The Chant of Savant

Saturday 31 March 2012





Blogu hii inajua kuwa April 1 ni siku ya wajinga. Ila hatutafanya ujinga kuleta kituko chochote kwa vile hakiwasaidii wasomaji. Badala yake tunawatahadharisha wasomaji kutoamini kila habari.

Tanzania wizi wizi mtupu!






Tanzania chini ya utawala wa sasa imeanzisha mtindo wa kula kwa zamu. Kila anayepata nafasi au cheo serikalini lazima ajitafutie jinsi ya kuitumia ili kujitajirisha na familia yake. Baada ya Mwanaidi Majaar kuangukia nafasi ya ubalozi kutokana na uhusiano wake mzuri na Jakaya Kikwete, amekuwa mbioni kuhakikisha anafanya kile wanachofanya akina Salma Kikwete, Anna Mkapa, Regina Lowassa na wake wengine wa vigogo. Tofauti na wao, Mwanaidi ameanzisha NGO ya mwanae sawa na watajwa walivyoanzisha NGO kupitia migogoni mwa waume zao. Mwanzoni tuliambiwa ni Foundation kumbe kampuni ya biashara. Huyu Hassan Majaar ukiachia mbali kuwa mtoto wa balozi ni nani Tanzania?

Taarifa zilizopo ni kwamba NGO hii ya ulaji imeanzisha duka la vitu mbali mbali jijini na kuliita la hisani wakati hakuna hisani yoyote bali usanii. Je kwa mchezo huu watu wetu watanusurika?

Je picha hii inakufundisha na kukumbusha nini?


Thursday 29 March 2012

Will Gaddafi’s spy chief spill beans?

Picture loading...

 The arrest of Former Libyan strong man Muammar Gaddafi’s spy chief, Brig. Gen Abdulla Senussi, has caused much controversy in Tripoli and all over the world. This is seen as opening Pandora’s Box especially for all he served with.  


BBC reported that Senussi was arrested in Nouakhchott Mauritania after landing there from Morocco on a fake passport. After his apprehension, the new regime in Tripoli quickly asked Mauritania to hand Senussi over to Tripoli something that was not accepted by Mauritania.  

Senussi who is said to be Gaddafi’s black box is wanted by the International Criminal Court (ICC) in The Hague for various crimes against humanity alleged to have been committed under Gaddafi’s 42 years rule. “Senussi is Gaddafi's black box, he has a lot of information," Tripoli resident Mustafa Jhyma was quoted by Reuters as saying. Knowing such many secrets does not only make Senussi vurnerable but also those in power today. They would not like to see their tainted and dark past been put on the agora for every eye to see and ridicule. 

  
Senussi is also wanted in France where he faces charges involving money laundering, embezzeling public funds and misuse of power for personal gains. This is according to Intepol report quoted by BBC recently. Interpol has already issued a ‘red notice’. Senussi also is wanted by France where he faces a life imprisonment after being found guilty and sentenced in absentia after allegedly he involved in the attack on a French plane that killed 170 in 1989. What is not clear is why French authorities waited till the fall of Gadaffi to ask Interpol to make a move? And if there was a request from Interpol from the time the offence was committed, then why didn’t Interpol work on it?   

Those in the know say that if Senussi is not returned or being handed over to Tripoli, chances are; he is going to be finished before spilling the beans to the extent that the heads for the current regime will find themselves in hot soup. Senussi has many secrets of the former regime as a spy Tzar and Gaddafi’s consgliore. This creates a lot of pressure on and fear for those who served in Gaddafi’s rule but are currently serving in the National Transition Council (NTC). One of them is the head of NTC, Mustapha Abdul Jalil who then was the minister for Justice. In other words, the first person who would like to see Senussi handed over to NTC or killed is Abdul Jalil himself. Abdul Jalil wants Senussi dead or alive in order to make sure that his dirtier-- past, currently unknown-- is concealed and sealed with the death or detention of Senussi. This is obvious given that Abdul Jalil as minister of justice knows and assented for many so-called Gaddafi’s injustices or crimes against humanity. 

Another reason why the new regime in Tripoli  wants Senussi is having an access to massive investment Gaddafi made all over the world. The new regime worries that, if Senussi is left in unsafe hands, chances are, he can use financial muscles he has to make a deal and get away with it. Many analysts wonder as to why Libya’s new regime is seeking the extradition of Senussi with much more urgency even than that of wanting Saad Gaddafi being extradited from Niger. Of course, NTC knows that Senussi has more information, secrets even access to weath Gaddafi made and protected than Gaddafi’s sons.  

Now that Senussi is under arrest in Mauritania, will he be handed over? If not, will he make a deal and get away with it? Will he be handed over to ICC where he is likely to spill beans and therefore endanger the lives of current NTC tops? If he is handed over to ICC even though this is impossible due to the fact that
Mauritania is not a signatory to Rome Statue, will he keep mum and die alone? Will he use this opportunity to toast his enemies? Will he be handed over to NTC so as to be neutralized and die with his top secrets?  The answers to those questions depends on what will decided upon regarding the plight of Senussi which in essence is the plight of most of  NTC’s top brass. Will Senussi be eliminated without spilling the beans or otherwise? 
By the way, do our current Senussi-like figures scoop any reasonable lesson from such kind of goings-on?
Source: African Executive Magazine March 28, 2012.

Wednesday 28 March 2012

Baada ya mchezo huu mchafu Tanzania itabaki nini?

SI uzushi wala uchochezi. Tanzania inaelekea pabaya tena sana.
Tangu kuingia kwa mchezo mchafu wa kikundi cha watu tena wachache kujihudumia na kutafuta utajiri kwa kuwauza wenzao, Tanzania si salama ingawa hakuna milio ya bunduki.

Uliza. Yako wapi mapambano dhidi ya ujambazi, ufisadi (ugamba), biashara ya mihadarati, kurekebisha mikataba ya kijambazi ya uwekezaji ambao ni uchukuaji na uwajibikaji? Si siri.
Kwa sasa Tanzania iko mikononi mwa maharamia tuseme majambazi hasa kiuchumi. Imefikia mahali majambazi yaitwayo wawekezaji yanakuja na kutuibia mchana kweupe kwa kushirikiana na wenzetu waroho wachache tuliwaamini.

Uliza uwekezaji kwenye Shirika la Reli uliishia wapi ilipoingia kampuni ya Kihindi iitwayo RITES?
Mijitu inakuja bila hata senti halafu eti inawekeza kwa kuilazimisha serikali iwape mikopo ili waendeleze mradi! Ni wawekezaji wangapi wanakuja na briefcases zao na makaratasi na kurejea kwao wakiwa na magunia ya dola?

Uliza. Ni wawekezaji wangapi hasa kwenye madini wanamiliki ndege na viwanja binafsi vya ndege wanavyotumia kutoroshea madini yetu bila kukaguliwa?
Ni wangapi wanachafua mazingira na hakuna anayewawajibisha?
Hebu zidi kupiga mbizi kwenye uchafu huu uone mengi. Hakuna ujambazi wa wazi kama unaofanywa na makampuni ya simu kwa sasa.

Wanakuja na kuweka mitambo chakavu halafu wanawatoza Watanzania viwango vya juu vya kutumia simu.
Huwa najiuliza. Inakuwaje kupiga simu, kwa mfano, kutoka Canada kwenda Kenya nitozwe senti tano za dola na Tanzania nitozwe senti 27 za dola kwa dakika?

Wakati viwango vya Kenya ni vidogo, mawasiliano baina ya Kenya, Uganda, Rwanda hata Burundi ni bora na rahisi wakati Tanzania ni utapeli mtupu.
Mtu unapiga simu unaambiwa ongeza salio, mara namba ya simu haipo, mara simu inatumika mara hili mara lile.

Kwanini hatusikii upuuzi huu tunapopiga nchi tulizotaja hapo juu kama hakuna namna?
Ajabu ya maajabu, kila mwaka makampuni ya simu yanabadilisha majina ili kuendelea kufaidi msamaha wa kipuuzi wa kodi.

Angalia mahoteli yenu yanavyobadili majina na wamilki kila baada ya miaka mitano ili kuendelea kufanya biashara bila kulipa kodi. Angalia watu wanavyouziana makampuni waliyookota Tanzania kwa bei ya kutupwa.

Anayebishia hili ajikumbushe Richmond ‘ilijiuza’ kwa Dowans kwa bei gani ikilinganishwa na bei ya maandishi tu bila kulipa pesa iliyoianzishia biashara hii hewa.
Leo tunaambiwa kuwa pesa tunayoilipa IPTL, kwa mfano inatosha kununua na kujenga mitambo bora na mikubwa kuliko tunayolipia.

Je, kwanini tunaona kujikomboa ni dhambi wakati tukiabudia maangamizi kama haya ya IPTL na makampuni mengine mengi ya nishati.
Je, hapa hakuna rushwa na ufisadi vya wazi? Je, wahusika hawajulikani? Nani anawagusa wala kuwashughulikia? Tunakwenda wapi?

Imefikia mahali watu wakiuliza ni kwanini uchafu huu unaendelea wakati kuna mamlaka, wanakufa kwenye mazingira ya kutatanisha. Jiulize. Mbunge wetu mmoja alipatwa na nini baada ya kuhoji ni kwanini alikuwa akiona watumiaji wa mihadarati hadharani ambao wangeweza kutuonyesha wanakonunua madawa.

Tufikie mahali tuambiane ukweli bila kuogopana wala kufichana. Bila kufanya hivyo na kubadilika nchi yetu itaishia pabaya.

Ni juzi juzi serikali ya Mali imeangushwa kutokana na hasira za jeshi kushuhudia wauza unga wakiwa ndani ya serikali na serikali isifanye kitu kwa vile wakubwa zake walikuwa wakinufaika na uchafu huu.

Je, sisi tu salama na hawa wauza unga na majambazi wa kiuchumi waliotapakaa nchini mwetu? Je, wananchi wataendelea kugeuzwa mbuzi wa shughuli kila mwaka?
Huwa siachi kusema kuwa Watanzania ni viumbe wa ajabu hata kama hawana mikia au macho kisogoni.
Maana ukiangalia kwa mfano, rasilimali zao zinavyoibiwa, wanavyolanguliwa huduma kama vile umeme, simu na mahitaji mengine na wakaendelea kuvumilia unashangaa hawa ni watu wa namna gani.

Nani kwa mfano anakumbuka na kuhoji ile kashfa ya utoroshaji wanyama iliyotokea Novemba 24, 2010 ambapo ndege ya kijeshi ya Qatar ilifanikiwa kutorosha wanyama mbali mbali 130 kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro?
Je, kama KIA wana uwezo wa kutorosha wanyama hai na wengi kiasi hiki wanashindwa nini kuingiza maelfu ya tani za unga?

Ukitaka kujua nini namaanisha, watafute wafanyakazi wadogo na wa kawaida viwanja vya ndege uone walivyo matajiri wa kutupwa.

Unadhani pesa hii wanaipata wapi kama si kuruhusu uchafu na jinai kama ile ya KIA?
Nenda TRA, Bandari, Uhamiaji. Mambo ni yale yale. Uchafu, uchafu mtupu. Nani anajali iwapo wanaofaidika wameweka watu wao kufanya kazi hiyo? mfano, vituo vyetu vya mipakani vimegeuzwa maduka ya wezi wachache kupitisha wamtakaye na wakitakacho bila kuulizwa na yeyote?

Je, namna hii nchi itakuwa salama? Je, namna hii tunaweza kujisifu kuwa yaliyotokea Mali hayawezi kutokea huko tuendako ambapo wahusika wasiporekebisha hali hii wananchi katika hali yoyote wataamua ‘enough is enough’.

Tumekuwa taifa la hovyo linalowazawadia watenda maovu!
Uliza waliotimuliwa madarakani kwa kashfa wanalipwa pesa ya umma kwa kazi gani zaidi ya kupaswa kuwa mahakamani hata magerezani? Tumegeuka taifa la watenda maovu na waovu kirahisi hivi?

Je, baada ya mchezo huu mchafu Tanzania itabaki nini? Tunaviandalia nini vizazi vijavyo iwapo tunafanya mambo kama mataahira kutokana na kufikiri kwa matumbo badala ya vichwa?
Chanzo: Tanzania Daima Machi 28, 2012.

Nkapa na Wahasira mmefilisika

JUZI nilicheka hadi nikalia niliposikia kampeni za kipuuzi kule Arushameru.
Mwanzoni vyama shindani hasa Chakudema na kile cha Magamba viliposema vitafanya kampeni na kampani za kistaarabu nilidhani itakuwa hivyo.

Hivyo niliacha safari yangu ya kwenda Nairoberry kumjulia hali nyumba ndogo yangu –Muthoni. Sorry sikuwa nakwenda kwa nyumba yangu ndogo bali kumsalimia rafiki yangu Ndirangu wa Ndamu wa Jamba Nene ya Ita kule Ithekahuno. Hayo tuyaache. Ila usimwambie bi mkubwa kuwa nilisema nilikuwa nakwenda kuona nyumba ndogo kule Nyeri.

Mie siyo kama Stivi ambaye nasikia kwa nyumba ndogo si mchezo.
Lakini ajabu ni kwamba yeye ndiye wa kwanza kuwashupalia wenzake kuwa wana nyumba ndogo wakati ukweli ni yeye.

Je, hii inatokana na jamaa kutoka usingizini na kujifanya Mpayukaji asijue kupayuka kuna wenyewe? Twende kwenye siasa za kipuuzi.
Kama mnakumbuka kijiwe cha kama wiki tatu hivi zilizopita, nilionya chama cha Magamba kutomruhusu Denjaman Nkapa kwenda Arushameru.

Kwanza nilihofia angepayuka hata kulipuka na kuvuruga kila kitu ikichukuliwa kuwa tangu afanyie umachinga ikuu na kujitwalia machimbo ya Nkaa wa Mawe alijishushia heshima na kuonekana kama waganga njaa wa kawaida.

Pili, anakabiliwa na kashfa ya kuanzisha na kubariki ujambazi wa HEPA ukiachia mbali mwingine kama vile ENBIISII, Chandarua Solution Group –tafsiri neno la kwanza kwa kimombo utajua nimaanishacho.

Tatu, ana kaugonjwa wa kupayuka payuka hasa anapozidiwa kiasi cha kujisahau na kubwabwaja hovyo.
Hivi kwa mfano, kwa msomi mwenzangu na mbishi kama Beni mambo ya Vise kwamba si mtoto wa Nchonga yangekisaidia vipi chama chake?

Kama Mzee alidhani Vice ni mtoto wa nje ya ndoa yeye hana?
Namheshimu sana Mzee wetu lakini anapovamia kazi yangu ya kupayuka sitamheshimu tena.
Kama aliona kupayuka ni raha si angewasiliana nami nikampa mbinu za kupayuka bila kuchemsha.
Najua Nkapa huwa ananisoma sana. Kwanza ni mwandishi mwenzangu ingawa baada ya kuula alianza kututukana waandishi kuwa hatujasoma wakati tumekula vitabu kuliko hata yeye.
Hivi kama angeulizwa alivyouza nyumba za walalanjaa angejibu nini? Natamani nyumba zile nizibomolee mbali kama zile za Gerezani ambazo ziliuzwa kihalali na lisirikali halafu likajipiga mtama na kuzitaka kwa bei ya kijambazi.

Kwangu mimi, Nkapa kama Wahasira walichemsha. Eti linadai litapigana kwa nguvu zake zote kurejesha ardhi ya Wameru iliyoporwa nalo! Ajabu, lingekuwa na aibu hata mmoja si lingeacha kujimilikisha nkaa wa mawe ukiachia mbali kunyakua ardhi huko huko Arushameru na Ushoto kwa kina mgosi Machungi.

Tangu lini mbwa akarejesha nyama?
Nilishangaa kuona jitu zima kama Stivi Wahasira likisema eti Daktari Silaha aliiba pesa wakati wa ujio wa papa sijui dagaa sijui nyangumi.
Mbona lenyewe linalala kila siku likipokea mshahara kwa kusinzia? Je, huu si wizi tosha wa njuluku za Wabongolalanlanders?

Eti ni kweli nawe unapolala huuota urahisi? Ama kweli siku hizi urahisi hauna tena maana hadi unawaniwa na wasinziaji.
Siku Wahasira akiteuliwa nitajinyotoa roho ili nisitawaliwe tena na kilaza mwingine.
Chanzo: Tanzania Daima Machi 28, 2012.

Monday 26 March 2012

Dunia inakwenda wapi na imani haba hivi?

Snapshots 032212
Ushirikina kitu kibaya. Unagundua nini ukiangalia picha hiyo hapo? Unaweza kuamini kuwa kuna watu na akili zao wanadhani eti malaika ameonekana kwenye mawingu? Kazi kwenu.

Sunday 25 March 2012

Breaking News Wade chariiiiii!!!



Abdulaye Wade rais aliyeangushwa kushoto na rais mteule Mecky Sall

Habari zilizotufikia ni kwamba rais babu  king'ang'anizi wa Senegal Abdulaye Wade ameshindwa vibaya na mpinzani wake Mecky Sall kwenye marudio ya uchaguzi uliofanyika leo. Wade alionywa asigombee kipindi cha tatu kinyume cha katiba lakini alikataa. Sasa amefurushwa kwa aibu na zomeazomea. 


Kwa mara nyingine chama tawala kimfurushwa madarakani kwa amani kupitia sanduku la kura.


Hata hivyo Wade ameonyesha ukomavu wa kisiasa kukubali kushindwa tofauti na vibabu kama Mwai Kibaki wa Kenya na Robert Mugabe wa Zimbabwe. Alluta Continua Afrika kunazidi kucha. 

Friday 23 March 2012

Uwekezaji na Tanzania ya kesho





mtoto akiwa amelazwa juani asijue atalala wapi

Kamanda wa polisi wa Ilala Faustine Shilongile akifurahia kazi safi wanayofanya polisi kulinda usalama wa watu wasio salama.

Kijiko kimefanya kazi yake. Waathirika watajiju.





Hapo juu ni mtoto mchanga akiwa amelazwa nje baada ya nyumba yao, kwennye zilizokuwa nyumba za wafanyakazi wa Bandari eneo la Shule ya Uhuru Dar es salaam kubomolewa kupisha ujenzi wa kituo cha mabasi yaendayo kwa kasi. Kweli wawekezaji wameanza kwenda kasi. Ukiangalia kichanga hicho na nchi inavyouzwa na watu wake unajiuliza swali moja kuu: Ni nani aliwaroga watanzania kuwa kondoo kiasi hiki?


Leo wawekezaji wamefikia kujenga viwanja vya ndege kwenye machimbo na kutorosha madini yetu mchana kweupe. Wawekezaji wamefikia kutulangua karibu kila kitu kuanzia simu hata dawa nasi tu kimya. Wauza unga sasa wana serikali ndani ya serikali na hakuna anayewagusa! Majambazi ndiyo wafadhili wakuu wa CCM. Rejea kisa cha Massawe wa Friendscorner kubainika ni jambazi la kutupwa na hapo hapo ni mfadhili tegemewa wa CCM.


Leo akina Lowassa wanalipwa kodi zetu baada ya 'kustaafu' kwa kuingiza faida ya Richmond. IPTL inaendelea kutuumiza na kutupandishia gharama za umeme ilhali pesa tunayoilipa IPTL inatosha kununua mitambo mipya na ya kisasa na kushusha bei ya umeme. Uliza wako wapi wahindi wa RITES waliokuja na mikoba ya makaratasi na kuondoka na magunia ya dola. Yote hayo ni tone katika bahari. Onyo: juzi serikali ya Mali iliangushwa kutokana na kukithiri kwa uchafu kama huo hapo juu. Kazi kwenu wenye nchi.



Wednesday 21 March 2012

Maskini Benjamin Mkapa!

“Kwa nguvu zangu zote wakati nina uhai, nitatetea haki za wananchi wa Tanzania pamoja na kumilki ardhi na kuitumia kwa maendeleo yao,” Hiyo ni nukuu ya aliyosema rais mstaafu Benjamin Mkapa alipokwenda kumnadi mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki.

Kwanza, kwa wengi, hiki kimeonekana kuwa kichekesho cha aina yake kinachomvua Mkapa nguo kiasi cha kuonekana kuishiwa mbele ya jamii. Kwani wengi wanauliza: Mbona hakufanya hivyo yaani kulinda haki za watanzania kwa nguvu zake zote wakati akiwa madarakani zaidi ya kujinyakulia mali za umma? hata hivyo, hapa kuna somo kuwa kila chenye mwanzo kina mwisho na ukipewa dhamana ukaifuja unaishia kuishi kwa aibu, kutegemea kulindwa na hata ghilba na hadaa. Kwa mtu wa hadhi ya Mkapa, kupayuka si saizi yake achia mbali kuongopa mchana kweupe. Maskini Mkapa!

Wakosoaji wanahoji: Mkapa anataka kumdanganya nani wakati siri zake ziko ugani kwa miaka nenda rudi? Hivi Mkapa anadhani watanzania ni wasahaulifu na mataahira kiasi hicho? Je hapa nani anajidanganya ukiachia mbali kudanganya? Mkapa hawezi kusameheka bila kuleta utetezi wake tena unaoingia akilini. Hakuna shaka kuwa sasa Mkapa anahaha kujua nani atamrithi Jakaya Kikwete ili amhakikishie ulinzi asishitakiwe kwa kashfa zake na familia yake. akitaka msamaha siyo ajitetee tu bali arejeshe mali za umma na kuomba msamaha kwa watanzania akikiri kuwa alikosea na kushawishika kiasi cha kuchafua ofisi waliomwamini kuiendesha kwa niaba yao.

Wengi wanashangaa kama kweli wananchi wa Arumeru Mashariki watakubali kugeuzwa wajinga na wapumbavu ambao wanaweza kuipigia kura CCM kwa kubariki kile kinachoonekana kwa wachambuzi wengi kama uongo wa Mkapa. Wengi wanahoji: Je Mkapa anaishi dunia gani ambaye hajui kuwa wananchi hao hao anaowahadaa kuwa atapigania haki zao kwa nguvu zake zote hadi kufa wanaendelea kukumbwa na matatizo yatokanayo na uhaba wa ardhi baada ya ardhi yao kubinafsishwa kwa marafiki na washirika wa Mkapa tena chini ya utawala wa Mkapa huyo huyo. Amenikumbusha kisa cha Alikwina yaani alikuwa wapi? Mkapa ulikwina ? Badala ya kujibu hoja vilivyo alikimbilia kujifanya mwanafamilia ya marehemu baba wa taifa kiasi cha kuwatoa wengine walioamua kumpasulia bomu ambalo limemuacha hoi.
Inashangaza kwa mtu mwenye hadhi ya Mkapa kukosa kumbukumbu kiasi hiki ukiachia mbali kusema vitu visivyoingia akilini kama vile. Kwa walioshuhudia au kusikia aibu iliyomkuta rais mstaafu Benjamin Mkapa wanajiuliza kulikoni.
CCM iliomba kuwepo na kampeni za kistaarabu na si matusi na uongo. Ajabu CCM hiyo hiyo ndiyo ilikuwa ya kwanza kuvurumisha matusi ukiachia mbali kusema uongo. Matusi yasiyo na lazima wala saizi ya Mkap, hata hivyo si kosa la Mkapa. Kwani CCM sasa ni chama kilichoishiwa kuliko wakati wowote wa historia ya kuanzishwa kwake.

Watu wanajua ukweliNBC, EPA IPTL Kiwira Tanesco-Net Group Problems ambazo zilikuwa dhana za utawala wa Mkapa kujikusanyia pesa binafsi nyuma ya pazia. Nani mara hii Mkapa alivyotishia kila aliyejaribu kumpa ushauri kwa mfano asiuze NBC? Ni juzi siri ya siri ilifichuka kiasi cha Mkapa kutuhumiwa kuwa nyuma ya kifo cha baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere kama ilivyodaiwa na mwanae ambaye naye hajajibiwa na Mkapa.
Kimsingi, ujio, na maneno na uwepo wa Mkapa Arumeru Mashariki haukuisaidia CCM bali kuiangamiza. Maana watu si wapumbavu wala wajinga kama anavyodhani. huwezi kwenda jukwaani ukahubiri matusi na uongo chama chako kikapewa kura hata kama wapiga kura wanakupenda au kukipenda chama chako. hapa hapendwi mtu bali haki na maendeleo ambavyo CCM imeshindwa kutimiza kwa miongo iliyokuwa madarakani zaidi ya kundi dogo la watu kujihudumia kwa kuwanyonya walio wengi ambao sasa linawahadaa na kuwafya vipofu na mataahira.
Hivi Mkapa anadhani watanzania wanasahau athari za kufanyia biashara ikulu ambapo wachukuaji wanaoitwa wawekezaji walifanikiwa kuiweka nchi yetu mifukoni mwao kwa kuwahonga wakubwa huku raslimali zetu zikigeuka laana kwetu? Kama amesahau aende Mara, Mwanza, Shinyanga hata arudi huko Arumeru aone madhara ya sera na uroho wake. Aende aone watu wake wanavyowanyanyasa watanzania huku wakipora raslimali zao na kuacha madhara makubwa kiikolojia. Maskini Mkapa hayaoni haya yote. Bado anaotea siasa za kibabe na urushi za wakati wake ambapo alidai kuwa sera yake ilikuwa uwazi na ukweli kumbe akimaanisha kinyume kama ilivyokuja kubainika kuwa sera yake ilikuwa ni uchukuaji, usiri na uongo.

Mkapa anapaswa kuambiwa kuwa aache kudhani kuwa watanzania ni kama mawe ambayo huwa hayabadiliki wazi wazi ingawa yanabadilika. Maskini Mkapa. Aibu! Wahenga waliasa kuwa asiyejua maana haambiwi maana na asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Heri Mkapa angejiendea Moshi, Lushoto au Mtwara akajipumzikia kama siyo kulowea Upanga kuliko kuzidi kuwachokoza watanzania aliowadhulumu yeye familia yake na marafiki zake alioshirikiana nao kwenye makampuni yao ya kuiba Kiwira.

Tumalizie makala hii kw a kumtaka Mkapa akumbuke maneno haya wakati akitafakari nafasi yake kama rais mstaafu. “Ndugu zangu msidanyanyike na kuendelea kuwasikiliza CCM miaka yote wameshindwa kurejesha ardhi ya Meru sasa wanaibuka…..huyo Mkapa alishindwa akiwa rais sasa amekaa nyumbani akisubiri posho ataweza kumshauri rais awarudishie ardhi yetu?” Mbunge Israel Natse (CHADEMA) jimbo la Karatu. Mnaweza kuongeza kuwa: Kwanini Mkapa kama ni jabali kweli hataki kujibu tuhuma za uchafu aliofanya akiwa ikulu?
Chanzo: Tanzania Daima Machi 21, 2012.

Mpayukaji alizwa hotelini akitanua na totos



Najua wengi hapa wameishaanza kupiga ramli kuwa huenda naongelea maeneo ya Beverly hills au New York kwa matajiri. Kwa waliowahi kuishi New York watakuwa wanajua maeneo kama Westbury, Brigdehampton, Sands Point na kwingineko ambako wenye nazo ima huishi au kwenda kutanua hata kwa kufanya mambo ya kipuuzi.
Pia wapo wanaodhani kuwa napanga kwenda kwa walevi wa Bongosalama kuwashitakia walioniibia kama siyo kutafuta kuhurumiwa kwa uzembe na sababu ya kweli iliyosababisha nilizwe. Mmenoa! Sikuibiwa New York wala siandiki kuomba kukutana na waze sorry walevi wa Dalasalama.
Mwenzenu juzi nilitinga kule Ngorongoro kwenye hoteli ambayo jina lake siri yangu kutanua na dogodogoz baada ya kumuacha bi mkubwa solemba. Baada ya kuwa amenichosha kutokana na kunenepeana ukiachia mbali kuwa bize kutumia nafasi yangu kutafuta ulaji binafsi yeye na ndugu zake, nilijihisi kumchoka. Hivyo, niliamua kutafuta vidosho lau nijiburudishe. Niliamua kwenda kufanyia ufuska wangu sehemu iliyojificha ili asininase. Nilijua nimepata kumbe sikujua nilikuwa nimepatikana. Nilijiona bonge ya mjanja nisijue mwisho wa yote nitaonekana fala haswa! Uliwahi kusikia stori ya paka mrembo yaani mama anayerembua mimacho kama hururaini la jamaa zangu fulani?
Baada ya kutinga zangu Ngorongoro nikijifanya nilikuwa kule kikazi, niliingia mitaani kuwasaka ndogondogoz bila kujua ni hatari. Ama kweli yule jamaa aliyeimba kuwa ndogondogo kwa pesa ni hatari hakukosea hasa mwenye kuwa nazo anapokuwa kigogo kama mimi. Hivyo basi, baada ya kutega nyavu zangu na kunasa kidosho cheupe, tuliamua kwenda zetu chumbani kwangu kujivinjari. Tulijivinjari kweli kweli hadi nikachoka sana. Kabla ya kulala tulipata kanywaji ili kuamsha mwenembago. Kumbe kale kanywaji kalikuwa kamewekewa bwimbwi kiasi cha kunifanya nilale kama kichanga. nilipokuwa nakoroma kama gogo, si dogodogo aliamka na kusanya kila nilichokuwa nacho kuanzia laptop zangu nne, dolari 80,000 nilizokuwa nimehongwa na jamaa waliotaka niwape tenda ya kusambaza kahawa kijiweni, madafu 20,000,000 ambayo yalitokana na msaada wa shirika moja ambalo sitaki kulitaja na hata god father yangu yaani pupi yangu. Nilipokagua vitu vyangu nilikuwa kuwa briefcases mbili zimekwenda, Sanduku la silaha ya kujikinga na umeme au kondoo muu nalo limekwenda. Inaonekana huyu manzi hataki kufa kwa miwaya. Yaani anaondoka hata zana zangu ili nisiwanonihino wengine siyo?

 
God father imekwenda, suruali, viatu, saa hata leso yangu vyote vimekwenda. Changu huyu alijua kukomba usiambiwe! Yote tisa. Hivi bi mkubwa akiipata naye si ataamua kunikomoa kama hana akili nzuri? Maana kwa mfumo dume huu tumekuwa kama vipofu bila kuangalia upande wa pili. hivi bi wakubwa zetu wakiamua kulipiza kisasi kuna mtu atapona kweli?

Baada ya kugutuka na kujikuta mimi na mashuka ya hoteli, nilipigwa na butwaa huku nikihisi kuchanganyikiwa jinsi nitakavyotengeneza stori ya kusadikika kwa ndata. Unadhani bila kutengeneza stori bi mkubwa angenielewa? Laiti angejua kilichosababisha nikwapuliwe wala asingehangaika kunionea huruma bali kunikomoa. Kwa vile wakubwa huwa hawaadhiriki, ilinibidi nicheze chess na ndata wambambikizie mzoba mmoja kesi ili kuninusuru. Unacheza na uzito nini?



 
Unaweza kuamini kuwa kama changu aliyeniliza angekuwa jambazi ningefungwa? Maana wakati akinisanya, nilikuwa kulikuwa na bastola niliyokuwa nimeazima kwa jamaa yangu ili kujilinda. Pia kulikuwa na SMG kali sana. Hamna haja ya kuanza kupiga ramli tena. Kinachoitwa SMG siyo bali jambia la kimasai. Hata hiyo bastola si ya kweli bali toy lake. Hayo tuyaache. Maana nisingeweza kuwa na bastola hata kama siku hizi ni ruksa kuzinunua na kuzitumia utakavyo kama brother Dittope. Kwa mtu kama mimi SMG la nini wakati mimi si jambazi? Hii imenikumbusha rafiki yangu mzee Headguard Makorora Majogoo aliyesafiri na gobole lake toka Bongo hadi ugabacholini bila kustukiwa. Walijisemea wahenga. Unaweza kumtoa mtu porini lakini huwezi kutoa pori kichwani mwake. sasa mzito mzima na misilaha ya kivita ya nini? tena hali inakuwa mbaya unapokuwa umebeba midude kama ile halafu ukajiingiza kwenye uchangudoa na uhuni kama ilivyotokea. Licha ya kunitokea mimi, imetokea wapi? Nachema chichemi njomba.
Pia mabingwa wa udaku nawashauri na kuwaonya wasihusishe kisa changu na cha yule kijogoo mwana wa Milima ya Kigoma aitwaye jina mumewe Eva. Yeye aliafanya uhuni watoto wa mjini wakamuingiza mjini kikweli kweli. Kwanza mzito na SMG wapi na wapi kama siyo ulimbukeni na ushanba? Wazito wanalindwa na bodigadi. Mi-SMG na mibastola ya nini kama siyo kuwa na kazi zaidi ya moja? Maana bila kuwa na shughuli za siri mtu wa aina yake asingeweza kujizungushia mizana mizito mizito kama Osama bin Laana.

 
 
Turejee kwenye kisa changu. Kwa vile huyu changu aliyeniibia amejifanya mjanja, basi ajue amejiharibia yeye na vyangu wote wa kaya hii. Maana mwakani nitakapogombea uzito na kuupata nitakuwa sichukui vyangu wanuka jasho wa kaya hii. Badala yake nitakuwa nachukua vikinda vya shule au chuo na kwenda kutanua navyo majuu ambako siwezi kugutukiwa wala kuibiwa. Ikizidi nitakuwa nachukua vyangu wa kizungu badala ya hivi vya Kiswahili ambavyo vina shughuli zaidi ya moja; yaani uchangu na ujambazi. Kuanzia leo natangaza rasmi. Changudoa yeyote atakayepita mbele yangu naramba shaba au njaramba. Sina mchezo tena. Machangudoa wote wawe wa kisiasa au kingono washindwe na kunyong’onyea. Na shetani aliyenishwawishi nikalala na changu akaniibia naye ashindwe pamoja na changudoa wake.
Hivi hii ni kweli? Nimeinyaka kuwa tangu jamaa alizwe kule kwenye mji karibu na bahari, vyangu sasa wanaipata fresh hasa pale ndata wanapowasanya kulipiza kisasi kwa kuingizwa mjini bwana wao. kuna mbea amenipa stori kuwa ndata nao wana lao. Maana wakiwakamata machangu huwatoa mchicha hata huduma ya chap chap. Jamani, miwaya itatumaliza hata tukijizungushia mipisto na miesmjii.
Chanzo: Tanzania Daima Machi 21, 2012.

Sunday 18 March 2012

Arumeru wangemuuliza Mkapa Kiwira, EPA na NBC



Wengi Wanaojua madudu ya rais mstaafu Benjamin Mkapa walishangaa mantiki ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumpa jukumu la kurejesha jimbo la Arumeru Mashariki baada ya kufariki kwa aliyekuwa mbunge wake. Kwa wanaojua jinsi Mkapa alivyomwangusha kipenzi chao Baba wa taifa mwalimu Julius Nyerere, walishangaa busara hii ya kumteua mtuhumiwa wa kufanya biashara ikulu, kuridhia ubinafsishaji wenye kila shaka, kujitwalia mali ya wananchi yaani mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira alioutwaa akiwa rais akishirikiana na waziri mwandamizi, familia zao na hata wakwe wa Mkapa. Hata hivyo habari zilizotufikia ni kwamba Mkapa amegwaya kwenda Arumeru Mashariki. Hili halituzuii kuuliza maswali ambayo angepambana nayo kule.
Wenye kumbukumbu na busara walishangaa kuteuliwa kushika usukani katika kampeni kwa mtu aliyewadhurumu wananchi benki yao ya biashara (NBC) iliyokuwa ikiingiza faida kuliko ilivyoelezewa. walishagaa mtu kama huyu aliyejenga msingi wa ufisadi na wizi wa wazi wazi unaoendelea kama kuingia mkataba wa hatari wa IPTL kupewa jukumu kubwa kama hili. Je huu si ushahidi kuwa CCM imeishiwa na kuparaganyika? Basi kwa niaba ya Mkapa iulizeni CCM itampelekea ujumbe wake. Je kule kutangaza mali zake wakati wa kuondoka madarakani kuliishia wapi? Muulize ni kwanini alibariki wizi wa pesa za umma chini ya ujambazi wa EPA ambapo mabilioni ya shilingi za wananchi yaliibiwa kugharimia uchaguzi wa aliyemfuatia ambaye naye, kama Mkapa, huwa hataki kujibu tuhuma. Endeleeni kumuuliza. Ni kwanini aliruhusu mkewe kujipatia utajiri wa haraka na haramu kupitia biashara ya NGO. Muulizeni ule uchumi wa kisasa alioahidi kwanini uligeuka uchumi wa kisasi na kifisadi. Muulizeni alikopata jeuri ya kujiuzia nyumba ya serikali na kuwapa marafiki zake nyumba nyingine. Muulize hata hayo mabilioni ya kujengea hekalu Mkuzi Lushoto yalitoka wapi?
Mngeweza kuendelea kumuuliza Mkapa hata CCM ni kwanini aliamua kukikabidhi chama cha wanyonge kwa mafisadi huku akiwaacha wakiwa yatima. Muulizeni ni kwanini ameendelea kunyamazia tuhuma zote zinazomkabili yeye, familia yake na marafiki zake? Je ataendelea kuishi kwa hisani ya Kikwete hadi lini? Kitu ambacho kiko wazi ni kwamba Mkapa hawezi kupata jibu lenye kuingilia akilini hata la swali moja. Sana sana akifika Arumeru Mashariki ataenda kupiga siasa za kukandiana na kujilisha pepo kuwa wapinzani hawana kitu wakati asiye na kitu ni yeye na chama chake ambacho kimeonyesha kuishiwa kulhali.
Kipindi hiki wananchi wa Arumeru Mashariki msikubali majungu naporojo za kwenye majukwaa bali muwape mtihani hao wanaotaka kuwawakilisha kuhakikisha wanaeleza na kuwahikikishia kuwa hawatakwenda kuwakilisha matumbo yao na koo zao hasa wale wanaoendekeza siasa za kurithishana kama ufalme.
Maswali mengine ya kumuuliza Mkapa ni kwanini chama chake na serikali yake wameamua kwa makusudi kutumia raslimali za umma kwa manufaa yao binafsi? Watu wa Arumeru Mashariki wanajua jinsi mbunga za wanyama zilizowazunguka zinavyonufaisha wageni na wenye madaraka wachache huku wanancni wakizidi kutopea kwenye umaskini wa kutengenezwa na waroho wachache wanaokaa ikulu kufanya biashara ya kujitwalia mali za umma. Hawa ni wezi wa kawaida hata kama wana madaraka. Hawa ni watu wa kuzomewa siyo kusikilizwa wala kushangiliwa. Kufanya hivyo ni kujidhalilisha hasa wananchi watakaotapeliwa na wezi wanaowajua fika. Je wananchi wa Arumeru Mashariki watajiruhusu kutumika kama daraja na ngazi ya watu waongo wachache kupandia kwenda kwenye neema itokanayo na kuwahujumu hao hao watakaopiga kura?
Kituko cha pili ni ubunge unaoanza kuwa wa kurithishana ambapo anayepeperusha bendera ya CCM ni mtoto wa aliyekuwa mbunge. Je tunaaza taratibu kujenga msingi wa siasa za kihindi? Hata hivyo, tujiulize, nani msafi kwa sasa anayeweza kuheshimika kwa wananchi ndani ya CCM baada ya wote kuchafuka au kuchafuana? Rejea kambi moja ya CCM hiyo hiyo iliyomtangaza mteule wa CCM Arumeru Mashariki kuwa si mtanzania. Leo uraia wake umepatikanaje haraka hivi?
Kama wananchi wa Arumeru Mashariki wanataka ukombozi na hawako tayari kutumiwa na wezi wenye madaraka basi wamuulize Mkapa swali moja kuu na la maana: ilikuwaje akajitwalia mali ya umma wakati alikuwa akituahidi kujenga uchumi imara ulioishia kuwa legelege?
Chanzo: Dira ya Mtanzania Machi, 2012

Wednesday 14 March 2012

Kikwete: Globetrotting Interrogated


President Jakaya Kikwete: Bye Bye!?


The editorial of one Swahili Daily, Tanzania Daima of February 22 carried a title: “Msafara wa Rais Nje Upunguzwe,” or literally, the Presidential entourage abroad should be cut down. This has been a thorny issue for Tanzanians especially when it comes to extravagance by their globetrotting ruler, Jakaya Kikwete.
Since he came to power six years ago, Kikwete has made over 300 tours abroad, an average of 50 trips annually or one trip in every two weeks. He is second to none in Africa when it comes to touring foreign countries ahead of presidents Yoweri Museveni (Uganda) and Jacob Zuma (South Africa). Analysts wonder why he conceals the names of his delegates, for during his foreign tour, only his wife is mentioned alongside him. It seems the list of delegates on his trip to Britain leaked.


Kikwete surprised the country when he left for Davos to attend the World Economic Forum (WEF) while back at home, Tanzanian doctors were on strike demanding good payment. Many patients lost their lives as the government maintained that it did not have money to give to doctors. To Kikwete, the doctors’ strike could not stand in his way. Fortunately for him, Tanzanians are ‘peaceful’ as politicians in the country like to refer to them.


If Kikwete does not have any fiscal discipline, what about those under his watch? Since he came to power, Kikwete has been accompanied by friends and controversial businessmen who have allegedly committed grand corruption in the country. Tanzanians want their president to be tamed and be held accountable for the hard-earned taxpayer money.


Despite all noises, Kikwete has kept mum and is doing more of his globetrotting. Tanzanians have consequently nicknamed him ‘Vasco da Gama,’ or ‘Tourist President.’ As of 9/9/2011 when Kikwete toured Kenya, he had already made 316 tours abroad since coming to power in 2005! Even Ian Khama of Botswana with its stable economy has not done this. Kikwete is traveling more often than presidents and PMs of donor countries such as the US, Canada and Britain! For example, as of November 19, 2011 President Barack Obama had made just 24 foreign tours since he came to power. This translates into eight tours annually.


Kikwete is doing exactly what Uganda’s President, Yoweri Museveni has been doing for decades. According to the Observer of February 22, 2012, UShs 3.810 billion was approved for State House travels in the financial year 2010/11 even though figures indicated that Museveni used UShs 7.423 billion to visit 13 countries, host 11 heads of state and foreign dignitaries, and to attend 12 regional and international meetings. That means the Shs 5.055 billion Museveni wants this financial year might actually shoot up.


