The Chant of Savant

Wednesday 3 October 2012

Mjue rais wa watu


Jose Mujica rais wa Uruguay ni mtu wa kutisha ingawa hana makuu. Nadhani ni rais pekee anayeendesha gari aina ya Gongo la Kobe au Volkswagen Beattle. Mujica haiishi hapo. Wakati marais wengi wakishindana kuiba na kujirundikia mali wao na familia zao, Mujica hutoa aslimia 90 ya mshahara wake kwa maskini. Ni rais ambaye urais wake una usalama zaidi kwa vile wanyonge wanamjua yeye ni nani kwao. Hata hivyo hakosi maadui hasa mafisadi na wapenda mali waliotamalaki dunia nzima. Je ni marais wangapi wanaweza kuvaa viatu vya Mujica?

1 comment:

Anonymous said...

wengi tuu Kikwete ni mmoja wao Kibaki Moi Bokasaa Museveni Idi Amin Ghadafy na wengi tuu