Thursday, 8 March 2012

Sisi ndiyo winter inaanza
Kwa tunaotokea Ikwete winter ya mwaka huu ilikuwa ni neema. Hatukuwa na theluji wala baridi ya kukata na shoka kama tulivyozoea. Wakati wenzetu wanangojea kufunga kipindi cha winter sisi ndiyo tumekianza. Je hii itaendelea au kuishia hapa. Who knows.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Yaani kuangalia hivyo tu mwili umesisimka ile mbaya..hapa ndo tulizani inakwisha kwisha kumbe...juzi ikaibuka tena theruji iyooooo kaaaazi kwelikweli maisha haya!!!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Siku zote huwa nasali nisiweze kuishi katika hali ya hewa kama hii. Na sala zangu zimekuwa zikijibiwa - Kutoka Tanzania mpaka Los Angeles na baadaye Florida.

Nilifikiri kuwa nitahama Florida lakini inavyoonekana nitabakia japo katika mji mwingine. Na nikitoka hapa nimeapa itakuwa ni kurudi Tanzania na si vinginevyo.

Poleni mnaoishi katika hali ya hewa kama hii....