Monday, 13 September 2010

Karibuni tutashika bomba kwenye pipaHizo ndizo zana mpya za kushikia bomba kwenye pipa. Bado wapiga debe nao kuajiriwa.
Kampuni moja ya kitaliano iitwayo Avioninteriors imekuja na mpya ilipobuni siti za kusimama kwenye ndege ili angalau wale wachovu kama mie nao waweze kupanda pipa kwa bei nafuu. Hapo juu ni viti vya kusimama au tuseme kushika bomba au SkyRider kama wao waviitavyo.

Zana hizo za kushika bomba kwenye pipa zilionyeshwa juzi miezi michache baada ya mkurungezi wa Ryanair, Michael O'Leary kusema kuwa shirika lake lilikuwa na mpango wa kuanzisha huduma ya kushika bomba kwenye pipa.

Hata hivyo sijaelewa. Hivi kweli itawezekana kwa mfano mtu kushika bomba toka Bongo hadi Marekani au toka Ujepu hadi Kanada hii?
Yetu macho.

No comments: