Wednesday, 6 January 2016

Waziri mkuu anapogeuka mwanamuzikiWa pili kushoto ni waziri mkuu wa zamani wa Kanada, Stephen Harper akiwa na wanamuziki wa kundi lake la  Herringbone baada ya kutumbuiza jijini Toronto hivi karibuni
Baada ya kubwagwa kwenye uchaguzi mkuu uliopita nchini Kanada, waziri mkuu wa zamani Stephen Harper ameamua kuwa mwanamuziki. Napiga picha kuwaona akina Edward Lowassa na Fredrick Sumaye hata Mizengo Pinda wakitumbuiza maeneo ya Manzese jijini Dar. Wenzetu ni wabunifu na wawazi. Hawafichi mapenzi yao hata wakiwa na madaraka makubwa kiasi gani. Wakati Harper akiingia kwenye muziki, Barack Obama anapanga kucheza mpira wa tufe au tenis hata ku-surf kwao Hawaii. Sijui Jakaya Kikwete zaidi ya kuizunguka dunia anapanga kujiburudisha kwa mchezo au tasnia gani. Nadhani Kikwete anafaa kujiunga na vikundi vya maigizo au filamu ili aonyeshe umahiri wake katika usanii, fani aliyoienzi na kuimudu zaidi.

No comments: