Rais Jakaya Kikwete akiwa amepanda kwenye gari la kukokotwa na farasi alipokuwa nchini Kanada kikazi. Pamoja na kuwasili kama mkuu wa nchi, Kikwete alipokelewa na waziri wa mambo ya nchi za nje badala ya waziri mkuu. Ingekuwa wakati wa mwalimu Nyerere huu ungekuwa mwisho wake kukanyaga kwenye taifa hili. Sijui ni kwanini viongozi wetu wa sasa wanatenzwa kama watoto wadogo?  Hii imenikumbusha ushabiki wa Kikwete kwenye kubembea kama ule aliofanya kule nchini Jamaica miaka michache iliyopita alipokwenda kule kujirusha.