Wednesday, 27 November 2013

Je huu ni mwanzo wa mwisho wa Zitto Kabwe?Kwa wanaojua kilichompata akina Augustine Lyatonga Mrema, kuna uwezekano kuwa kinachoendelea ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni mwanzo wa mwisho wa mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe aliyekuwa Naibu Katibu mkuu wa CHADEMA.
Kama Mrema, Zitto alilelewa na CHADEMA sawa na Mrema na Chama Cha Mapinduzi (CCM).  Kama Mrema, Zitto ameponzwa na tamaa kutaka madaraka, sifa na kuonekana ni bora kuliko wengine. Kama Mrema, Zitto ameonyesha papara na uchu mkubwa wa ukubwa. Kama Mrema, Zitto ataondoka CHADEMA na CHADEMA haitakufa sawa na Mrema na CCM.
Tofauti ya Mrema na Zitto ni kwamba Mrema aliondoshwa CCM si kwa kutumiwa na chama kingine zaidi ya mipango yake ya kuusaka ukubwa. Hapa unaweza kuwaunganisha watu kama Seif Sharrif Hamad ambaye kuondoka kwake CCM hakukuiyumbisha sawa na alivyoondoka Mrema sawa na itakavyokuwa kwa Zitto na CHADEMA.
Tofauti na Mrema, Zitto ameondolewa mapema mno. Hakufaidi ulaji ndani ya serikali kama ilivyokuwa kwa Mrema aliyejijengea sifa ya utendaji hata kama ulikuwa wa kiimla na kihuni.
Zitto anaingia kwenye vitabu vya historia kama kijana aliyeanzia kwenye mavumbi ingawa anawez akurudi kwenye mavumbi kama hatarejea CCM ambao wanadai kumtumia. Ushahidi ni ile hali ya mkutano wake na waandishi wa habari kuandaliwa na kusimamiwa na UVCCM jambo ambalo Zitto na wenzake hawajakanusha. Huenda watafanya hivyo ingawa it is a bit too late too little.
Hakuna nyundo itakayommaliza Zitto kama kukiri kwa “mtu wake”, Dk. Kitila Mkumbo kuwa kweli waliandaa waraka uliowatia kitanzini pamoja na juhudi za bila mafanikio za kumtenga Zitto na waraka huu.
Maswali makuu,: Kama kweli Zitto hakuhusika na waraka husika wa uhaini na usaliti chamani, kwanini hakuukana alipokutana na waandishi wa habari? Kwanini Zitto alikuwa too apologetic and diversive kwenye press conference yake? Kwanini Zitto aliruhusu waasi waliokwisha aangukiwa na panga la CHADEMA kuupamba mkutano wake kama hakuna namna?
Je mwanzo wa mwisho wa Zitto ndiyo unaanza? Je ni mapema kuanza kuandika tanzia yake kisiasa au kutegemea kumuona akifufukia CCM?Je kweli Zitto hakutumiwa na CCM iwe kwa bahati mbaya au makusudi? Rejea uhusiano wake na marehemu Amina Chifupa.

No comments: