Sunday, 24 January 2016

Biashara ya dini-Anonymous

Biashara ya dini imeaanza tangu zama za kale pale mwanadamu alipoaanza kujielewa kuwepo kwake hapa dunia na kuanza kujiuliza na kutafuta maana hiyo ya kuwepo hapa duniani.Tukiangalia kwa mapana zaidi maana ya dini kuanzia uchawi na makuhani wake,dini ya mababu na makuhani wake hatimae dini zinazojulikana za mbiguni au za ardhini na makuhani wake,tunakuta tu kwamba mfumo wote wa dini hizo za aina mbali mbali zimekuwa zenye kuanzisha biashara kubwa ya kidini tangu zama hizo hadi dunia itapokwisha.
Ukweli usiopingika ni kwamba dini ni biashara kubwa na mtaji wake ni uwongo unaopambwa na kuonekani ni kweli na wateja wake ni wale ambao hawana wakati wa kutafakari kuhusu biashara hiyo na kuwaachia makuhani wa dini hizo kutafakari kwa niaba yao na makuhani hao wamefanikiwa katika biashra hiyo baada ya kuwahakikishia na kuwakinaisha waumini wao kwamba wao kama makuhani wanauhusiano mkubwa sana na wakaribu sana na miungu yote ya dini hizo mbali mbali,na baada wateja hao kufikia imani hiyo wamejikuta wakiibiwa mchana kweupe ili hali wenyewe wakiridhika. kwa kutoa sadaka ambazo haziwafikii waungu wa dini hizo wala haziwahudumia wao kama ilivyokuwa inapaswa.
Jambo la kushangaza zaidi la makuhani wa dini zote hizo tangu zama hizo hadi hii leo ni kujisogeza kwao sana kwa watu wenye madaraka na nguvu za kiuchumi na kisiasa ujisogezaji ambao umewafanya wawe kitu kimoja katika kuwakandamiza wananchi wao kwa kutumia biashara hiyo ya dini.Wenzetu wa bara la ulaya katika karene ya 15 waliishitukia na hatimae waliikataa biashara hiyo baada ya kuwagunduwa makuhani hao ni mizigo isiobebeka tena katika jamii na kuiondoa biashara hiyo kabisa na waliokuwepo madarakani hawakuwasogeza tena makuhani hao karibu yao zaidi ya huduma zao ambazo zinachukuliwa ni kama huduma za kijamii tu ndani ya makanisa yao,hii ukiondoa nchi kama Marekani ambapo biashara hiyo ya kidini imkuwa ni kubwa mno lakini tofauti yao na sisi waafrika kwamba wanaoibiwa huko Marekani ni waumini wa kawaida ambao wametawaliwa na kuzongwa na maisha ya Mada(materialism) na hatimae hawana pa kukimbilia isipokuwa mikononi mwa makuhani hawa wa kidini.
Mwalimu Mhango,tatizo la kwetu Afrika au kwa nchi za ulimwengu wa tatu ni kwamba makuhani takriba wote wanajipendekeza kwa watawala kwa imani tu kwamba wakiwa karibu na watawala hao biashara yao itazidi kuwaletea faida ya kiuchumi,kuzidi kukubalika kwa jamii kubwa na kuzidisha haiba yao ya kidini na kijamii,Ilikuwa juu ya viongozi wetu wawaone tu kama ni wafanya biashara tu wa dini ambao wanataka kujitajirisha kupitia migongo yao,lakini kwa bahati mbaya viongozi wetu wengi wanajikuta wamekamatwa na makucha ya wafanya biashra hao kwa vile malezi yao ya awali ya kijamii hayatofautiani sana na wale waumini wa kawaida na hatimae wamejikuta na wao ni wateja wazuri tu kwa makuhani hao.
Mwalimu Mhango,ebu na tuuone ukweli huu kwamba dini ni uhusiano wa yule anaeamni,anachokiamini na anachokiabudu tunakuta tu kwamba ni uhusiano binafsi(private) ambao muumini huyo inabidi awe mwenye kujiamini na kuwa huru kuabudu anachokiabudu na kuomba anachokiabudu bila ya kuingiliwa na mtu mwingine katikati na kumuombea kwa niaba yake kwa hicho anachokiabudu kwa njia yyote ile anayoiona ni muwafaka,lakini inapotokea kuwapa makuhani haki ya kuwaombea wengine kwa niaba au kufikia mpaka ujasiri wa kuiombea Kaya au kumuombea mtawala awe Rais au Mfalme hapo sasa ndio utapeli wa wazi na wa hali ya juu ambao biashra hiyo ya dini inakuwa na mafanikio makubwa.
anaaamini kama wanavyoamini wanadamu wengine iweje leo tuwape makuhani hao haki ya kutuombea au kuombea Kaya?Je ni wapi walipopewa uhakika kwamba maombi yao yanakuwa na nguvu au uhakika au dhamana ya kujibiwa huko wanapo omba?Je kwa nini tuwape nguvu hiyo ya maombi makuhani hao kama si sisi wenyewe kuamini kwamba kumekuwa na makubaliano kati yao na hao miungu yao kwamba wakiomba hawatokataliwa maombi yao au na wao ni sehemu ya miungu hiyo ambayo inaishi na sisi duniani katika maumbile ya kibinadamu?
Naam,Mwalimu Mhango,umefafanunua vya kutosha na umehadharisha vya kutosha na msemo wako wa "uvivu wa kufikiri"ndio unaosababisha biashara hii ya kidini kuendelea kuwa kubwa na kuna mzsemo mwingine wa mababu zetu waliosema kwamba "wajinga ndio waliwao"na tuwaondolee wafanya biashra hii ya dini uvivu wa kufikiri inawezekana ikapatikana nafuu kubwa sana kama walivyo waobdelea watu wa bara la Ulaya wafanya biashara hawa.Je tutaweza kufanikiwa hilo katika jamii yetu ambayo mihimili yote ya Primitive Society bado inatutawala hata kama tunaishi katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia na wengine wetu tunamiliki shahada za juu za kielimu?
Chanzo: Anonymous

No comments: