The Chant of Savant

Tuesday 7 February 2012

Wabunge wa CCM wanamdanganya nani?

KATIKA kikao cha Bunge kinachoendelea mjini Dodama wabunge wa Chama Cha Mapinduzi wamekuja na mpya-eti kuikosoa na “kuikomalia” serikali yao! Kioja hiki cha aina yake kilianza pale mbunge wa kwanza kuonyesha ‘usanii’ alikuwa Charles Tizeba aliyesema, “Kwanza waziri (Mkulo), angetuambia kwa nini alikaidi ushauri wa kamati na hasara ambayo taifa limepata, wenzangu wamesema ni usikivu, lakini mimi sioni zaidi ya ukaidi, huu si mwenendo mzuri. Ushauri wa wabunge unakuwa na nia nzuri,”

Je, Tizeba anaishi wapi huyu asiyejua tabia ya chama chake cha kupongeza kila upuuzi? Tukija kwa Mkulo na ‘sanaa’ zake za eti kupunguza ushuru wa maji ya kunywa ya chupa kwa kuwaonea huruma watu wa kawaida, ni vituko mtindo mmoja.

Tangu lini makapuku wakanywa maji safi ya chupa iwapo wengi hasa wale wa Dar es salaam wanakunywa maji ya mitoni wayanunuayo toka kwa wauza maji wanaoweza kuchota maji popote bila kujali afya ya mnunuzi? Kama Mkulo hajui basi aambiwe kuwa makapuku wengi hunywa maji ya visima au ya Sumaye na Makamba ambao waliwahamasisha kuchimba visima ambavyo kimsingi si visima kitu bali maji ya chooni yanayonywewa kwa kusingizia kuwa yanatoka visimani wakati huko chini ya ardhi mtandao ni mmoja.

Niliwahi kulalamikia suala hili kwenye mwaka 2001 kiasi cha kukosana na Yusuf Makamba wakati ule akiwa Mkuu wa Mkoa na Frederick Sumaye akiwa Waziri Mkuu. Je, Mkulo amewahurumia watu wa chini au amepewa chochote na wauza maji? Je, maji ya chupa ameona bora kuliko kulanguliwa umeme huku wizara ya Mkulo ikiongoza kutoa misamaha ya kodi kwa wafanyabiashara wakubwa wakubwa?

Aliyefuata kwa vituko ni William Mgimwa (Kalenga) aliyesema, “Kama TRA inakusanya asilimia 102 na kuna upungufu wa fedha, basi kuna tatizo na tunahitaji maelezo maana tuna takwimu za makusanyo, lakini hakuna maelezo ya matumizi,” Je, mkipewa maelezo au kutopewa maelezo mtafanya nini iwapo mnapojifanya kupinga huitwa na kukalishwa chini kama kamati ya chama na kuminywa mbavu kiasi cha kukaidi viapo vyenu?

Je, mmesahau kuwa wananchi wanajua usanii wetu na ushirika wenu na serikali yenu? Kuko wapi kutelekeza dhana ya kujivua gamba ambao kimsingi ndiyo chanzo cha maafa yote ya Watanzania?

Hebu turejee kwa Tizeba tena. Alikaririwa akisema, “Punguzo hilo halitamsaidia mlaji wa kawaida zaidi ya wenye viwanda kama waziri alivyokiri ameandikiwa na wenye viwanda… kwa hiyo itanufaisha wenyewe.”

Je, kama mbunge na wabunge wengine wanajua ukweli kuwa alichotaka kufanya Mkulo ni kufanikisha ‘deal’ lake, wanamchukulia hatua gani kwa mamlaka waliyo nayo? Maana yake ni kwamba Mkulo analidanganya Bunge jambo ambalo ni kosa linalopaswa kumwajibisha. Lakini nani atamwajibisha nani iwapo na wabunge nao wanawadanganya waliowachagua na kuishia kulala kitanda kimoja na serikali pamoja na mazabe yake yote?

Wabunge wetu hasa wa CCM ambao mara nyingi hutumika kutia mhuri kila upuuzi wa serikali wangekuwa wanamaanisha wanachosema, wezi wa Richmond wangekuwa gerezani ukiachia mbali kufuta mikataba ya kijambazi kama ile ya IPTL, Aggreko, Dowans na mingine mingi.

