Tuesday, 21 September 2010

Salma Kikwete Imelda Marcos wa Tanzania


Ridhiwan akifanya mazoezi ya kuwa rais. Chini yake ni bi mdogo wa mzee akifuatiwa na Ridhiwan akikagua gwaride la machinga wa kesho ambao wametengenezwa na utawala wao na kufuatiwa na Imelda Marcos wa Bongo akilakiwa na mkuu wa mkoa wa Dodoma kabla ya kukagua vikundi vya ngoma kama mpendwa chaguo la Mungu mzee Marcos mwenyewe bila kusahau mauzauza (Risiti) za Kinana.
Mauzauza ya Kinana

Je risiti hizi ni halali?

Baada ya kuwa tunalalamikia matumizi mabaya ya pesa ya umma na madaraka hasa kuhusiana na jinsi mke wa rais Salma Kikwete anavyoliibia taifa, Chama Cha Mapinduzi, juzi, kilijikosha kwa kutoa risiti za kukodi ndege ya bi mkubwa.

Kama risiti, hata kama zinatia shaka, zinavyoonyesha, ndege ya bi mkubwa inalipiwa dola za kimarekani 3,000 kwa saa! Kwa kazi gani ya mno kama siyo ulimbukeni, upenda raha na kutafuta per diem. Ajabu mama huyu mpenda raha na pesa anapokwenda mahali hupokelewa kama mkuu wa nchi! Je ni yale ya mbwa wa mfalme kuwa mfalme wa mbwa wote?

Huyu ndiye mama aliyewahi kuwaongopea wanawake wa Tanzania eti aliwahi kunyanyaswa akijifungua bila kutaja lini wapi na nani walimdhalilisha eti wakati mumewe akiwa waziri wa mambo ya nchi za nje. Hivi kweli huyu ana uchungu na wanawake wa taifa hili au kuwatumia kama majuha kupata mradi wake?

Hapa hatujaongelea pesa inayotumiwa kumkodishia ndege mtoto wa rais Ridhiwan Kikwete anayezurura kama mama yake kila uchao mikoani. Sasa kama Kikwete ameamua kutumia familia yake kupiga kampeni hii maana yake urais wake ni kwa ajili ya familia na si watanzania kama anavyowahadaa. Leo Ridhiwan akikuchukia chamani ujue utaondolewa taka usitake. Rejea yaliyowakuta Hussein Bashe na Hamad Yusuf Masauni walipotofautina naye. Interestingly, alimtuma baba yake kufanya kazi hii chafu. Je hapa rais kati ya Ridhiwan na Jakaya ni nani?
Je huu si ufalme wa nyuma ya pazia? Bahati mbaya hata mfalme mwenyewe yupo yupo kama kibonzo. Anatumiwa kwa remote control na kila aina ya wapuuzi kuanzia shehe Yahya, Lowassa, Rostam, Makamba na wengine! Je huyu bado anafaa kuwa rais wa nchi kweli? Jamani tuondolee hii aibu kwa kumnyima kura lau liwe somo kwa wababaishaji wengine.

Niliwahi kuhoji mantiki ya Salma kutambulishwa kama mwenyekiti wa shirika lake la ulaji la WAMA ilhali akipigia kampeni CCM. Nimekuwa na ugomvi na mama huyu muda mrefu kiasi cha kumuandikia mara kwa mara.

Haiwezekani kulala kitanda kimoja na rais kutumiwe kutufilisi. Hapa hatujaongelea nyumba ndogo ya Kikwete iendayo kwa jina la Rahma Kharoos.
Tufikie mahali tukatae upuuzi huu. Je muda ambao tumekuwa tukimuona Salma akizurura kila mahali ameishatumia dola ngapi na zingeweza kuwasaidia kina mama wajawazito au watoto wa kike wangapi? Ni unafiki na ufisi kiasi gani?

6 comments:

Anonymous said...

Mbona bi mdogo hasaidii kampeni ya kikwete?

NN Mhango said...

Bi mdogo anasaidia kupitia kujifanya mnadhimu na mfadhili wa michezo. Tafuta habari zake utajua ninachosema.

Anonymous said...

Kumbe wabongo wengi hawajui kuwa rais wao ni kiwembe wa kunuka! Huyo Rahma cha mtoto. Mbona kuna Mkuu wa wilaya wa zamani wa Masasi anayejulikana ni nyumba ndogo yake? Huyu jamaa hafai. Hili jimama limewekeza kwenye madini kwa kutumia ngono yake na Kikwete

Anonymous said...

Wow! I did not know Kiwete is garbage president who is supposed to be hanged just like any rapist, thief and fisadi. Fuck you Kikwete and your gang of thieves.
Nkwazi, tafadhali usizime ujumbe huu najua jamaa au jamaa zake wanakusoma sana. Kikwete ni laana kwa taifa na hapaswi kuchaguliwa tena au kuruhusiwa kuiba kura zetu kama alivyozoea.
Fuck you Kikwete and your gang of criminals especially Edward Lowassa, Rostam Aziz, Yusuf Makamba, Ridhiwan, Salma, Rahma, Ben Mkapa, Anna Mkapa, Salva Rweyemamu, Tido Mhando etc.

Anonymous said...

We sale online generic valium online. Order valium now! http://osdir.com/ml/scsi/2003-11/msg00063.html buy valium. The good quality.

Anonymous said...

UK Financials Ltd offered Bad credit tenant loans having Very low Rate of interest Bad credit profile is usually a could require there are factors to consider plus compromises to generate payday advance in 1 hour 500), in addition to promises to pay it off within a thirty day period (or when the next pay out cheque happens