Free Thinking

I Fear Nothing But Fear Itself

The Curse for Salvation

The Curse for Salvation

Saturday, 14 May 2016

Viapo vya akina Makonda vina uhalali kisheria?



            Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda aliwalisha viapo wakuu wa idara mkoani mwake kufichua wafanyakazi hewa. Huu ni utaratibu mpya ambao sijui unatoka kwenye katiba gani hasa ikizingatiwa kuwa kuna baadhi ya kada ya wafanyakazi isiyohitaji viapo inapoajiriwa. Je sheria za nchi zinasemaje kuhusiana na masuala kama haya? Je hivi viapo vina uzito na uhalali kisheria? Je walioviandaa wamezingatia sheria gani na mambo gani? Je viapo hivi vinaweza kuheshimika mahakamani kama waliovila watavivunja? Sijui kama kisheria viapo kama hivi–ambavyo bila shaka–havina mashiko kisheria vinaweza kutekelezwa mbele ya mahakama au kupata hadhi ya mkataba kisheria. Nasema hili ni jambo jema linalofanyika vibaya kutokana na kutokuwa na mizizi katika katiba yetu. Kulishana viapo kienyeji bila miiko inayoeleweka ya uongozi na utumishi wa umma ni kama kutapatapa. Hata huko makanisani wanapolishana viapo, huwa kuna kanuni na utaratibu vinavyoeleweka na kukubalika kisheria. Si hilo tu, kuna namna ya kisheria ya kutekeleza viapo hivyo na madhara yake vinapovunjwa kisheria. Rejesheni katiba mpya muepuka kusumbuka na kuhangaika jambo ambalo linaweza kutafsiriwa kama ombwe la sera jambo ambalo si jema kwa serikali iliyodhamiria kuleta mageuzi katika mfumo wa utawala wa taifa letu.

             Wengi wanashangaa sana namna ambavyo baadhi ya watu wanaweza kufanya mambo. Japo huu unaweza kuonekana kama ubunifu, bila kuwa na utaratibu maalumu kisheria, ubunifu unaweza kuonekana kama vurugu na hata ubabaishaji.  Inashangaza sana kufikia hatua hii hasa ikizingatiwa kuwa kulikuwa na fursa ya kurekebisha mambo na kuwa na utaratibu unaojulikana lakini watu wachache wakaifuja. Fursa hii ilijitokeza pale ilipoamriwa kukusanywa maoni kwa ajili ya kuandika katiba mpya ambayo watawala woga na wasio na udhu waliyapuuza na kuizika katiba ikiwa hai huku wakiwa wameitia nchi hasara ya fedha na muda. Ni ajabu sana kuona hawa wanaowaapisha wenzao ndiyo wanaosifika kuua katiba mpya ambayo bila shaka ingeondoa huu uoza kirahisi. Nchi haiwezi kuendeshwa kwa mipango na mawazo binafsi ya rais ua wasaidizi wake bali kanuni na sheria vinavyoeleweka na kukubalika kwa wananchi wote.  Leo Makonda anawalisha wakuu wa idara wa Dar es Salaam kwa kiapo fulani. Kesho atakuja mwingine na aina yake ya kiapo. Je hii haijawa vurugu na usumbufu kwa umma usio na mabavu ya kupinga wala kuzuia vurugu hii? Tunajua hawa wanaolishwa viapo hawawezi kufurukuta tokana na woga uliolikumba taifa hasa kutokana na wafanyakazi wengi kuzoea kufanya kazi kwa mazoea na kuvurunda kiasi cha kutoa nafasi ya mambo kama haya ya hovyo kufanyika.

            Ni jambo la hovyo na hatari kumwachia kila mkuu kwenye nafasi yake kujiundia utaratibu wa kuleta uwajibikaji. Kufanya hivyo–zaidi ya kuonyesha ombwe–ni vurugu na fursa ambayo inaweza kutumika vibaya. Lazima katika uongozi wa taifa, kuwe na vigezo na kanuni zinazofanana. Leo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam anajiundia kiapo chake. Kesho mkuu wa mkoa mwingine atafanya hivyo. Mwisho wa siku, tutakuwa na wafanyakazi wenye nyadhifa zinazofanana lakini waliolishwa viapo tofauti.  Ni vizuri tukafahamu na kukubali si watendaji wote wana ujuzi wa mambo ya kisheria wala si wote wanaoweza kuwa na utashi wa kuheshimu haki za wenzao hasa wakati huu ambapo kila mkubwa anajitahidi kumridhisha rais na si wananchi.

