Sunday, 25 March 2012

Breaking News Wade chariiiiii!!!Abdulaye Wade rais aliyeangushwa kushoto na rais mteule Mecky Sall

Habari zilizotufikia ni kwamba rais babu  king'ang'anizi wa Senegal Abdulaye Wade ameshindwa vibaya na mpinzani wake Mecky Sall kwenye marudio ya uchaguzi uliofanyika leo. Wade alionywa asigombee kipindi cha tatu kinyume cha katiba lakini alikataa. Sasa amefurushwa kwa aibu na zomeazomea. 


Kwa mara nyingine chama tawala kimfurushwa madarakani kwa amani kupitia sanduku la kura.


Hata hivyo Wade ameonyesha ukomavu wa kisiasa kukubali kushindwa tofauti na vibabu kama Mwai Kibaki wa Kenya na Robert Mugabe wa Zimbabwe. Alluta Continua Afrika kunazidi kucha. 

No comments: