How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Friday, 19 October 2012

Vurugu za kidini je ni akili kumfia Mungu asiyekufa na mwenye nguvu?

Kinachoendelea nchini Tanzania ambapo vurugu zimeishatokea kinaelezewa kama vurugu za kidini. Je ni kweli ni chuki za kidini au kukata tamaa kwa watu wetu? Nimejaribu kujihoji na kuhoji mantiki ya mtu ambaye ni kiumbe dhaifu kuliko vyote kuwa tayari kuua hata kuuawa eti kwa ajili ya ima dini au Mwenyezi Mungu. Nashindwa kuelewa kutokana na ukweli kuwa Mungu hafi ila binadamu anakufa. Je hapa wahusika hawasemi ukweli kuwa wanapambana kupata maisha bora kwa wote kwa kutumia mgongo wa dini? Kama tutamfia Mungu asiyekufa yeye Mungu atafanya kazi gani? Kwanini tufie dini zake wakati mwenyewe yupo anaangalia? Je sisi ni vichaa na mataahira au ni wajanja wenye hoja fichi? Wanangu nataka maoni yenu lau tujadili jinsi ya kulielekea hili. Maana tukilinyamazia litalimaliza taifa letu.

3 comments:

Anonymous said...

mpagani leo anataka kuongea habari mungu.what is the point here

Anonymous said...

huyo hana lolote khasia zipo tokea majuzi alikuwa wapi amelala?

Anonymous said...

kweli akutukanae hachagui tusi
hivi unaongelea kitu gani mpagani
kama huna cha kuandika bora ufyate
ahh nipo kariakooo nangojea $$ kuelekea mwenge