How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Monday, 22 August 2011

Hivi rais kufuturisha siyo kufuja pesa ya umma?

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia baadhi ya wakazi wa mji wa Lindi waliohudhuria futari aliyowaandalia jana jioni mjini Lindi
Baadhi ya wananchi na viongozi walioalikwa katika futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanian Alhaj Dk Jakaya Mrisho Kikwete,wakichukua chakula katika utaratibu maalum uiloandaliwa huko viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.(21/08/2011)
Watu wakifaidi futari iliyoandaliwa na ubalozi wa Tanzania mjini London




Ingawa nchi yetu haina dini, watu wake wana dini. Hivi karibuni rais Jakaya Kikwete ameanzisha mchezo mwingine wa hatari ambao, kimsingi, ni kuchanganya siasa na dini. Amekuwa akifuturisha umati wa watu kwenye maeneo mbali mbali ya nchi. Ameishafanya hivyo Dar es salaam Mtwara na Zanzibar. Je ni halali kwa rais kutumia pesa ya watanzania waislamu wasio waislamu na wasio na dini kufuturisha watu wake? Je hii futari anayotoa rais anaitoa kama rais au mtu binafsi? Kwanini hafanyi hivyo nyumbani kwake badala ya ikulu? Je huu nao si ufisadi na matumizi mabaya ya pesa ya umma? Je watanzania wana shida ya futari au mambo mengine muhimu? Rais wa Zanzibar, mkewe hata ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza nao wanafuturisha! Kwa pesa ipi na ya nani na kiasi gani? Imefikia mahali futari imekuwa dhihaka kiasi cha wahusika kuwafuturisha hata wasio waislam!
Tunahoji maswali haya si kwa chuki na dini yoyote bali kutaka kuwepo uadilifu na ulinganifu katika matumizi ya pesa ya umma.

3 comments:

Anonymous said...

Hiki ni kioja kingine cha awamu ya nne.
Ni wazi kunamkakati wa kuwarubuni watu.
Bomu analolijenga kikwete hataondoka duniani kabla halijalipuka.
Bila shaka yeye na uzao wake watakuwa wahanga.
Time will tell

Anonymous said...

Tena futari yenyewe haijali ni mkristo au muislam. Huyu Prezidenti uchawara.Nimeona kawaleta na masista kufuturu. Mie sio kama mbaguzi wa dini bali hii ni siasa; anatumia pesa kuwarubuni watu kwa vijizawadi kama kawaida yake. Wape watu maendeleo na si chakula cha siku moja ni vimifuko vya vizawadi kama watoto. Aache siasa zake za kitoto kwanza ni kuwadhalilisha wananchi wake.

Anonymous said...

Waddau hapo juu mmenena. Kikwete ni kafiri tu hana uislam wala imani. Maisha yake ni ya kihuni kama alivyowahi kusema baba wa taifa Mwalimu Nyerere.