Tanzanians are agitating that Kikwete’s trips abroad be probed after he left for Britain accompanied by 40 people. How can a country whose budget depends on donors by 40% be extravagant at a time when many strong economies are grappling? When will he sit in office and serve the people?
Source: The African Executive Magazine March 14, 2012.

Nilichojifunza kutoka mgomo wa madaktari, makala iliyoichefua ikulu na kutishia gazeti

INGAWA mgomo wa madaktari wa nchi nzima ni tukio lililosababisha vifo ambavyo si kazi ya Mungu bali serikali, kuna somo umetoa.
Sijui kama watu wengi hasa waathirika wameliangalia kama mimi. Wenye akili wanasema kila tukio limtokealo binadamu mwenye akili ni darasa tosha. Hivi ndivyo ilivyokuwa kwangu binafsi kama mwana taaluma na mkereketwa, ukiachia mbali kuwa mwanaharakati wa haki za binadamu.
Hata kama siishi Tanzania, bado nayajua masahibu na mazingira ya watu wetu. Hivyo siandiki kutokana na hasira ya kuathiriwa na mgomo wa madaktari kwa vile nilipo sina upungufu wala shida ya huduma ya madaktari, ikichukuliwa kuwa afya ni haki ya msingi ya kila mwananchi (hapa si Tanzania).
Siandiki kujisifu bali kuchochea hasira na welewa wa ndugu zangu Watanzania. Sitaki nieleze hali ya afya hapa Canada ikoje kwa vile kila mtu anajua kuwa kuna mfumo mzuri kuliko hata jirani zetu kusini, yaani Marekani. Ukimwambia Mcanada kuwa afya si haki ya binadamu anaweza kukushauri ukapimwe akili. Hayo tuyaache.
Katika mgomo uliokwisha ambao umezaa mwingine nimejifunza yafuatayo:
Kwanza, rais wetu haambiliki wala hasikii na sijui hii inasababishwa na uwezo wake wa kuelewa au anavyojiona baada ya kuwa rais.
Maana ukiangalia yule Kikwete tuliyeambiwa ni kipenzi cha watu na chaguo la Mungu unashangaa inakuwaje kipenzi cha watu na chaguo la Mungu anakuwa mkatili ambaye hajali hata taarifa kuwa kuna watu wamepoteza maisha kutokana na mgomo.
Unashangaa alipopata mshipa wa hata kuweza kwenda kwenye mkutano usio na umuhimu wala ulazima huku watu anaowaita wake wakifa kutokana na uzembe wa kawaida wa wateule wake! Kama hutajizuia kuhukumu ili usije ukahukumiwa, unaweza kumuita hata majina mengine ambayo si sahihi.
Sitaki nifikie hapo. Unashangaa ni baba au mama gani anaweza kwenda kwenye biashara wakati wale anaowaita watoto wake wakiugua na kufa kutokana na sababu anazoweza kuzuia hata kuingilia, achia mbali kuzuia.
Hivi waliopoteza maisha wangekuwa watoto wa Kikwete hata wapendwa wake kama vile Haji Mponda na Lucy Nkya, angeweza kupata hamasa kwenda Davos huku akiacha wakiteketea kwa kitu kinachohitaji si pesa wala nini, bali tamko lake? Je, huu ni ubinafsi na upogo kiasi gani?
Hakuna haja ya kupindisha maneno, rais wetu, sijui wao, hajali. Maana angekuwa rais wetu angetujali badala ya kujali kujilisha pepo kwenye vikao visivyo na ulazima ikilinganishwa na wapendwa wetu waliopoteza maisha, ukiachia mbali wale wanaouawa na polisi wake.
Siachi kujiuliza si mara moja wala mbili. Hivi hawa waliopoteza maisha wangekuwa watoto wake au hata mkewe angefanya alivyofanya? Lakini atajalije wakati yeye na familia yake wanatibiwa nje kwa pesa ya walalahoi wanaouawa na serikali kwa kuwadharau na kuwanyonya wananchi?
Nasema hivi kutokana na yaliyotokea. kwa wale waliopoteza ndugu zao serikali kwao haina maana na ni mnyonyaji wa kawaida.
Maana walipoichagua walijua itaingilia kwenye hali kama hizi. Kutofanya hivyo kunaifanya kupoteza uhalali mbele ya macho yao hata kama wanaogopa kuifurusha kutokana na woga ujinga na hata kuishi kwa matumaini.
Kitu kingine nilichojifunza ni kwamba Watanzania ni watu wa ajabu ambao hawana tofauti na kondoo kwa kushindwa kuwaunga mkono madaktari. Usishangae ukakuta wanawalaumu madaktari bila kuangalia upande wa pili ambao unatibiwa nje.
Hebu jiulize. Rais anaandamana na watu 40 kwenye ziara ya kutanua huku akiacha umma unateketea. Anapata wapi hiyo pesa ya kufanya hivyo kama si kutojali? Cha msingi cha kuzingatia ni kwamba ni hao hao wadharauliwa na wapuuziwa wanaokatwa pesa itokanayo na kazi na jasho lao kumlipia rais na wapendwa wake kwenda kutanua wakati punda hao hao wanaomwezesha wakipukutika kama wadudu yeye asihangaike hata kutumia akili ya kawaida achia mbali elimu.
Kitu kingine nilichojifunza japo kinatia aibu ni kwamba wateule wa rais si wa kuguswa hata wakifanya madudu kiasi gani. Rejea Mponda na Nkya na wanaodaiwa kughushi vyeti vya taaluma. Yuko wapi bwana EPA bin Kagoda? Si anaendelea kutumia mahakama zetu na za kimataifa kuvuna pesa yetu huku tukijua mchezo wote na tusichukue hatua?
Rais yuko tayari kuwatoa kafara wananchi ili kuwalinda wateule wake ambao kwake ni kila kitu na si wapiga kura.
Hata hivyo ana shida gani na wapiga kura wakati hana mpango wala haki ya kugombea tena? Je, huu si utapeli wa kimfumo ukiachia mbali kuwa unyama wa ajabu ambao hata simba na fisi hawawezi kuufanya?
Kitu kingine ni kwamba Tanzania ina ombwe kubwa la uongozi kuliko ambavyo imewahi kutokea. Kiongozi wetu huyu ni ajali ya kihistoria kutokana na ukosefu wa upendo na heshima kwa wananchi, amembebesha zigo waziri mkuu kiasi cha kuonekana mbaya wakati mbaya si yeye .
Kimsingi, kinacholisumbua taifa ni ibada za sanamu, ambapo rais anaombwa badala ya kuamrishwa kama mtumishi yeyote wa umma. Nashindwa kuendelea.
Chanzo:Tanzania Daima Machi 14, 2012.

Wanawake wa Nairoberry ni kiboko ya wanaume


Simon Kiguta akiwa kwenye Hospitali ya Nyeri Feb. 11, 2012. Alikatwakatwa mapanga usoni na mkewe baada ya kurejea nyumbani  usiku akiwa amelewa. (Joseph Kanyi/Nation photo)
Baada ya kutoka zangu London juzi nilipitia Nairobi kuongea mawili matatu na wanakijiwe cha River Road na Ngala. Sikukwa na mpango wa kusimama kidogo Nairobi. Ila nikiwa zangu London Mureithi ambaye ni mwenyekiti wa Kijiwe kile alinitwangia simu akiomba nipitie Nairobi lau nitoe ushauri.
Nilifaidi sana uzuri wa mji wa London. Barabara zote zina lami, taa, zinapigwa deki usiambiwe. Nilipofika Heathrow airport, sorry, International Airport nilitaka kuzimia nilipolinganisha na jiji letu la uchafu na ufisadi liitwalo Chafusalama.
Sikuona mgambo wa site mamantilie wala wazee wa mabao kwenye barabara za London. Kitu kimoja kilinistua sana-London kaya inachomwa hadharani na hakuna anayejali! Nilipomuuliza mvuta kaya mmoja akacheka na kusema kuwa kaya haina tatizo kwa taifa bali kwa mtu binafsi. Hivyo, nami niligundua kuwa kumbe hapa kwetu heri turuhusu watu wajichomee kaya kuliko kuruhusu ufisadi. Maana ufisadi unaumiza wengi. hata uchafu wa miji yetu ni hatari kwa kila ajae na aishie kwenye miji yetu. Ni ushahidi wa uchafu wetu wa kitabia.
Najua nikirejea kijiweni kwangu wengi nitakaowasilimulia usafiw a London watanisuta na kuhoji kama naona hivvyo kwa wenzangu nashindwa nini kutekeleza kwangu? Najua wengi wataniona kama juha na mtalii asiyejifunza. Hata hivyo tuache utani. Tuna tatizo tena si dogo. Yaani tunashindwa kujifunza hata mambo ya msingi kama usafi, mipangilio ya miji na mambo madogo kama haya? Au nayo tunataka waje wafadhili watusaidie kama walivyofanya kutuchimbia vyoo tukaishia kuvichafua?
Tukirejea kwenye kijiwe cha River Road Nairoberry ni kwamba siku hizi kule umeibuka mchezo wa akina mama kuwashikisha adabu waume zao. Ukichelewa kurudi unapatiwa. Wajua kupatiwa maana yake nini? Kuadhibiwa. Ukishindwa kufanya shughuli za ndani hasa za night unapatiwa. Ukitoroka kwa nyumba kwenda kula kwa hoteli, ukirudi unapatiana adhabu kama kawaida. Ukinywa sana kanywaji na kushinda kumudu idara zote, unapatiana adabu.
Huwezi kuamini kuwa juzi nilikuwa kwenye mahakama ya Kilimani kushuhudia mama mmoja akikabiliwa na kosa la kumpiga mumewe hadi akazimia. Toka na vipigo vya hapa na pale vya mara kwa mara, walume wa nchi ya Nyayo wameamua kuanzisha chama cha kulinda haki za walume. Kunogesha stori ni kwamba kipindi nilichokuwa kule, walume wote walikuwa wamekubaliana kugoma kula chakula nyumbani ili akina mama wapunguze morali wa Kikyuki.
Hakuna kitu kiliniua kama maongezi haya kijiweni. Mara anakuja Wagacohi na kuamkua, “Kohani atya?”
Njoroge na Wamauseto wanaitikia, “Kutiri na kaolu.”
Wagacohi anaendelea, “Mnajuanga kuwa Ithe wa Kinywa amepigwa na bibi yake hadi akepelekwa hosi?” Hosi maana yake ni hospitali.
Anaendelea, “Nyina wa Kamuyu ameniambia kuwa alipokwenda kunywa akaselewa kurudi akapatiana adhabu kali sana.”
Gathuma anadandia, “Haki mimi bibi yangu akipatiana adhabu na mimi nitaua yeye.” kabla ya kuendelea, Gitau anachomekea, “Kama umeoanga Central hasa Nyeri jua unapigwanga tu. Vinginevyo uwe umeoa kibeti cha Kikamba.” Wamuseto hana mbavu. anasema, “Haki, kwetu Matuu, Mbooni na Woote bibi hapingangi bwana. Sisi wakamba bibi akipinga bwana atalaaniwa aote devu. Kibeti ya Kikamba siyo Kama hii ya Kikuyu.” Anakunywa kahawa yake na kutafuna mirungi kidogo na kuendelea, “Wajua siku moja mimi naona bibi kule Ithekahuno akitwanga bwana hadi bwana anakufa kwa muda?”
Anamalizia, “Ukiona bibi anatwanga wewe understad wewe ni nugu-nyani.”
Mzee Gate anachomekea, “Wacha mabo yako wewe. Bibi akiamua twanga wewe anatwanga tu. Hukuona Luse alivyopiga watu ya habari pale Nation na hakuna ameshitaki yeye? Hata Kebaki mwenyewe hasemangi Luse akileta matata.”
“Kama munene kama Kebaki anapindwa nani wewe ulete nyoko nyoko kwa bibi ya kisasa asitwange wewe?” Mara mzee Gate ananigeukia. “Kama unataka bibi asipige wewe nenda kanunue bibi TZ. Huko nasikianga wanasema tafadhali wacha kuselewa na kurudi usiku badala ya kupatiana adhabu.”
Wamuseto anamuunga mkono mzee Gate, “Nasikianga watz ni wapoa sana. Tena ni wabeautiful.”Mie sina mbavu.
Tukiwa tunaendelea kupata kahawa na kutafuna miraa si alikurupuka rafiki yangu Ndirangu. Anakuja akipiga kelele, “Woi woooi, nakwa nie yaani nakufa mie.” punde si punde mkewe Wanjiku anatokea akiwa ameshika gongo akitaka ammalizie Ndirangu.
wanjiku anahanikiza, “Rehe besha zakwa ngiri igiri na ihenya, yaani leta pesa yangu elfu mbili haraka.” msishangae kusikia elfu inaitwa ngiri. Anaendelea, “Ithe wa Katuru, nuuga rehe besha zakwa naihenya.”
Ndirangu kuona walume wenzie tupo akajitutumua na kusema, “Dhie wega naiwe. Mutumia mworu uyu-yaani nenda salama, mwanamke mbaya huyu.”
“Ati, kama unatusi mimi kwa vile iko mbele ya watu, ukija kwa nyumba napatiana adhabu kali saidi ya Hii. Hii mabo ya kuleta mudomo kwa bibi hapa jua italeta taabu mingi kwa wewe.” Alijibu Wanjiku kwa ukali huku akigeuza kurudi zake nyumbani tayari kumngojea mumewe ili akija ampatie discipline.
Akiwa anaondoka alisema, “Kwa vile hutaki kuleta besha yangu, ile nyama ya roho na mukimo amepika hukulangi leo (anamaanisha nayana ya moyo na ugali). Kama unaweza shukua ngwashee uchomege ukule hapo kwa kahawa.” (Ngwashee ni viazi).
Muiruri anamgeukia Ndirangu na kusema, “Jamba, mabo ya nyuba uwe unamaliza kwa nyuba siyo kuja hapa na kuleta matata.” Anatafuna miraa na kuendelea, “Wewe hapana kamata bibi sawa sawa hadi napata mudomo kukuja hapa na kuropoka bere ya wanaume.”
Izo kumba za moyo sizikwa
Nakoma mabvuto akulobeta mama ine moyo
Moyo wanga ni mabvuto ine moyo
Sunga wa busee
Ndinu oletwa ambuye
Oletwa ndinu
Usanga zose ndinu
Moyo moyooo
Naona bi mkubwa kaja acha nitimke kabla hajanitia discipline.
Chanzo: Tanzania Daima Machi 14, 2012.

Sunday 11 March 2012

Nilivyoshehekea Siku yangu ya kuzaliwa




Ingawa sikufanya sherehe kubwa zaidi ya kukusanyika na familia yangu, Siku ya kuzaliwa kwangu ilifana si haba.  Ilifanyika wapi?  Altona MB, Kanada.

Thursday 8 March 2012

Sisi ndiyo winter inaanza




Kwa tunaotokea Ikwete winter ya mwaka huu ilikuwa ni neema. Hatukuwa na theluji wala baridi ya kukata na shoka kama tulivyozoea. Wakati wenzetu wanangojea kufunga kipindi cha winter sisi ndiyo tumekianza. Je hii itaendelea au kuishia hapa. Who knows.

Tuesday 6 March 2012

Wade: Will He Make It?


Adoulaye Wade and Macky Sall Photo courtesy

Some people are lucky; others are not. Senegalese strong man, Abdulaye Wade is among the luckiest old men even though he behaves like an adolescent. Had it been not for divided and ever-greedy opposition, Wade would have been history now. Voters gave him a very heavy blow in the first round. He secured a leading of 34,8% ahead of his former protégé and PM, Macky Sall who garnered 26.5%. Other former PMs took third and fourth place: Moustapha Niasse with 13.2% and Idrissa Seck with 7.8%.

Such low votes speak volume and signify defeat. This translates into the fact that had the opposition backed one candidate, the results would have been Sall 47% and Wade 34.8%. Again, there wouldn't have been there any run-off that Wade can use to rig votes to fulfil his power-hunger to remain in power.

In other words, Senegalese were able to get rid of Wade in the first round had it not been for the opposition to help him secure a second chance of survival. Will Wade let it go easily without applying traditional African science of survival-rigging and cheating? Shall this happen, will the people and their weak opposition bite the bullet or give him a hard time once again?

One thing though is obvious that that Wade showed maturity for not rigging in the first round. Is it because of being cornered, his belief in democracy or the result of over confidence that he'd have won in the first round? If he allowed justice to take its course, will he keep this ma
turity or cascade back to his dreams of dying in power?

Although Abdulaye Wade, managed to tamper with the constitution to be able to run for a third time aimed at remaining in office, will he manage to manipulate the votes and get away with it. Results conclusively indicated he did not make it outrightly in the first round. This of course dented him badly. Sall gave him a spirited fight so as to change Wade’s tone from braggadacios to conciliatory one. Will this become Wade’s waterloo?

The ballot box can still boot Wade out if not to tame him. Senegalese should maintain the momentum they displayed in the first round whereby Wade lost outrightly. For those who remember his braggadacios that there won’t be any run-off, what happened is victory phase one. If voters fulfil their responsibility for the sake of their nation and democracy, Wade can still lose comfortably so as to be forced to lose in this-game-changer-like run-off.

Voters ought to deny Wade the votes he’s going to use to abuse them and their country. He’s been in power for twelve years. What can he do he did not do in these twelve years? Why should Senegalese voters prefer a centurion to a half ager Sall? If anything, Wade’s plight is squarely in the hands of voters who must punish him for ignoring them and abusing their office and constitution altogether.

Many people wonder where Wade got the guts and wits to tell former Libya strongman, Muamar Gaddafi and Ivorien one, Laurent Gbagbo to relinquish power last year while he cannot do the same now.

Due to the science of aging, we understand: Wade’s brain if wearing off. This contributes to the controversy he’s created apart from his greed to cling unto power. From what he does and says one can surely assert that this old man deserves to retire shall he deserve to be remembered honourably and favourably. Wade’s confusion can be noted in many things. He’s recently quoted saying,"I am president and father of the nation. This is what the Europeans do not understand," he told French weekly Sunday newspaper Le Journal du Dimanche. He added, “My majority is so overwhelming that I think I will be elected with a strong percentage in the first round,” Ask him where is hallucinatory majority went in the first round. He started changing the tone and tune altogether.

It is sad to note that Wade does not know that the father of Senegal is none other than Leopord Sedar Senghor. For Wade to equate himself with Senghor who became the first African leader to voluntarily retire when he was ten years younger than Wade connotes mischief to the nation and Africa in general. Senghor relinquished power in December 1980 retiring in favour of the Prime Minister, Abdou Diouf. After his retirement, Senghor did not involve himself in politics till his death on 20 December 2001.

As banned candidate, Youssou N'Dour put it, “The Senegalese are not stupid.” This will be justified by the votes they will cast in the favour of Sall. Shall Wade rig their votes; they still have the chance to prove that they are not stupid by seeing to it that he is not getting away with it.

Wade is an educated man by all standards. Again, as William Feather put it, “An education is not how much you have committed to memory or how much you know. It is being able to differentiate between what you do know and what you don’t know. It is finding out what you need to know and using the knowledge once you get it. I doubt if Wade knows where to go if he cannot willingly retire. I wonder if Wade knows where to go and get what he deserves-retirement instead of daydreaming going for a third time at such eleventh hour.

Wade, a cliffhanger, who promised crushing first round victory ended up saying this as the results were trickling in, "To all of my supporters, my allies, my sympathisers, I ask that you remain mobilised," Wade was quoted by BBC. He added "At this very hour... everything is still possible - victory or a run-off," Let Senegalese make it possible for Wade to pack and hit the road to oblivion.Will the opposition goof again to let Wade win?


Source: The African Executive Magazine March 6, 2012.

Mama Maria Nyerere anapofunda wasiofundika!

HIVI karibuni mke wa Baba wa Taifa, Maria Nyerere alikaririwa akitoa wosia ufuatao kwa wake wa viongozi. Alisema: “Unapokuwa mke wa kiongozi unapata changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kutoa dira kwa wengine...unapaswa kufikiri kwa niaba ya wengine, iwe ni kwenye ujasiriamali, elimu, afya au masuala ya kijamii hasa namna ya kukabili changamoto za kina mama na watoto.”

Haya maneno ni ya maana kwa wenye kutia akilini. Ni mazito yenye kueleza mengi katika uchache wake. Mama Maria anawataka wake wa viongozi wa sasa na hata waliopita watoe dira.

Hawa wana dira gani zaidi ya kuchuma na kujineemesha? Nani mara hii kasahau, mfano, fuko la Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) lililoishia kuwa mrija wa kutengenezea pesa kwa kisingizio cha kuwainua kina mama?

Nani amesahau Anna Mkapa alivyotokea kuwa milionea baada ya mumewe kuingia madarakani huku akitajwa karibu katika kashfa nyingi asijibu? Alishindwa hata kumshauri mumewe kutangaza mali wakati wa kuondoka.

Kwa kumbukumbu, zama za Mwalimu, jinsi Mama Maria ambavyo alifanya kazi kuu za kumtunza na kumshauri Baba wa Taifa, wanashangaa kuona wake za watawala waliofuatia kuwa marais nyuma ya pazia kwa kuanzisha NGOs zenye kutia kila aina ya shaka. Ukiacha mke wa Mzee Ali Hassan Mwinyi ambaye naye alishutumiwa kutumia ofisi ya mumewe kuwapatia mikopo ndugu zake, wake wa waliofuata wamekuwa kama wafanyabiashara wa kawaida ambao sijui kama wana dira hata mawazo ya kuwashauri waume zao.

Kama kuna ushauri mke wa Mkapa aliompa ni kujitwalia mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira ulioishia kuwa aibu ya mwaka kwa ukoo mzima wa Mkapa.

Nani mara hii kasahau kashfa ya Net Group Solution ambayo ilisemekana kuletwa na waliokuwa karibu na ukoo wa bwana mkubwa hasa bi mkubwa?

Ukija kwa mke wa Rais Jakaya Kikwete, Salma, sijui akama anamshauri vizuri mumewe kuhusiana na anavyopasa kutawala zaidi ya kutumia muda mwingi kwenye NGO yake ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) ambayo sawa na EOTF inalalamikiwa sana. Sina ugomvi na NGO hii zaidi ya kuona umma unavyoiangalia kwa jicho baya kutokana na namna inavyoendeshwa.

Swali kuu ni kwanini kuwa na NGO baada ya mume kuingia madarakani? Je, NGO hizi zinaweka wazi taarifa zake za ukaguzi wa mahesabu kila mwaka?

Mama Maria alikuwa na uwezo hata udhu wa kuanzisha NGO na ikawa ya kuwahudumia wanawake hata watoto kweli kuliko hizi za sasa ambazo ni shaka tupu. Lakini hakufanya hivyo kutokana na kuepuka mgongano wa maslahi na kujenga mazingira ya waovu kuweza kuitumia kuchafua uongozi wa mumewe.

Nani hajui kuwa ukichunguza wafadhili wengi wa NGO za wake wa wakubwa si watu wenye nia njema? Hili liko wazi hasa kutokana na ukweli kuwa baada ya waume za wenye NGO kuondoka madarakani, NGO zao hudoda kiasi cha kutovutia tena wafadhili. Je, hapa kinachofadhiliwa ni NGO au zinatumiwa kuwa karibu na jungu kuu kama ilivyo sasa?

Huwa nashangaa kusikia kwa mfano mke wa rais anakwenda kutafuta misaada kwa ajili ya wanawake na watoto wakati huo akishindwa kumshauri, kwa mfano, mumewe kuwashughulikia mafisadi, kupunguza ukubwa wa serikali, safari za nje zisizo na ulazima zaidi ya kuumiza uchumi na mambo mengine kama hayo.

Je, huyu asiyeona haya anaweza kuwa na uchungu na hao anaodai kuwa nao uchungu au kuwatumia kwa faida binafsi? Je, kazi ya wizara ya kina mama na watoto ifanye kazi gani kama kila mke wa rais anayeingia anataka kuwatumikia kina mama na watoto?

Basi tufute wizara, maana wizara ya kina mama na watoto ya First Lady ipo na inapokea misaada.

Kama kwelli hawa wanaochangia wana uchungu na kina mama na watoto kwanini wasichangie hiyo wizara husika ambayo ina waziri, naibu waziri, katibu wa wizara, wataalamu na wafanyakazi lukuki kikatiba? Jamani hapa nani anamdanganya nani na nani anamtumia nani?

Ukiondoa Tanzania, sikumbuki kwa mfano kusikia eti mke wa rais mstaafu wa Kenya Daniel arap Moi au wa sasa Mwai Kibaki kuwa na NGO.

Pamoja na ufisadi wake wa kunuka aliokuwa akifanya, hata Mobutu Sese Seko hakuruhusu mkewe kuwa na NGO.

Turudi kwa Mama Maria na kuwafunda wasiofundika wala kufundwa. Je, aliwaambia aliyowaambia kutokana na kuona hawafanyi hayo au kupwaya? Aliwashauri watoe dira baada ya kugundua kuwa hawana dira?

Je, aliwaambia changamoto kutokana na kugundua kuwa changamoto mojawapo iliyowakabili na kuwashinda ni kujitajirisha kutumia mgongo wa ikulu?

Yote yanawezekana. Je, hawa aliokuwa akiwafunda walikuwa na lolote la maana la kumuonyesha mama gwiji huyu au kujikomba tu?

Anasema: “Unapaswa kufikiri kwa niaba ya wengine, iwe ni kwenye ujasiriamali, elimu, afya au masuala ya kijamii, hasa namna ya kukabili changamoto za kina mama na watoto.”

Je, hawa walengwa wetu wanafikiri kwa niaba ya wengine au familia zao tu? Je, wanakabiliana na changamoto zinazowakabili kina mama na watoto au kuwatumia kuwatupia moja katika kila kumi waisakayo kwa kuwatumia hawa wanyonge na madaraka ya waume zao?

Leo utasikia kwa mfano mke wa rais amejenga shule kwao au mwingine kupeleka miradi kwao au kwa mumewe.

Kwanini asiachane na ubangaizaji akamshauri mumewe akawa na sera safi zenye kuwezesha kujenga hizo shule popote badala ya kwao au kwa kuuweka urais majaribuni kama ilivyo? mie naona ni bora ya Mama Maria ambaye hakuacha nyuma hata shule moja wala utajiri binafsi kuliko kuacha shule mia zitokanazo na kufanyia biashara Ikulu na cheo cha rais.

Sikumbuki kusikia tuhuma zozote dhidi ya Mama Maria, mumewe wala watoto wao. Je, hawa wa sasa hali ikoje?

Kila kona ni tuhuma na bahati mbaya hazikanushwi zaidi ya kutoa vitisho visivyo weza hata kutekelezwa. Hivi tuhuma za mtoto wa Kikwete, kujinufaisha kwa kutumia mgongo wa baba yake ziliishia wapi?

Kimsingi, ingawa mawazo ya Mama Maria ni lulu, ima amewafunda wasiofundika au ameamua kuwapasha kwa hekima. Yote yanawezekana.


Chanzo: Tanzania Daima Machi 6, 2012.

Nakwenda kwa mama kutuliza hangovers

BAADA ya kupona kufa kutokana na migomo ya matabibu, Dk. Mpayukaji Nkwazi Nkuzi Mhango Msemahovyo, na marafiki zake kina Mgosi Machungi, Mzee Maneno, Mchunguliaji na wengine wapatao 50 wamepata ofa ya kwenda kwa Mama kutumia na kupunguza hangovers za kahawa na kinywaji.

Wakati tukipanda pipa na kujitoma zetu kwa mama, wanywa kahawa wengi walikuwa wakilalamika kuwa tumechukua njuluku za kijiwe kwenda kutanua.

Hakuna kilichowakera wanywa kahawa kama mimi kuwa naandamana na marafiki zangu na mke wangu karibu kila mahali. Hakuna kilichonikera kama kusikia upuuzi huu wakati pesa tunayotanulia si yao bali wafadhili wetu ambao leo sitawataja.

Kwanini nisiende kwa mama baada ya kumaliza mgomo wa wachemsha kahawa waliokuwa wakitaka kuongezewa marupurupu hasa kashata na maadazi kutokana na kazi yao ya kuhakikisha uhai wa wanywa kahawa haudhuriwi na uchafu hata polonium kama ile ya daktari Mwakiwembe?

Kabla ya kuendelea, wajua kuwa kijiweni kwetu umetokea mchezo mbaya wa kurogana na kulishana hata kupakana sumu? Juzi Msomi Mkatatamaa alikuwa akilalamika kuwa anahisi amegusishwa Polonium kiasi cha kuanza kuwashwa washwa sehemu za nonihino.

Kwa vile kumalizana imeanza kuwa fasheni kwenye kutafuta ulaji, wanywa kahawa wengi walitaka nitoe maelezo.

Nami kuona zali hili ni kubwa kuliko ubongo wangu wa P’eege nimeamua kwenda kwa mother kutuliza akili ili mambo yapoe kama alivyowahi kusema Willy Mkama kuwa Waingereza wakiona mambo yamepamba moto huunda Royal Commission kuwazuga wajinga kuwa wanachunguza ili mambo yapoe na yakipoa wanaendelea kuhomoa kama ilivyo kwa Bongolalaland ya Danganyika ambapo mafisi na mafisadi hushika kani huku walala njaa wakiendelea kutolewa njuluku na kusota.

Hebu turejee kwenye malalamiko ya wanywa kahawa. You know what. Hawa jamaa wanaungua ugonjwa uitwao Ammaglobulimenia yaani kuwa na mfumo uliovurugika mwilini.

Matokeo yake ni kuugua ugonjwa wa Bulimia unaoandamana na mwingine uitwao Megalomania. Watu wanaougua ugonjwa huu huwa wanajifanya hamnazo. Hata uwambie nini huwa hawashughuliki na kujibu wala kutoa maelezo. Kwa mfano, mgonjwa wa Bulimia ukimwambia kuwa anachofanya ni kibaya hufanya zaidi.

Huwezi kuamini eti wanasema nami naugua Bulimia kwa vile wakiniambia niache matanuzi mimi na marafiki zangu natanua zaidi. These guys are super stupid so to speak. How can a big guy with all ulaji under my control be that silly? Hooey! Samahani nimechonga umombo kwa sana kama maandalizi ya kwenda kuchonga na kwini.

Pia nachonga umombo kuwaonyesha wanaoshuku udaktari wangu wa kupewa kuwa nimebukua hata kama sikupata honours. Hayo tuyaache.

Wanywa kahawa kwa umbea sina hamu. Yaani mie kuandamana na maswahiba zangu 50 imekuwa stori. Je, wanataka niende na wangapi? Mwakani nitakwenda na 800 kama alivyokuwa akifanya shujaa wangu Mobutu Sese Seko Mwizi wa Zabanga kule DRC.

Hawa jamaa hawajui kuwa waliponichagua kuwa mkuu wao hawakujua kuwa sikugombea kuwaendeleza bali kujiendeleza mimi na nyumba yangu.

Hawajui kuwa nilipowaahidi maisha ya kuukata nilimaanisha yangu marafiki zangu na nyumba yangu? Kalagabaho na shauri yao! Imeandikwa kuwa mchungaji atakunywa maziwa ya kondoo awachungao. Kosa langu nini kula pesa ya nyinyi niwachungao? Pia imeandikwa kuwa ya Kaisari muachie Kaisari.

Kwanini wanywa kahawa hawataki kuniachia yangu kuwa yangu? Niliwahi kuuliza swali hili Msomi Mkatataama aakijibu kuwa wanachotaka si ya Kaisari maana kahawa si mali ya Kaisari yaani mimi bali wao. Jamaa mshenzi!

Ana maana kuwa hata walipa kodi wana haki ya kujua kodi yao inatumikaje kwa vile ni yao na si ya mkuu siyo? Wee koma. Sasa unaanza kugusa pabaya! Kama mkuu anawala waliwa wewe yakuhusu nini iwapo nawe unawala wanywa kahawa? Wajinga ndio wafanywao punda.

Sijui niwambie nini hadi waelewe. Huwa nakwenda nje mara kwa mara kubomu ili maisha yasonge mbele. Wengine husema eti nakwenda kufanya biashara na kukagua akaunti zangu huko. Well, hata kama ni hivyo, kwani nimewazuia wao kwenda? Sasa nasema wazi wazi.

Huwa napenda kwenda ughaibuni kutafuta wawekezaji wa kuja kuchukua sorry kuwekeza kwenye kijiwe. Bila mimi kwenda kule wawekezaji watagoma. Mbona watu wanasahau mapema! Bila ya yule jamaa yangu Ni Ziro Kamalagi kwenda kusaini mkataba wa Buzwagiii kule London tungekuwa na wawekezaji kweli? Au wanatumia akili mbovu ya Mzito Kabwela anayetaka kaya iache kuwalipa washikaji wa wakubwa waitwao AIPITIELO matrilioni eti wawekeze kwenye gesi.

Huyu kijana hana adabu. Anataka wazito wale polisi? Inaonyesha hata kwenye kijiwe kuna watu wa Mzito Kabwela. Maana nakumbuka alikuwa akipita kupata kikombe cha kahawa. Huenda aliacha magugu nyuma alipopita. Namshauri akatapeliwe kule Loliyondo kwa kupewa kikombe kichafu cha kutibu ujinga cha mchungaji Ashomile Mwatapeli.

Nasikia jamaa huyu kanogewa na kutangaza miujiza mingine ya kuwatapeli wajinga ndio waliwao waliojazana Bongolalaland ya Danganyika. Kwanini hawatumii vichwa wanatumia masaburi?

Nikifika London lazima nikajinome kwenye mitaa ya Trafagar, nitabembea na bi mkubwa pale Brent Park (Siyo Jomeika ambako iliniwia soo), Hounslow, Richmond, Kingston upon Thames, Buckingham, Gunnesbury, Isle of Dogs na kwingine. Wajua nimekulia London?

Ukiachia upuuzi wa malalamiko ya wanywa kahawa, hawajui kuwa mie huwa sipendi kukaa sana kijiweni. Huwa naboreka kukaa kijiweni nikisikiliza malalamiko mbali mbali ya wanywa kahawa.

Ili kuepuka kuusonesha moyo wangu kwa kuletewa habari mbaya kila siku, huwa napenda kwenda nje kutumia. Hivi utajisikiaje iwapo kila siku utaletewa mashitaka yanayowahusu watu wako hasa mke, watoto na marafiki kuwa wanatumia ukuu wako kujineemesha kwa kukiibia kijiwe? Wanataka nikae kijiweni waje siku moja wanilazimishe kuamrisha watu wangu waaibishwe na mgambo wa city kwa kutumia ulaji wangu kujineemesha?

Hata hivyo kuna kosa gani kwa mke wa mkuu wa kijiwe kuwa mkuu wa wanawake wote au mtoto wa mkuu wa kijiwe kuwa mkuu wa vijana wote?

Naota nakuwa kwini siyo! Pesa ya safari hii imetolewa na kwini. Ila usimwambie mtu.

Chanzo: Tanzania Daima Machi 6, 2012.

Monday 5 March 2012

Tanzania itakuwa shamba la bibi hadi lini?

Hivi karibuni gazeti moja la kila siku wiki liliripoti kuwa kigogo mmoja wa dini mkoa mmoja kanda ya ziwa angefikishwa mahakamani kwa kosa la kuhujumu uchumi.

Kosa lake ni kwamba alikuwa akitumia dini yake kupata misamaha ya kodi ilhali alichokuwa akifanya hasa kwenye kununua saruji ni kuwasaidi wafanya biashara kukwepa kodi ya mamilioni kila mwezi. je huyu kweli ana dini au ni kafiri wa kawaida? Je ni wangapi wanatumia taasisi zao za kidini zilizochipuka kama uyoga kujitajirisha? Je hiki ndicho chanzo cha utajiri wa ghafla wa viongozi wengi wa madhehebu ya dini?

Nimekuwa nikilalamikia uholela na urahisi wa kusajili madhehebu ya kidini bila kusikilizwa. Nadhani Kwa tukio hili angalau tunaoshuku biashara hii ima ya misamaha hata unga ukiachia mbali kuiba sadaka na kutapeli wananchi tutaanza kusikilizwa kwa makini kama hakuna mkono wa serikali kwenye ushirika huu mtakakitu.

Pia kuna uwezekano kuna maafisa wa serikali wanaojua mchezo huu. Lakini kwa vile wananufaika nao hawataki hata kuishauri serikali kuweka vigezo vigumu kusajili madhehebu ya kidini ambayo siku hizi yamegeuka kama maduka ya kawaida.

Nchi yetu ina utaratibu wa hovyo kwenye mambo mengi kuliko nchi zote za Afrika Mashariki. Shilingi yetu iko chini kuliko sarafu zote kwenye eneo hili. Tunazidiwa na hata na Burundi na DRC pamoja na kukumbwa na misukosuko miaka nenda rudi! Angalia tulivyo na maduka mengi ya madawa tena mengi yakiuza madawa feki na yaliyo expire utadhani nchi yetu ni ya wagonjwa wa akili?

Tazama maduka ya mikorogo yalivyotapakaa huku tukiendelea kuhatarisha afya za watu wetu hasa akina mama. Tazama tulivyowekeza kweney glosari kuliko hata shule. Niliwahi kuliongelea hili kwa kulinganisha na Uganda ambako kuna shule nyingi wakati sisi tuna glosari na guest house za chap chap nyingi. Hili ni tatizo hata tunapodanganywa tuugane na nchi nyingine za Afrika mashariki ambazo hazina raslimali nyingi kama zetu na ardhi. Tatizo jingine ni kwamba hatuna hata mipango mizuri. Bado tunafanya unafiki wa kutangaza matangazo ya kuchochea ngono kwa kisingizio cha kupambana na ukimwi.

Turejee kwenye kuhujumu uchumi kwa kutumia majoho ya dini. Kwanini serikali haitaki kujiuliza ni kwanini madhehebu ya dini yameongezeka huku wanaojipachia uchungaji, ushehe, uaskofu, utume-bado upapa-ni wengi na hawafanyi kazi yoyote zaidi ya kuhuburi lakini bado ni matajiri wa kutupwa? Wasitudanganye kuwa pesa inapatikana toka kwa waumini maskini wanaolalamika kila siku. Lazima kuna njia nyingine nyuma ya pazia na huu ndio motisha wa kila mtu kupenda kufungua makanisa na misikiti. Imefikia mahali hata wageni wanakuja kufungua makanisa Tanzania kwa vile hakuna sheria ya kuwazuia wala kuwachunguza.

Mbona Yesu alipiga marufuku watu kukalia kupiga kelele badala ya kufanya kazi maana binadamu hawezi kuishi kwa neno pekee? Kwa kutilia mkazo mtume Paulo alisema asiyefanya kazi na asile. Ajabu hawa wetu wanakula hata kuwa matajiri bila kulazimishwa na sheria kutoa maelezo walivyopata utajiri wao! Mbona Sayyidina Omar bin Affan aliwazuia waislamu kupoteza muda mwingi kwenye ibada bila kufanya kazi miaka zaidi ya 1,000?

Tunao wezi wengi wanaowaibia watu wetu na kuwahadaa. Kwanini mhasibu au mfanya kazi wa serikali anapoiba ofisini kwake linakuwa kosa la jinai lakini kiongozi wa dini akiliibia kanisa au dhehebu lake haliwi kosa la jinai? Mwizi ni mwizi hata awe askofu au shehe au rais. Kinachokera ni pale serikali inapozidi kuwapumbaza watanzania kuwa ni nchi ya amani wakati ni nchi ya kuibiana. Hivi haya maelfu ya wetu wanaotapeliwa na majizi haya na kutumia nafasi zao kukwepa kodi yanaashiria amani?

Tusipofumbuka macho tutajikuta tuna makampuni yanayoonyesha kunawiri kuliko mengine si kwa sababu ya umahiri katika kufanya biashara bali umahiri katika kukwepa kodi. Kwanini taifa letu hasa viongozi wetu ni wagumu kujifunza? Wawekezaji wengi wamekuja wameiba na kuondoka huku tukizidi kukaribisha wengine kuja kuiba. Wako wapi wahindi waliokuwa ‘wamewekeza’ kwenye shirika la reli? Wako wapi majambazi wa Dowans walioendelea kutuzidi akili kwa kubadilisha majina ya biashara zao? Nenda kwenye mahoteli yetu mashuhuri. Kila baada ya miaka mitano yanabadilishwa majina ili kupewa muda mwingine wa kutuumiza. Angalia makampuni ya simu yanavyobadilisha majina mara leo so tell kesho mot el tel tel tel tel mpaka lini? kwanini msiseme ni stealtel?

Bado makampuni hayo hayo ya simu yanayolangua watu wetu ukiachia mbali kuwalisha huduma mbovu kuliko nchi nyingine za kiafrika. Imefikia mahali watu walioko nje kupiga simu kupitia nchi jirani kuepuka kulanguliwa. Hebu tutoe mfano mdogo. Ukipiga simu toka Kanada kuja Tanzania kwa Tanzania unachajiwa senti 25 za dola ya Kanada wakati Kenya wanakutoza senti 5. Hii maana yake ni kwamba kupiga simu Tanzania ni aghali mara tano kuliko Kenya. Je ni kwanini hali inakuwa hivi kana kwamba hakuna serikali? Hata ukipitishia Uganda hata Burundi bado ni nafuu kuliko kupiga moja kwa moja Tanzania. Hapa bado hujapambana na upuuzi kuwa namba unayopiga haipo mara huna salio la kutosha na ushenzi mwingine mwingi? Je huu ndiyo uwekezaji au uchukuaji? shame on you all!

Nikijumlisha yote hayo hapa juu huwa mara nyingi nafikia hitimisho kuwa nchi yetu imo mikononi mwa ima mataahira au watu wasiojua wanachofanya na kama wanajua basi watu wasiopenda nchi yetu. Imo mikononi mwa watu hatari ambao huko tuendako watasababisha vurugu na balaa kwa taifa. Maana hakuna kisicho kuwa na mwisho. Watu wetu hawawezi kuendelea kugeuzwa mbuzi wa shughuli au bidhaa kwa ajili ya wezi wachache kujitajirisha

Chanzo:Dira Machi, 2012