Saturday, 9 November 2013

Maisha bora kwa Wadanganyika wote!

Ni Maisha Bora kwa Wote au rais Bwana na raia Mtwana? Hapa chini rais Jakaya Kikwete akiwa anamsikiliza mlalahoi aliyepigika huku mkubwa akiendelea kutanua ndani na nje ya nchi. Bwana mkubwa huwa hakai ofisini kusikiliza na kutatua shida za walioingia mkenge wakampa kura ya kula. Atatumikia lini baada ya kuwatumikisha kwa miaka yote? Who knows? Huenda akishaondoka ofisini atatumia NGO ya mke wake kama siyo kuunda yake kama mtangulizi wake kuwatumia sorry kuwatumikia watanzania. Kazi kwelikweli.

Picha kwa hisani ya Ofisi ya Rais.

No comments: