Friday, 22 November 2013

Blogs zinapomkera Kikwete hadi akapayuka


"Tunatumaini na matarajio yetu sisi tuliobakia nyumbani ni kwamba mtaisemea vizuri nchi yetu, mtaitetea nchi yen na mtaihangaikia nchi na kuleata faida numbani. Ni jambo haliingii akilini kuwa baadhi yenu manweza kuishi hapa na kazi yenu ni kushinga kwenye mablogu mkilaumu nchi yenu wenyewe. Nchi mbaya, viongozi hawafai...mnapata faida gani?"Jakaya Kikwete akiwa nchini Poland alipowaponda wanaomponda.

Hiyo hapo ni nukuu ya rais Jakaye Kikwete ambaye anaonekana kukwera na baadhi ya blog kwa kuishambulia serikali yake bila kujua kuwa huo ndiyo ukweli. Ingawa si lengo la blog hii kuchambua malalamiko ya Kikwete, amesema uongo kudai kuwa watu wanashinda kwenye blog. Watu tuna kazi zetu na hatuandiki kwa vile hatuna kazi za kufanya. Tunaishi maisha ya kuheshimika na elimu ya kutosha. Hivyo kama Kikwete anadhani wengi wa wanaoandika ni watu wa vijiweni kama wale aliowatengeneza huko si wote. Wengine kuandika na kufundisha ndicho kibarua chetu.
Maswali mepesi, kwani viongozi si wabaya na nchi haina hali mbaya iwapo wachache wanawaibia wengi kipuuzi? Je Tanzania si balaa tokana na uongozi mbovu wa Kikwete uliojaa uzembe dhidi  ya ufisadi ujambazi na uuzaji mihadarati?

5 comments:

Jaribu said...

Kumbe blogs zinamkera? Anafikiri kila mtu ananunulika kama Mjengwa au Michuzi?

NN Mhango said...

Jaribu,
Kukereka kwa Kikwete ni furaha kwetu sisi tunaoonekana kutokuwa na kazi huku ughaibuni bali kumkera. Nadhani huu ni ushahidi kuwa sisi tusio vyangudoa kimaadili au wachumiatumbo tunatimiza wajibu wetu kwa taifa letu. Kikwete alikosea kusema eti wote tuliopo ughaibuni tunamsema vibaya wakati anazo blog nyingi nyumba ndogo zake ughaibuni sawa na zile zinazoimba sifa zake hata anapopaswa kulaaniwa.

Jaribu said...

Umenena kweli. Na shida yake ni kwamba anashidwa kutofautisha kati ya taifa na yeye. Unamposema yeye si kwamba unaisema nchi, unless ni mmoja wa wale wanaodai kuwa "Tanzania ni nchi yao."

Unanimkumbusha juha mmoja kwenye hizo blog nyingine aliyekuwa anasambaza hoja hiyo ya kuwa wanaomsema Kikwete hawana kazi ya kufanya bali ni kushinda kwenye mablogs. Hawajui kuwa kila mtu ana uwezo wa kuamua kuwa atatumia vipi muda wake. Unless sisi tunaomponda tunaifanyia kazi serikali ya Tanzania, haimhusu kama tuna kazi au la. Lakini mimi kwa ujumla huwa sitegemei kauli yote ya msingi kutoka kwenye kinywa chake.

Anonymous said...

Yeye amejuaje kuwa huko kwenye "ma-blog" watu wanamkandia/kandia Bongo badala ya kumfagilia/fagilia nchi? Kumbe naye anashinda humo badala ya kufanya kazi aliyopewa kuifanya. ]

Kabla ya uchaguzi uliopita, kulikuwa na blog mbili zilizokuwa zinaimba sifa za huyu bwana, hata kufika pahala mmiliki wa blog moja kuanza kujiita "Mkuu wa wilaya", sijui aliahidiwa au la. Kuna mwingine alikuwa haishi kuipamba B'moyo etc. kila uchao. Kweli njaa mbaya, hususan ikiingia "upstairs" kama asemavyo mwl. Mhango.

Ooooops, ngoja niachane na blogs nifanye kazi sasa. Hehehehehe...

Anonymous said...

Na bado huu ni mwanzo tu, hivi anafikiri kila ,mmoja ni mfuasi wa uzandiki wa ccm na serikali yake mufilisi? Amenoa!