            Kwa wanaomfahamu mtu kama Makonda ambaye anasifika kwa kutenda kwa mabavu, watakubaliana nasi kuwa kama viapo vyake vitakiukwa–jambo ambalo ni la kawaida kwa binadamu–uwezekano wa kutoa huku zisizolingana na makosa ni mkubwa hasa ikizingatiwa kuwa viapo vya namna hii havina nguvu na uhalali kisheria. Kwa lugha nyepesi ni kwamba ombwe la kanuni na sera linaanza kuzaa vurugu bila sababu. Hivyo tunamtaka rais afanye yafuatayo:

            Mosi, akemee ujitwaliaji huu wa madaraka ambao unaweza kufanyika kwa kisingizio cha kuteleza amri zake. Pia hii inaweza kuonyesha kuchanganyikiwa kwa wahusika kiasi cha kufanya mambo kwa mazoea au hisia badala ya sheria.

            Pili, kuondokana na kadhia hii, rais anapaswa kuanzisha utaratibu wa kurejea kwenye katiba mpya akianzia pale tulipoishia baada ya katiba husika kuuawa kifisadi na kiwoga.

Tatu, rais atangaze utaratibu utakaofuatwa na muda utakaotumika kuipata katiba mpya ili kuepuka kupoteza fedha na muda zaidi kwenye jambo ambalo lilishakamilika.

            Nne, rais atangaze wazi wazi kuwa utumishi wa umma hufuata sheria zilizowekwa na hivyo uzingatiwe; na kama zinapwaya zirekebishwe ili kuepusha vurugu hii ya kimfumo. Haiwezekani mtu akaamka na kujichukulia uamuzi wa kufanya vitu vinavyofunja sheria akaachwa hata kama nia yake ni nzuri. Huwezi kutekeleza jambo zuri kwa njia mbaya bado likaendelea kuwa baya wala kufanya jambo baya kwa nia nzuri likawa jema.

            Tumalizie kwa kusisitiza kuwa serikali ianzishe utaratibu kwa watendaji wake kufanya mambo ndani ya sheria tena kwa sare kwa taifa zima badala ya kila mtu kujifanyia atakavyo. Kwani kufanya hivyo ni vurugu tupu. Nani anataka kuishi chini ya mfumo wa jazba, vurugu na ombwe?
Chanzo: Mwanahalisi.
Posted by Ndugu Nkwazi N Mhango at 05:57

No comments:

Post a Comment

Newer Post Older Post Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

Cordially and unlimitedly welcome to this blog.


Writing and reading are two different processes but which share the same goal-to educate, communicate and entertain.
It is my pleasure to have you as the guest of this tablet.
I, thus, warmly and always, welcome you to share ideas.
Importantly and eminently, shall there be anything amiss or you think can advance this blog, please donate it.
Allow me to humbly and kindly welcome you once again.
Nkwazi N Mhango- A Man And a Half

When wisdom brings no profit, to be wise is to suffer. Not all thoughts are good and constructive. Others are even worse than bullets. The good thinkers are the ones that think constructively for the manumission of all bin-Adams regardless their diversity. Mwl. Nkwazi N Mhango,
Canada.


Hail Mama SWAPO Nandi-Ndaitwah

Hail Mama SWAPO Nandi-Ndaitwah

I Love My Country Tanzania

I Love My Country Tanzania

The Curse of Salvation

The Curse of Salvation

Gen Z and Internet Revolution

Gen Z and Internet Revolution

I Cry for Ambazonia and Darfur

I Cry for Ambazonia and Darfur

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do.

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do.

