The Chant of Savant

Monday 8 October 2012

Watawala ombaomba kwa kupenda ukubwa!

Watawala wa nchi ombaomba za kiafrika hawaishiwi vituko. Licha ya kujilipa mishahara na marupurupu lukuki wanapenda kuishi kwenye mahekalu wakati wale wanaowawezesha wakiishi mitaani au kwenye mbavu za mbwa. Hiyo hapo juu pichani ni nyumba yenye thamani ya shilingi  za Kenya 400,000,000 inayomaliza kujengwa kwa ajili ya makumu wa rais. Ajabu hao wanaopenda makuu na matumizi ya kijinga wamezaliwa kwenye nyumba za tembe. Hata wakiachia madaraka hurudi huko huko na wasidhurike. Je hapa tatizo ni kutokujiamini, roho mbaya, upogo au ulimbukeni?

No comments: