Saturday, 31 March 2012

Tanzania wizi wizi mtupu!


Tanzania chini ya utawala wa sasa imeanzisha mtindo wa kula kwa zamu. Kila anayepata nafasi au cheo serikalini lazima ajitafutie jinsi ya kuitumia ili kujitajirisha na familia yake. Baada ya Mwanaidi Majaar kuangukia nafasi ya ubalozi kutokana na uhusiano wake mzuri na Jakaya Kikwete, amekuwa mbioni kuhakikisha anafanya kile wanachofanya akina Salma Kikwete, Anna Mkapa, Regina Lowassa na wake wengine wa vigogo. Tofauti na wao, Mwanaidi ameanzisha NGO ya mwanae sawa na watajwa walivyoanzisha NGO kupitia migogoni mwa waume zao. Mwanzoni tuliambiwa ni Foundation kumbe kampuni ya biashara. Huyu Hassan Majaar ukiachia mbali kuwa mtoto wa balozi ni nani Tanzania?

Taarifa zilizopo ni kwamba NGO hii ya ulaji imeanzisha duka la vitu mbali mbali jijini na kuliita la hisani wakati hakuna hisani yoyote bali usanii. Je kwa mchezo huu watu wetu watanusurika?

2 comments:

Anonymous said...

Huyo Hassan Maajar ni mwanae wa kiume Mwanaidi Maajar aliyefariki kwenye ajali ya gari Swaziland.

However, you may have a point kuhusu "Trust Fund" inayodaiwa kuanzishwa kugeuzwa biashara.

Jaribu said...

Unajua kuna jamaa wa MSNBC alianzisha mchango wa kupeleka madawati Malawi na anapeleka kweli, nafikiri jamaa wakaona kuwa wao wanaweza wakapata ulaji.