The Chant of Savant

Friday 6 May 2011

Siku nilipokiona kifo kinakuja

Hapa naangalia madhara mke wangu alipokuja kunichukua toka kwenye eneo la ajali
Hapa ni eneo la ajali ambapo mke wangu anaangalia madhara kwenye eneo la tukio asiamini


Wapendwa wasomaji nachukua fursa hii kumshukuru Mungu kuwa leo nimenusurika kwenye ajali ya barabarani ambapo gari langu limepinduka na kubiringika kama mara tano. Nimetoka mzima bila mchubuko wala maumivu. Ni muujiza.

21 comments:

Mbele said...

Pole sana. Kweli ilikuwa ajali mbaya. Mungu ni mkubwa, kakupisha salama.

Ingawa huenda hujisikii maumivu mara baada ya ajali, ushauri ambao nimewahi kuusikia hapa Marekani ni kuwa ni vema kumwona daktari kwa uchunguzi zaidi. Pole sana, na nakutakia kila la heri.

Mwanasosholojia said...

Dah!Pole sana mkuu!Ama kwa hakika huu ni muujiza, maana mara tano si mchezo..kutoka salama ni uthibitisho tosha kabisa kuwa bado mchango wako unahitajika hapa duniani..endelea kuitumia vyema nafasi hii kwa kutekeleza majukumu yako bila hofu. Pole tena ndugu yangu.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Kaka Mbele kwanza habari za siku nyingi? Je ulishamaliza kusoma kitabu changu? Ushauri wako ni wa kweli. Baada ya kutolewa pale brake ya kwanza ilikuwa ni hospitali ambako nilikaa kama nusu saa ili kuhakikisha kila kitu ni sawa. Baada ya hapo nilikwenda polisi na kutoa taarifa. Baada ya hapo niliwasiliana na watu wangu wa bima. Kutoka hapo niliwataarifu wenzangu ninaowajibika nao.
Kweli Mungu ni mkubwa. Maana nilipotoka sikuamini kuwa nilikuwa mimi na bila hata kovu. Kwani nilipokumbuka msisukosuko ya kubingirika utadhani nimezama baharini, iliniwia vigumu kuamini.
Kwa vile ni wikendi, nimejipa mapumziko ya muda japo si kwenye kuandika na kusoma ili lau ninywe bia yangu aina ya Faxe Royal toka Denmark taratibu.
Kaka nakushukuru sana.
Mwanasosholojia asante nawe pia. Sina jinsi ya kuwashukuru kwa kujali kwenu. Mungu awalipe kwa ajili yangu.

Jaribu said...

Pole sana, yahe. Mimi nishapata ajali nyingi ndogo ndogo, nothing serious kama kupinduka. Enjoy hiyo bia, maana trauma ya mawazo itakukaa kwa muda hivi.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Mie ngangari ndugu yangu Jaribu. Hata wife mpaka sasa haamini kuwa nimeponyoka na anadhani napata hii kitu kumzuga. Lakini ukweli ni kwamba niko mezani naandaa kijiwe cha jumatano kwenye Tanzania Daima na makala za magazeti mengine.
Nakushukuru ndugu yangu Jaribu kwa kunijulia hali. Hii kitu ilikuwa kali kweli maana nilikuwa ni kama naogelea vile.

Subi Nukta said...

Pole sana kwa ajali kaka Mhango.
Picha za ajali hii zimenistua sana, nimemwita rafiki yangu nikamwonesha ikabidi tumshukuru Mungu kwa pamoja kwa ajili yako baada ya kukumbukia ajali nyingine na madhara yanayotokana nayo. Naungana na Prof. Mbele na ninashukuru kuwa umefika ER na kupata huduma ya awali ya uchunguzi. Hata kwa siku zinazofuatia, ukijisikia maumivu kokote, usisite kwenda ER tena kwa kuwa mara nyingine viungo vya ndani vinaweza kudhurika lakini isioneshe kwa uchunguzi wa haraka (x-Ray, CT, MRI etc). Pole sana!

Yasinta Ngonyani said...

Pole, Pole SANA kaka Mhango kama wengine walivyotoa ushauri ni kweli NI MUHIMU SANA KUMWONA DAKTARI na kufanya (X-ray.) POLE SANA.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Da Subi na Da Yacinta nawashukuruni pia kwa sala n maombi yen. Ni kweli ajali inatisha ila wakati mwingine siku kama ndiyo imefika huna ujanja. Maana hata nami kutoka salama ndani ya kajeneza kale haukuwa ujanja bali Mungu mwenyewe.
Nitazingatia ushauri wenu na inshallah tuzidi kuombeana heri.
Kila la heri.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Mwalimu. Pole sana. Mimi pia niliwahi kubiringika na gari nikitoka Los Angeles kwenda San Francisco usiku. Yaani ilikuwa ni kama vile kwenye muvi. Kwa vile nilikuwa nakwenda mwendo kasi basi gari lilibiringika zaidi ya mara sita na kwenda mbali kabisa ya barabara. Ajabu ni kwamba nilitoka nikajiangalia na sikuwa na hata mkwaruzo mwilini. Ajabu zaidi ni kwamba kama ajali hii ingetokea mbele kidogo tu sijui ingekuwaje kwani kulikuwa na milima na makorongo ya hatari. Mungu ni mkubwa.

Kama alivyosema Mwalimu Mbele, polisi walikuja na wakaita gari la wagonjwa. Hospitalini nilifanyiwa vipimo vyote na nikaonekana niko sawa.

Samahani kwa kuingiza hadithi yangu hapa lakini ni mkasa unaofanana na wangu. Hadithi yangu inazidi kunoga zaidi kwani huko San Francisco nilikuwa nakwenda kumwona mchumba. Baada ya ajali hii basi nilimwambia kwamba "kwa vile nimepona kufa nikiwa nakuja kwako basi mi nakuoa kabisa". Na leo ni zaidi ya miaka 10 tukiwa kwenye ndoa ya furaha na amani. Mipango ya Mungu!

Pole sana na hongera kwa kutoka salama. Mungu Angali Anakuhitaji ili uendeleze harakati.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Asante sana bwana Matondo na pole sana kwa kupitia niliyopitia. Pia hongera kwa kunusurika.
Tofauti yako nami ni kwamba nilikuwa nakwenda nhyumbani toka kwenye chaki. Hivyo sijui nami nioe chaki sana au?
Otherwise ni experience ya aina yake. Maana miaka 16 iliyopita nilipata ajali ya pikipiki na kutoka bila jeraha. Nilichofanya ni kuiuza na kuachana na kichaa cha pikipiki. Kwa wanaonijua nilikuwa napenda sana mapikipiki makubwa sana. Lakini tangu siku hiyo sijawahi kupanda pikipiki hata kwa kupewa lift.Anyway ni maisha.Ni jambo la kumshukuru Mungu.

Anonymous said...

Mhango, pole na tumshukuru muumba. Lakini pia siku hizi lazima muwe makini wakati wa kununua hivi vigari - vi-ECHO vingine vinatengenezwa Uchina!!!!!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anonymous nakushukuru na kukubaliana nawe kuwa hivi vijeneza si vya kuamini. Huwa sipendi kukitumia hiki kidude. Lakini kutokana na kuwa na safari za kila siku karibu kilometa 200 za kwenda kuwajibika hujikuta mara nyingine najibana mafuta kwa kutumia hiki kipande cha mashine.
Hata shemeji yako mara nyingi huwa ananishauri nitumie gari kubwa. Mara nyingi huamini katika majaliwa ila nimepata somo.
Kinachouma ni ukweli kuwa vipanya hivi ni aghali ukilinganisha na magari mengi ya North America ambayo ni oil guzzlers.
Nashukuru sana ndugu yangu.

Anonymous said...

pole sana kaka Mhango ingawa tumechelewa kufika, lakini tumefurahi kusikia kuwa upo salama.usisahau ushauri wa kaka yetu pro mbele.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anonymous 11:48 nakushukuruni. Hukuchelewa ndiyo muda uliopata.Heri kuchelewa ukafika kuliko kukosa kabisa. Tuzidi kuombeana na ushauri wa kama Mbele niliishaufanyia kazi.

Anonymous said...

Pole sana Mpiganaji Mhango. Tunamshukuru mungu kwa kukuepusha na balaa. Malkiory Matiya.

malkiory said...

Samahani kwa kuingia kama anonymous, sikujua kama kuna option zingine hapa, maana nimeifunga google account yangu kwa sasa na nimehamia wordpress. www.malkiory.com

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

BWana Matiya,
Usijali sana kaka. Hii ndiyo faida ya kuwa na zana nyingi za kitekenolojia kila mara.
Nakushukuru kuwa kunijuliia hali na kunitakia uzima tele.
Kila la heri

Anonymous said...

Kama ni bongoland hapo hamna namna ni kwamba tu umelogwa au ni zengwe maana huku hamna bahati mbaya.

Pole sana, we have every good reason to thank God for your survival in that fatal accident.

Inshaaalllaahh utaendelea na vita ya kupambana na mafisi.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anonymous 06:14 nakushukuru. Ni kweli imani za uchawi na ushirikina zipo. Ukiweka kila kitu kwenye kipimo na miwani ya ushirikina huwezi hata kutembea bila kuhisi hofu.
Ndiyo namshukuru Mungu na nitajitahidi kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi kwani Mungu amenipa nafasi nyingine.
Kila la heri

uswazi said...

pole pole sana ndugu yetu. Samahani nimechelewa kidogo kukupa pole lakini nafikiri shock ya ajali itakuwa imepungua sasa. Naomba usiache kuandika, maana hii blog yako siyo mchezo! Pole sana.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Asante sana Uswazi.
Siwezi kuacha kuandika kwa vile huo ndiyo wito wangu.
Kila la heri,na haukuchelewa. Shock kweli imeishatokomea na naendesha kama kawa bila kujali. Maana imani yangu ni kwamba siku moja nitatoweka. Vipi? No one knows except the Creator.