Sunday, 8 November 2015

Habith Salva Rweyemamu ang'atuka ikulu
Taarifa zilizotufikia ni kwamba yule mwandishi kidhabu na mchumitumbo Salva Rweyemamu hatimaye ameondolewa ikulu na utawala mpya wa awamu ya tano. Kwa tunaomjua kwa kufanya naye kazi kwa karibu, tunamjua kama alama ya uoza wa serikali ya hovyo na fisadi iliyomaliza muda wake. Rweyemamu na waandishi wenzake wengine nyemelezi walitumiwa na Jakaya Kikwete kuosha nepi zake na kuweza kuwazuga watanzania na kumchagua rais wao jambo ambalo watalijuita milele. Kidhabi na habithi inasemekana haziivi na Dk Kanywaji Makufuli. Kwa tunaomjua, ni mtu wa hovyo mnafiki na hasidi ambaye kuwa kwake ikulu ni machukizo kwa Mungu na watanzania. Hayawi hayawi. Tunangoja na wengine wote waliopewa vyeo kwa kulipana fadhila kuanzia za ngono hadi kufua nepi watimliwe mara moja ili kurejesha heshima ya ofisi za umma. Hongera Magufuli kuanza kuonyesha ndia. Nenda mwanakwenda Salva. Nenda katokomee kusikojulikana. Nenda utuondelee mbu kiza na aibu.Nenda mwanakwenda na ukatokomee. Nenda usiangalie nyuma. Nenda kama kibwengo na moto wake kichwani. Nenda mwanakwenda usigeuke nyuma. Nenda ukaishie uishiako. Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA

No comments: