Friday, 8 October 2010

Kama Sheik Yahya anaumwa ajue mojaNimepata habari kuwa shehe Yahya Hussein yule tapeli anayejiita mtabiri maarufu Afrika Mashariki na Kati amelazwa. Ana mazoea ya kuwatabiria wenzake mabaya hasa wapinzani ili apate fadhila toka kwa Jakaya Kikwete mgombea wa Chama Cha Mapinduzi ambaye kwake ni Mungu.

Kwa vile mzee huyu mtu mzima hovyo amemsahau Mungu wa kweli na pekee na kumtukuza na kumwabudia binadamu tena mchafu, wakati umefika wa kumwambia kuwa zake zinazidi kwisha. Katika safu yangu ya Jicho la Kijiweni nilitabiri kuwa badala ya kufa wapinzani atakufa yeye. Kama anavyowaombea mabaya wapinzani, mie namwachia Mungu aamue. Naomba kila siku kile anachowambea wengine kimrjee ili awe somo kwa wachumia tumbo wengine wanaoabudia upuuzi kama vile wenye madaraka na vitu. Hata akina Kagoda na wenzake wanajidanganya. Wanatesa watu wengi wa Mungu na Mungu hafurahishwi na hili. Hata huyo baba yao fisadi mkuu ni suala la wakati akaenda njia ya Oumaru Yar'Adua kutoka na kujifanya mjanja wakati siyo kwa kuficha maradhi yake.

Wacha Mungu tuombe sana Mungu atutetee dhidi ya mafisadi hawa wanaojiona miungu.
Je kati ya utabiri wa Yahya na wangu ni upi utakuwa wa kweli? Ni suala la muda. Na hii ni namna ya Mungu kuongea na wachumia tumbo na wasaliti kama Augustine Mrema na waandishi wa habari wanaotumiwa kama nepi kuwachafua wapinzani. Inshallah Mungu yupo na analipa hapo hapo.Kesho nitatangaza vifo vya wenye picha hizo hapo juu na lini mazishi yao yatafanyika hasa yule wa kwanza hapo 31 Oktoba 2010 inshallah. Tusione aibu kuonyesha hisia zetu dhidi ya mafisadi hawa. Mbona wao wanatangaza vitisho na uovu wao bila woga wala kificho kuanzia kutumia majini hata majeshi? Lt Gen Shimbo na mbwabweka wenzako mpo?

1 comment:

Malkiory Matiya said...

Hapa umenena mkuu. Mtu mwenyewe afya yake migogoro halafu hana hata tone la aibu kuwatakia mabaya wenzake.