaga mayai kuanzia 200 hadi 400 katika kipindi chote cha uhai wake. Kwa sasa kunguni ni tishio kwa wenye majumba na biashara kadhalika.
Tatizo haliko Toronto tu. Majimbo mengine kama Quebec na British Columbia yameishalalamika. Nashukuru Mungu kwenye jimbo langu hawajafika nami nikaipata fresh.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment