Friday, 29 November 2013

Zuma aonyesha tamaa na kufuru zake

 Jacob Zuma's Nkandla residence
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini huwa hakaukiwi vituko. Ukiachia kashfa yake ya kujipatia mamilioni ya dola kwa kumtumia mhindi rafiki yake na kashfa ya ubakaji, Zuma anakabiliwa na kashfa nyingine ya kutumia pesa ya umma kujenga makazi ya kifahari kijini kwake Nkandla, (kama yanavyooneka hapo juu). Hata hivyo, mahakama ilimsafisha kwenye kilichoonekana kama mizengwe. Japo si wote, watawala wetu ni wezi, waroho, wenye roho mbaya na majizi ya mali ya umma. Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.

4 comments:

Anonymous said...

Tatizo ni wapiga wa kiafrika hawatambui umuhimu kura zao katika kuadhibu viongozi wababaishaji na wezi ndiyo sababu wapo tayari hata kujitokeza kugombea nyazifa mbalimbali za kisiasa na kushinda Tanzania...

Wapiga kura wa Tanzania watafanya vivyo hivyo mwaka 2015 wakati bei ya umeme inapanda kila siku kwa sababu zipo wazi lakini leo watu hao hao waliofanya hayo madudu wizi wa mchana kweupe ndiyo wanaonekana malaika.

Katika mazingira haya tusitegemee miujiza kama watu wengi wanavyoamini hapa nyumbani kwamab tumwachie mungu. Wanasahau Mungu amesema jibidishe nitabariki siyo kumpigia kura mwizi halafu utegemee Mungu ambadili awe Mzalendo... Kamwe haitatokea na maisha yataendlea kuwa magumu na yalijaa ubabaishaji

NN Mhango said...

Anon,
Mie siamini katika miujiza. Magharibi hawakuendeleza nchi zao kwa kutegemea miujiza bali ubunifu na uwajibishaji. Ningekuwa naweza kueleweka ningewashauri watu wetu waingie mitaani kuhakikisha kila mwizi anatimliwa na kuwa na katiba inayozuia ujambazi kama unavyoendelea.

Anonymous said...

NN Mhango,

Tupo pamoja, nilichosema hapo awali ni kwamba imani iliyojengeka kwenye akili za watanzania walio wengi ni kwamba Miujiza(Mungu) ndiyo jibu ya matatizo yao.

Na hii ndiyo sababu hata hao wezi wanatumia majukwaa ya kidini na imani kujihalalisha kwamba wao ni malaika na kujibalaguza kuwa hawahusiku kilichopo.

Hivyo kwa kutambua akili za wapiga kura wao wanatumia dini sehemu ya kujificha rangi zao baada ya uchaguzi kupita wanazionesha tena rangi zao. Uchaguzi ukikaribia tena wanajithaminisha tena kupitia dini.

Ukingalia kwa undani utanielewa kuwa watanzania wanategemea miujiza kwa kuchagua viongozi ovyo ovyo na wezi halafu wanategemea miujiza..

NN Mhango said...

Anon,
Nakubaliana nawe hasa nikiona jinsi matapeli wa kinigeria wanavyovuna utajiri toka kwa watu wetu maskini na wajinga. Pia tunao matapeli wa ndani kama vile Kakobe, Gamanywa, Lusekelo, Rwakatare, Mwakasege na wengine wengi wanaowaibia watu wetu sawa na wanavyofanya majambazi wa kisiasa.