Wangeweza kuja na hoja na miswaada ya kufumua uwekezaji upya na kuusuka upya kwa masilahi ya taifa. Lakini nani anajali iwapo wanapewa ujumbe kwenye kamati na bodi mbali mbali na kupata ulaji wao? Nani anajali iwapo wote wanatenda dhambi ile ile na wana sharubu kama samaki wengine hasa mapapa?

Wabunge wetu hasa wa CCM wangekuwa wakweli na wawakilishi wa kweli wa wananchi wasingesumbuka kutaka maelezo ya kuridhisha wakati serikali inayojidai kukusanya kodi kwa asilimia 102 ikidai haina pesa ya kulipa malimbikizo ya mishahara na stahiki za walimu.

Wasingeelewa kitu wala kudai maelezo bali uwajibikaji kwa serikali yenye kukusanya kodi kwa 102% lakini ikashindwa kuongeza mishahara ya watumishi wake hadi madaktari kugoma nchi nzima.

Ni ajabu kwa serikali hii inayoweza kukusanya kodi kwa asilimia zaidi ya mia kupata pesa ya kugharimia safari za watawala nje zisizo na umuhimu lakini ikashindwa hata kupeleka huduma kwa wananchi!

Maana kwa wanaojua maana ya kulipa kodi, watakubaliana nasi kuwa wananchi hulipa kodi kwa serikali ili iweze kuwaletea huduma wasizoweza kuzitoa mmoja mmoja. kazi ya kodi siyo kuwalisha watawala na kuongezeana hata posho za makalio bali kurejesha hiyo kodi kwa wananchi waliochanga ili kujiletea maendeleo.

Ni bahati mbaya kuwa kwa Tanzania kodi inahimizwa kulipwa ili kugharimia maisha aghali ya watawala na wapambe wao na familia zao. Ni kodi ya kujihudumia na si kodi ya maendeleo kama inavyoitwa. Wananchi wangejua haki zao vilivyo, wangegoma kuilipa kodi serikali isiyo tekeleza ahadi na wajibu wake. Yako wapi maisha bora kwa watanzania yaliyoahidiwa na CCM kwenye uchaguzi?

Wabunge wa CCM wangejishughulisha na hili wangeleta maana zaidi ya kutafuta sifa. Mwenye kubisha na kunikosoa na kuonyesha udhaifu wa hoja zangu kama anaona upo. Ni mara ngapi wabunge wa CCM wanaikamia serikali na kuwekwa sawa kwenye kamati ya chama na kunywea?

Je, wabunge wa CCM wanamdanganya nani na nani anaweza kuwa ‘chizi’ awaamini? Tunawashauri waendelee na biashara yao ya kupongezana badala ya kuuhadaa umma kuwa wanaujali.


Chanzo: Tanzania Daima Februari 8, 2012.

8 comments:

Anonymous said...

WABUNGE WA CCM WOTE NI MAFISADI HIVYO HAWANA MUDA WA KUJALI MASILAHI YA WALALA HOI

Anonymous said...

My beta test project:
http://blog.erolove.in/?new-si.html
http://blog.erolove.in/land?browse-ik.html

Anonymous said...

[url=http://hermes-paket-versand.hermeshuts.com]hermes paket versand[/url]

Anonymous said...

[url=http://hermes-summary.hermeshuts.com]hermes summary[/url]

Anonymous said...

how's life ? mpayukaji.blogspot.com blogger discovered your website via search engine but it was hard to find and I see you could have more visitors because there are not so many comments yet. I have discovered website which offer to dramatically increase traffic to your website http://xrumerservice.org they claim they managed to get close to 1000 visitors/day using their services you could also get lot more targeted traffic from search engines as you have now. I used their services and got significantly more visitors to my site. Hope this helps :) They offer most cost effective backlinks Take care. Jason

Anonymous said...

Thank you so much for doing this web site. [url=http://a-lebovski.narod2.ru/powerpoint-2010.html ]Office 2010[/url] and [url=http://a-lebovski.narod2.ru/powerpoint-2003.html ]Powerpoint2003[/url]

Anonymous said...

This is Babulerman.

Annawxbu said...

WABUNGE WA CCM WOTE NI MAFISADI HIVYO HAWANA MUDA WA KUJALI MASILAHI YA WALALA HOI