Wednesday, 29 September 2010

Tumepata KAPAYUKAJI


Baba akiongea na mwana
Mama akimhusia mwana
Wapendwa wasomaji wangu,
Naomba nichukue fursa hii kuwataarifu kuwa familia yetu imepata mtoto wa kiume (pichani) aitwaye NKUZI (Kapayukaji) mnamo tarehe 25 majira ya saa 2:51 za Manitoba. Kwa Tanzania ilikuwa saa ilikuwa ni saa 11:51 alfajiri. Kichanga chetu kilizaliwa Boundary Trails Medical Centre, MB.
Mama mzazi, Nesaa Nkwazi Mhango na kichanga wanaendelea vizuri.
Nimeona niwafahamishe kutokana na ukaribu uliojengaka baina ya wasomaji wangu nami na bila shaka na familia yangu.
Chanzo: Mhango Family Libarary.

12 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Mpayukaji. Hongera sana kwako na familia yako kwa kutuletea kapayukaji kengine katakakoendeleza harakati.

Mungu Akabariki na nyote nawatakieni mibaraka, furaha na amani katika kipindi hiki cha furaha. Blessings!!!

Mbele said...

Hongera sana na kila la heri.

NN Mhango said...

Walimu wenzangu na ndugu zangu Masangu na Mbele siwezi kuelezea furaha yangu kutokana na kasi yenu ya mawasiliano na dua zenu. Ni kweli nina furaha kupata mshika kijiti huko tuendako. Najumuika nanyi kama ndugu. Maana ndugu si kufanana bali kufaana. Nawashukuruni kwa kunitumia salamu zenu za dhati kabisa.

Malkiory Matiya said...

Hongera mkuu Mhango kwa Copyright! Hakika huyo amekuja wakati mwafaka wa uchaguzi mkuu! huyo bila shaka atakuwa mpiganaji wa kweli.

Yasinta Ngonyani said...

Hongereni sana na Mungu awabariki na pia nawatakieni baraka , furaha na pia amani katika nyumba yenu. Na pia awape nguvu za malezi kwa hyuyo mpayukaji

SIMON KITURURU said...

Hongera sana Mkuu!

NN Mhango said...

Nawashukuruni nyote mliotutumia salamu za pongezi na mbarikiwe sana.
Kwa niaba ya familia yangu,

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

hongera sana kwa kukaleta 'kapayukaji' kengine....nyote mbarikiwe sana!

NN Mhango said...
This comment has been removed by the author.
NN Mhango said...

Mt. Kitururu, Ngonyani,Malkiory na Ng'wanambiti nawashukuruni kwa kuwa nami katika ujio huu wa Kapayukaji.
Mungu awazidishie upendo na afya.
Kila la heri ndugu zanguni.

Anonymous said...

Hongera sana, Mwenyezi Mungu amjalie mtoto afya njema pia ninyi wazazi mdumu katika nia moja ya kumlea katika maadili mema.......amen

Tecson said...

Mpayukaji. Hongera sana kwako na familia yako kwa kutuletea kapayukaji kengine katakakoendeleza harakati. Mungu Akabariki na nyote nawatakieni mibaraka, furaha na amani katika kipindi hiki cha furaha. Blessings!!!