Wednesday, 6 May 2015

Hii Kiboko yao

5 comments:

Anonymous said...

Salamu Mwalimu Mhango,
Mwalimu Nyerere alipochukua nchi na kuitaka nchi yetu changa kuiweka katika ramani ya nchi changa ambazo zinazoendele akiweka mihimili yote ya siasa ya Ujamaa na kujitegeme pamoja na nguvu za kibepari,kibeberu na wapinga maendeleo duniani ambao walitaka Tanzania isifike pale inapotakiwa ifike.Mwalimu,aliaweka msingi wa kuwahudumia wananchi wake kwa utaratibu wa elimu,bure matibabu bure na ardhi ni ya wananchi(serikali) alijuwa wazi kwamba ktika upande wa elimu atakabiliwa na nguvu ya vijana wengi sana watakaomaliza darasa la saba,vijana ambao ni lazima wawe na nafasi yao ya kuchngia taifa lao katika uzalishaji.Kwa hiyo pamoja na kulenga kuweka viwanda nchini kama sehemu ya taifa lijitegemee lenyewe lakini aliwaweka vijana hawa akili na kuwatilia maanani maan bia ya kuweka viwanda nchini vijana hawa watakuwa ni mzigo mkubwa sana kwa nchi na jamii kam ilivyokuwa hivi sasa.

kwa hiyo alianzisha viwanda ambavyo vilitoa ajira ya uhakika kwa jeshi hili la darasa la saba.Nitaviorodhesha hapa viwanda ambavyo ninavyovikumbuka na hata vile nisivyovikumbuka kwa majina naweza kuashiria tu vilikuwa vinazalisha nini,
Viwanda vya utengenezaji nguo:
1-Urafiki-Dar.
2-Sungura -Dar.
3-Mwatex - Dar
4-Mwatex-Mwanza.
5-TANITA (kiwanda cha kuchambua korosho) Dar.
6-UFI, (kiwanda cha vifaa vya ukulima)Dar.(uvuvi)Dar.
7-MNC (cha kukobo;ea nafaka)Dar.
8-Bora Shoes-(viatu )Dar
9-Moro Shoes (viatu)Morogoro.
10-Kiwanda cha Tumbaku,Morogoro.
11_Kiwanda cha Sukari,Morogoro.
12-Kiwanda cha Mafuta-Mwanza.
13-Kiwanda cha viwembe (Perma Sharp) Dar.
14-KIBO (vibiriti vya njiti na vijiti vya meno)Arusha
15-Kiwanda cha mbolea,Tanga.
16-Kiwanda cha chuma,Tanga
17-Kiwanda cha Saruji,Tanga.
18-Kiwanda cha saruji .Dar.
19-Kiwanda cha saruji,Mbeya.
20-Kiwanda cha sigara (TTC)Dar.
21-kiwanda cha kutengeneza mabati ya ujenzi na vyombo vya nyumbani(aluminium)Dar.
Mwalimu hivi ndivyo viwanda ambavyo ninavyovikumbuka mimi na ambavyo ilikuwa ni fahari ya nchi yetu na kutuwezesha kusimama kwa miguu yetu kwa kukidhi mahitaji yetu na hata kufanya biashara za nje kwa bidhaa zetu wenyewe.Leo viwanda hivyo vimebaki ni historia ya kuhuzunisha na matokeo yake ndiyo haya sasa tunayoyaona kwamba kila kitu anachokihitaji mwananchi wa tanzania ni lazima kitoke nje na tunakuwa na kuona fahari kwamba ni cha nje hata kama kinatoka china,kenya na Afrika ya Kusini.

Na kwa nguvu za mabepari wa nje na wa nadani wakishirikiana na vibaraka vyao ambao baadhi yao ambao tumewapa madaraka ya kutuongoza ndio watazidi tu wanatukandamiza wananchi na kuikandamiza nchi yetu ili tutegemea kila kitu kutoka nje na huku wakituibia rasilimali zetu lukuki.

NN Mhango said...

Anon umenipa elimu kubwa. Kwanza naomba nichote hii orodha ya viwanda ili niitumie kwenye mswada wangu kuhusu kuunganisha Afrika. Uliyosema itakuwa ni kuyaharibu kama nitaongezea zaidi ya kusema kuwa ukikumbuka visheni ya Nyerere kwa taifa na waafrika unatamani ulie hasa ikizingatiwa kuwa wale waliomkwamisha na kumsaliti ni watoto wa maskini aliwawezesha kupata elimu ambayo, hata hivyo, haikuwa na faida kwa taifa. Nyerere ni sawa na simba aliyezaa mbwa au mtakatifu aliyezaa shetani kama si msomi aliyezaa wapumbavu. Hata hivyo, halikuwa kosa lake. Sitaki niharibu mchango wako adhimu na adimu.

Anonymous said...

Mwalimu Mhango,
Umeniacha hoi na hii analogue yako kuhusu Mwalimu Nyerere.Ni ukweli mtupu na ni ukweli mchungu,wakati mwingine mpaka unafikia kuelewa au kuamini kwamba Nyerere alizaliwa sehemu sio sahihi japo alikuja kwa wakati ulio sahihi,kwani bila ya mchango wake mkubwa wa kihistoria, historia ya ukombozi wa Bara la Afrika labda ingeandikwa kwa namna nyingine.Mchango ni mkubwa mno sana hata naweza kudai kwamba bila ya yeye viaongozi kama akina Nelson Mandela wasingefika pale walipofikia.
Mwalimu Mhango,kuna swali linanyima raha kila ninapojiuliza hadi hii leo nakosa jibu,nalo ni hili kwa nini Tanzania(serikali)inashindwa kujenga au kumjengea Mwalimu Nyerere sanamu katika mikoa mbali mbali ya Tanganyika?Je kuna siri gani hapa?Mababa wa taifa duniani kote hujengewa sanamu zao ili iwe kumbukumbu kwa kizazi kijacho na hata kwa wageni wanapotembelea nchi.Katika nchi kama ya kwetu ambako siku zijazo utamaduni wa kujisomea utatoweka itatosha tu watoto kuwauliza wazazi wao kwamba je sanamu hili ni la nani?Kwa kujibiwa kwa mtoto kwamba sanamu ni la nani amekuwa tayari amepata elimu ya kuweza kumsaidia kumfuatilizia baba huyo wa wataifa.

Namalizia kwa kulirudia swali,Je kuna siri gani ya kutojengewa Baba wa taifa Mwalimu Nyerere sanamu lake hadi hii leo katika mikoa mbali mbali ya Tanganyika?

Anonymous said...

Mwalimu Mhango mfikishie ujumbe Kipanya nanyongeza hapa kidogo na matibabu ya magonjwa pia yanayfanyika ng'ambo ughaibuni kwa viongozi wetu na baadhia ya wale wanaoweza kwenda India!

NN Mhango said...

Anon, hawawezi kumjengea ukumbusho kwa vile wanataka asahaulike. Wanamchukia sana kwa sababu kuu kadhaa. Mosi, jinsi watanzania waliokata tamaa wanayomkumbuka na kumtaja. Pili matamko yake yanaporejewa kila sehemu kwenye uchambuzi hata mikutano ya kisiasa kwa baadhi ya vyama vya upinzani.. Tatu wivu na uvivu wa kufikiri. Maana wao wangetaka wawe ndiyo maarufu kuliko wote. Mwisho ni roho na nafsi zao kuwasuta. Hukumbuki hata maadhimisho ya siku ya kifo chake yamegeuka jinamizi kwao kiasi cha kuyaogopa na kuyakwepa?