Liberal Peace Conflict, Gender, and Peacebuilding

Liberal Peace Conflict, Gender, and Peacebuilding

Yoo-hoo, Africa Is Yowling

Yoo-hoo, Africa Is Yowling

The Story of Stories

The Story of Stories

The Chant of Savant

The Chant of Savant

AFRICA’S CONTEMPORARY FOOD INSECURITY Self-inflicted Wounds through Modern Veni Vidi Vici and Land G

AFRICA’S CONTEMPORARY FOOD INSECURITY Self-inflicted Wounds through Modern Veni Vidi Vici and Land G

AFRICA MUST DEAL WITH BLATS FOR ITS TRUE DECOLONISATION

AFRICA MUST DEAL WITH BLATS FOR ITS TRUE DECOLONISATION

Epistle to Afrophobic South Africa

Epistle to Afrophobic South Africa

Magufulification

Magufulification

BORN NUDE

BORN NUDE

Total Pageviews

Heko Rais Magufuli

Heko Rais Magufuli

DECOLONISING EDUCATION

DECOLONISING EDUCATION

Kudos President Magufuli

Kudos President Magufuli

JOKEY HORSE-JOCKEY NORTH-SOUTH RAPPORT Diagnostic-cum-Prognostic-Academic Perspectives on Who Truly

JOKEY HORSE-JOCKEY NORTH-SOUTH RAPPORT Diagnostic-cum-Prognostic-Academic Perspectives on Who Truly

The Family Friend of Animals

The Family Friend of Animals
Children's Book

Matembezi Mbuga ya Wanyama

Matembezi Mbuga ya Wanyama
Kitabu cha Watoto

Our Heritage

Our Heritage
Children's Book

How Africa Developed Europe:Deconstructing the His-story of Africa, Excavating Untold Truth...

How Africa Developed Europe:Deconstructing the His-story of Africa, Excavating Untold Truth...

Africa's Dependency Syndrome: Can Africa Turn Things around for the Better?

Africa's Dependency Syndrome: Can Africa Turn Things around for the Better?

'Is It Global War on Terror' or Global War on Terra Africana?

'Is It Global War on Terror' or Global War on Terra Africana?

Perpetual Search

Perpetual Search

Africa's Best and Worst Presidents

Africa's Best and Worst Presidents

Psalm of the Oppressed

Psalm of the Oppressed
Psalm of the Oppressed

AFRICA REUNITE or PERISH

AFRICA REUNITE or PERISH
A new approach towards empowering Africa

BORN WITH VOICE

BORN WITH VOICE

Soul on Sale

Soul on Sale

Soul on Sale

Nyuma ya Pazia

Nyuma ya Pazia

We are one

We are one

SAA YA UKOMBOZI

SAA YA UKOMBOZI

Feel at home

You are always welcome to this epistle again and again time after time, ad infinitum.


Most read Posts

  • Sarkozy’s Take on African Fat Cats a Welcome Move
    At last the chicken are coming home to roost! French authorities made a groundbreaking decision by culling three most corrupt African presid...
  • Napanga kuanza kuuza mitumba na si maneno
    Ingawa mimi si mtumba, napanga kuuza mitumba. Nimechoshwa na jamii ya mitumba. Kila kitu mitumba. Mitumba, mitumba mitupu. Siasa za mitumba...
  • Better or Bitter Life for all?
    When I deeply muse on how an arrogant and brutal cabal of hoity toity (Coverted Con Men (CCM)) is tirelessly hoodwinking and dividing the ho...
  • Africa's Becoming more Despotic and Nepotistic
    "King of Kings" Gaddaffi The seven-day 40th anniversary of Libya strongman’s autocratic rule and charade elections in Gabon where...
  • Kuna siku tutataifisha haya mahekalu haki ya nani
    Taarifa kuwa waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige alinunua nyumba kwa zaidi ya shilingi bilioni moja licha ya kuwastua wananchi na...
  • Nyangumi mdogo akutwa amekufa ufukweni BC
    Hii ni picha iliyotolewa ya Nyangumi aina ya Humpback ambaye alikumbwa na maji na kutupwa kwenye ufukwe wa bahari ya Pasifiki kwenye eneo l...
  • Kikwete, Charity Begins at Home!
    President Jakaya Kikwete Pea...
  • Kweli binadamu si chochote wala lolote, wamkumbuka huyu?
    Walioko madarakani mkiabudiwa kama miungu au sanamu kumbukeni vijana hawa hata baba zao  ambao maiti zao zinaoza jangwani. Ungewaambia...
  • Pinda kulia hakutoshi, awajibike
    INGAWA kilio cha Waziri Mkuu, Mizengo Peter Kayanza Pinda, kinaonekana kuyeyusha hasira za Watanzania kwa muda, kuna haja ya kudodosa zaidi....
  • Hawa si wachungaji bali ni fisi na mbwa mwitu
    KUMEZUKA mtindo mchafu na wa rejareja wa baadhi ya wachumia tumbo na matapeli kumtania hata kumtumia Mwenyezi Mungu kufanya utapeli na ujamb...

Followers

Blog Archive

  • ►  2025 (84)
    • ►  December (1)
    • ►  November (11)
    • ►  October (9)
    • ►  September (7)
    • ►  August (12)
    • ►  July (8)
    • ►  June (7)
    • ►  May (5)
    • ►  April (4)
    • ►  March (6)
    • ►  February (8)
    • ►  January (6)
  • ►  2024 (92)
    • ►  December (7)
    • ►  November (4)
    • ►  October (11)
    • ►  September (9)
    • ►  August (7)
    • ►  July (9)
    • ►  June (9)
    • ►  May (8)
    • ►  April (7)
    • ►  March (6)
    • ►  February (7)
    • ►  January (8)
  • ►  2023 (118)
    • ►  December (10)
    • ►  November (10)
    • ►  October (9)
    • ►  September (2)
    • ►  August (4)
    • ►  July (6)
    • ►  June (9)
    • ►  May (8)
    • ►  April (18)
    • ►  March (13)
    • ►  February (9)
    • ►  January (20)
  • ►  2022 (208)
    • ►  December (14)
    • ►  November (14)
    • ►  October (20)
    • ►  September (20)
    • ►  August (12)
    • ►  July (25)
    • ►  June (22)
    • ►  May (18)
    • ►  April (13)
    • ►  March (18)
    • ►  February (18)
    • ►  January (14)
  • ►  2021 (323)
    • ►  December (23)
    • ►  November (34)
    • ►  October (26)
    • ►  September (13)
    • ►  August (19)
    • ►  July (21)
    • ►  June (29)
    • ►  May (25)
    • ►  April (23)
    • ►  March (43)
    • ►  February (29)
    • ►  January (38)
  • ►  2020 (290)
    • ►  December (33)
    • ►  November (37)
    • ►  October (28)
    • ►  September (35)
    • ►  August (31)
    • ►  July (26)
    • ►  June (17)
    • ►  May (21)
    • ►  April (18)
    • ►  March (15)
    • ►  February (17)
    • ►  January (12)
  • ►  2019 (160)
    • ►  December (8)
    • ►  November (7)
    • ►  October (12)
    • ►  September (9)
    • ►  August (27)
    • ►  July (18)
    • ►  June (18)
    • ►  May (11)
    • ►  April (11)
    • ►  March (9)
    • ►  February (16)
    • ►  January (14)
  • ►  2018 (162)
    • ►  December (12)
    • ►  November (6)
    • ►  October (13)
    • ►  September (10)
    • ►  August (20)
    • ►  July (9)
    • ►  June (14)
    • ►  May (9)
    • ►  April (16)
    • ►  March (21)
    • ►  February (17)
    • ►  January (15)
  • ►  2017 (306)
    • ►  December (20)
    • ►  November (23)
    • ►  October (20)
    • ►  September (26)
    • ►  August (31)
    • ►  July (31)
    • ►  June (34)
    • ►  May (26)
    • ►  April (24)
    • ►  March (20)
    • ►  February (28)
    • ►  January (23)
  • ▼  2016 (269)
    • ►  December (22)
    • ►  November (21)
    • ►  October (22)
    • ►  September (15)
    • ►  August (12)
    • ►  July (27)
    • ►  June (24)
    • ▼  May (23)
      • Ile nadanganya veve kuwa Swahili iko na sida nenda...
      • Boozers Want Special Seats Rescinded
      • Mlevi kusafirisha bangi na mirungi kwa ndege
      • Racism: India can't get away with murder anymore
      • Kijiwe chamuaga Kitwanga
      • Nyimbo zangu nilipokuwa Kenya
      • Mugful: Boozers need their houses back
      • Sukari: Mnamuonea Magufuli
      • Wake za mawaziri waitwe "mawazira"
      • Kijiwe: Walioficha njuluku ughaibuni wanyongwe
      • Crucify those who offered 8tn tax exemption
      • Viapo vya akina Makonda vina uhalali kisheria?
      • Makufuli chunga wasikuKolimbe au kukuSoikone
      • Hii Kali sijui macho yangu!!!!!!!!
      • Kijiwe chataka waliosamehe kodi wanyongwe
      • Kumbe bado tunao akina Magufuli wengi tu!
      • MY NEW BOOK IS OUT!!!!!
      • When suited beggars expel ragged ones
      • Viongozi wa kiroho nao wataje mali zao
      • Mlevi kuhamia mlima Kilimanjaro
      • Kijiwe chamchimba Makufuli
      • Magufuli ondoa madili rejesha maadili
      • Mugful, don’t reward failures and hangers-on
    • ►  April (29)
    • ►  March (26)
    • ►  February (27)
    • ►  January (21)
  • ►  2015 (399)
    • ►  December (34)
    • ►  November (24)
    • ►  October (22)
    • ►  September (34)
    • ►  August (29)
    • ►  July (37)
    • ►  June (22)
    • ►  May (32)
    • ►  April (35)
    • ►  March (46)
    • ►  February (47)
    • ►  January (37)
  • ►  2014 (502)
    • ►  December (47)
    • ►  November (49)
    • ►  October (47)
    • ►  September (37)
    • ►  August (40)
    • ►  July (42)
    • ►  June (30)
    • ►  May (35)
    • ►  April (47)
    • ►  March (44)
    • ►  February (39)
    • ►  January (45)
  • ►  2013 (399)
    • ►  December (37)
    • ►  November (27)
    • ►  October (31)
    • ►  September (26)
    • ►  August (33)
    • ►  July (39)
    • ►  June (28)
    • ►  May (40)
    • ►  April (44)
    • ►  March (39)
    • ►  February (26)
    • ►  January (29)
  • ►  2012 (597)
    • ►  December (27)
    • ►  November (26)
    • ►  October (27)
    • ►  September (30)
    • ►  August (47)
    • ►  July (94)
    • ►  June (86)
    • ►  May (119)
    • ►  April (83)
    • ►  March (23)
    • ►  February (17)
    • ►  January (18)
  • ►  2011 (261)
    • ►  December (20)
    • ►  November (19)
    • ►  October (20)
    • ►  September (21)
    • ►  August (27)
    • ►  July (12)
    • ►  June (15)
    • ►  May (20)
    • ►  April (27)
    • ►  March (32)
    • ►  February (24)
    • ►  January (24)
  • ►  2010 (205)
    • ►  December (25)
    • ►  November (23)
    • ►  October (23)
    • ►  September (23)
    • ►  August (17)
    • ►  July (13)
    • ►  June (12)
    • ►  May (10)
    • ►  April (18)
    • ►  March (9)
    • ►  February (16)
    • ►  January (16)
  • ►  2009 (163)
    • ►  December (19)
    • ►  November (14)
    • ►  October (11)
    • ►  September (6)
    • ►  August (12)
    • ►  July (9)
    • ►  June (11)
    • ►  May (20)
    • ►  April (22)
    • ►  March (14)
    • ►  February (12)
    • ►  January (13)
  • ►  2008 (191)
    • ►  December (12)
    • ►  November (11)
    • ►  October (14)
    • ►  September (15)
    • ►  August (16)
    • ►  July (23)
    • ►  June (10)
    • ►  May (19)
    • ►  April (16)
    • ►  March (19)
    • ►  February (17)
    • ►  January (19)
  • ►  2007 (33)
    • ►  December (13)
    • ►  November (20)

About Me

My photo
View my complete profile

Travel theme. Powered by Blogger.