How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Friday, 23 March 2012

Uwekezaji na Tanzania ya kesho





mtoto akiwa amelazwa juani asijue atalala wapi

Kamanda wa polisi wa Ilala Faustine Shilongile akifurahia kazi safi wanayofanya polisi kulinda usalama wa watu wasio salama.

Kijiko kimefanya kazi yake. Waathirika watajiju.





Hapo juu ni mtoto mchanga akiwa amelazwa nje baada ya nyumba yao, kwennye zilizokuwa nyumba za wafanyakazi wa Bandari eneo la Shule ya Uhuru Dar es salaam kubomolewa kupisha ujenzi wa kituo cha mabasi yaendayo kwa kasi. Kweli wawekezaji wameanza kwenda kasi. Ukiangalia kichanga hicho na nchi inavyouzwa na watu wake unajiuliza swali moja kuu: Ni nani aliwaroga watanzania kuwa kondoo kiasi hiki?


Leo wawekezaji wamefikia kujenga viwanja vya ndege kwenye machimbo na kutorosha madini yetu mchana kweupe. Wawekezaji wamefikia kutulangua karibu kila kitu kuanzia simu hata dawa nasi tu kimya. Wauza unga sasa wana serikali ndani ya serikali na hakuna anayewagusa! Majambazi ndiyo wafadhili wakuu wa CCM. Rejea kisa cha Massawe wa Friendscorner kubainika ni jambazi la kutupwa na hapo hapo ni mfadhili tegemewa wa CCM.


Leo akina Lowassa wanalipwa kodi zetu baada ya 'kustaafu' kwa kuingiza faida ya Richmond. IPTL inaendelea kutuumiza na kutupandishia gharama za umeme ilhali pesa tunayoilipa IPTL inatosha kununua mitambo mipya na ya kisasa na kushusha bei ya umeme. Uliza wako wapi wahindi wa RITES waliokuja na mikoba ya makaratasi na kuondoka na magunia ya dola. Yote hayo ni tone katika bahari. Onyo: juzi serikali ya Mali iliangushwa kutokana na kukithiri kwa uchafu kama huo hapo juu. Kazi kwenu wenye nchi.



4 comments:

Jaribu said...

Hawa ni washenzi. Je, huwa wanawalipa wenye nyumba fidia au ndiyo bomoa bomoa tu?

Malkiory Matiya said...

Uwekezaji ni msamiati mbadala wa uwizi wa rasilimali za nchi yetu, jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia migongo ya mafisadi na viongozi wetu vipofu. Viongozi waliolewa misifa ya madaraka.

Malkiory Matiya said...

Ndugu yangu, mpendwa wangu na raisi mtarajiwa. Ebu weka email yako hadharani kuanzia leo. ASAP

Malkiory Matiya said...

Mkuu, hili limekaaje? http://www.issamichuzi.blogspot.com/2012/03/tangazo-la-usitishwaji-wa-matangazo-ya.html