Saturday, 31 March 2012

Blogu hii inajua kuwa April 1 ni siku ya wajinga. Ila hatutafanya ujinga kuleta kituko chochote kwa vile hakiwasaidii wasomaji. Badala yake tunawatahadharisha wasomaji kutoamini kila habari.

4 comments:

Jaribu said...

Afadhali maana huku kuiga kwingine kunakuwa too much. Naona minjemba mizima inalishana keki wenyewe wanaona ndio maendeleo.

Hivi Canada huwa wanasheherekea hiyo sikuku? Maana US ndiyo haina dili, nashangaa Waswahili wameitoa wapi..labda Ulaya.

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli...Nimekuwa najiuliza kweli kuna wajinga?

NN Mhango said...

Hapa Canada hakuna kitu kama hicho. By the way, tangu ukoloni wazungu wanaamini fools live in Africa. Umesikia wakanada walivyogundua mafuta Kenya huku ikibainika kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje wa zamani wa Kenya, Moses Wetangula alishauza kile kisima kwa dola milioni kumi kwa mkanada ambaye amekiuza kwa kampuni ya Tullow kwa dola milioni sitini? Hawa kimsingi ndiyo wajinga. Maana ukiangalia mablogu mengine huamini kama kweli watu wanatumia akili. Haya wapendwa Jaribu na Yasinta shukrani kupita ugani mwangu. Nimefurahi kuona msivyopwakia mambo kama wajinga wetu.

Jaribu said...

Ala! Mimi nilisikia BBC wakishabikia hayo mafuata nikajua itawanufaisha Wakenya sikujua ishauzwa zamani. Hata wakulima wa Texas wakigundua mafuta huwa hawauzi visima vyao kwa bei ya kutupa. Wanahakikisha na wao wanapata percentage as long as kuna production hapo.

Tunashukuru na wewe pia kutuhabarisha. Mambo mengi nimeyasikia mara ya kwanza hapa. Endelea na msimamo.