How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Tuesday, 19 October 2010
Fikra Mbadala-Ningekuwa Kikwete nisinge.........
Fikra mbadala
Wapendwa wageni wangu, nawataarifuni kuwa kila nipatapo fursa na wahayi, nitakuwa nikiwaletea wazo mbadala kwenye uga huu.
Leo najiuliza na kutoa baadhi ya dukuduku na majibu tuelekeapo Oktoba 31.
Ningekuwa Jakaya Mrisho Khalfan Kikwete nisingefanya yafuatayo;
Nisingegombea urais kwa awamu nyingine. Badala yake ningewaomba msamaha watanzania kwa kuwaangusha vibaya sana.
Nisingekubali mke wangu na mtoto wangu kuwa wasemaji wangu kwenye kampeni huku nikiwapiga teke marais na mawaziri wakuu wastaafu ambao nao wamegoma kunisaidia hasa saa hii ya kujaribiwa. Na wala nisingewaruhusu kuitumia ikulu na mamlaka yangu kusaka ngawira kama wale walionitangulia. Ningepiga marufuku NGO za wake wa wakubwa.
Nisingeruhusu upuuzi kama kutumia uhuni kama vile kutuma ujumbe mfupi kwenye simu wenye, waandishi wa habari nyemelezi na vyangudoa kuwachafua wenzangu au uzushi wa kumwaga damu wakati wamwagaji wa kweli wa damu ni chama changu.
Pia nisingejiruhusu kutegemea mafisadi kurejea ikulu. Badala yake ningewategemea watanzania ambao ningewambia fika; sina udhu wala sera kugombea tena. Ili niwafanyie nini zaidi ya kuwaingiza mkenge. Pia nisingetoa ahadi nyingine wakati za awali zilinishinda.
Kadhalika, nisingeruhusu wachumia tumbo na wapiga ramli kunizuga nikijua fika nikiporomoka watanikimbia kwa vile msosi utakuwa nao umetimka.
Nisingejidanganya na kuwadanganya watanzania kuwa nafaa wakati najua fika sifa hata kuwa mjumbe wa nyumba kumi.
Ningekuwa Kikwete, ningeanza kujiandaa kustaafu na kuachia haki katika uchaguzi itawale kama alivyofanya mzee Kenneth David Kaunda wa Zambia ili umma unisamehe na kuniheshimu.
Kabla ya kutokomea ningehakikisha natoa maelezo kuhusiana na kuhusishwa kwangu kwenye list of shame ya Dk. Wilbroad Slaa.
Ningewachisha kazi Yusuf Makamba,Lawrence Masha, Salva Rweyemamu, Abdulrahman Kinana, Tambwe Hiza na wachumia tumbo wengine ambao wamegeuka kongwa.
Zaidi zaidi, ningeenda kujipumzikia na kujiuguza badala ya kujipa moyo ilhali nikijua najidanganya.
Ningefanya mambo mengi kubwa likiwa ni kuanza kutubia na kuomba msamaha kwa sana.
Kila la heri. Nategemea ushauri na mawazo mbadala. Naomba ushauri wenu ili lau nijinusuru na taifa letu. Enough is enough. Wale wanaonitegemea kula watafuta pa kula au wakale Ukonga. Time will come when this will be cinch reality. Je wewe ungekuwa Kikwete ungefanya nini?
Nkwazi
By STAFF REPORTER THE SUN October 19, 2910.
Soma habari za mjukuu shoga wa mfalme wa Saudia ambaye alimuua mwenzake huko Uingereza na kukutwa na hatia.
A GAY Saudi prince is facing life in jail today for brutally battering and strangling his servant to death.
Saud Abdulaziz bin Nasser al Saud carried out a campaign of "sadistic" abuse against his manservant.
He was today found guilty at the Old Bailey of murdering Bandar Abdulaziz in a "brutal" assault in their five-star hotel suite.
The prince was fuelled by champagne and "sex on the beach" cocktails when he bit the 32-year-old hard on both cheeks during the attack in February.
They had just returned from a Valentine's Day night out when al Saud launched the ferocious assault.
When he was arrested he at first wrongly believed he had diplomatic immunity, but his special status as a Saudi royal could not save him from British justice.
The 34-year-old, a member of one of the world's richest and most powerful dynasties, was found guilty of murder today by the jury after just one hour and 35 minutes of deliberation.
Al Saud showed no reaction as the decision was announced.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Tunatawaliwa badala ya kuongozwa. Udikteta ndiyo usiseme. Wazee wastaafu wanapigwa mabomo ya machozi kwa kudai haki yao ya msingi. Magazeti yanaandika habari ya kueleweka yanatishiwa kufungiwa. Sijui tunaelekea wapi?
Post a Comment