Kudos to President Magufuli

Tuesday, 1 March 2016

AFRICA REUNITE or PERISH chaanza kufundishwa chuoni

titletitle

Nimepata habari njema kuhusiana na vitabu vyangu hasa AFRICAN REUNITE or PERISH kuagizwa na chuo kikuu cha The Great Zimbabwe University kuanza kutumika kufundishia. Sambamba na ARP vitabu vya Born with Voice na Souls on Sales navyo vimeagizwa. Kama haitoshi, nimekaribishwa kwenda kufundisha African Studies kwenye chuo husika. Hakika ni mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi. Kwa sasa nangojea kitabu kingine cha The Best and Worst African Managers wakati nikimalizia kingine cha Need to Decolonise Education.
  • Soul On Sale

2 comments:

Anonymous said...

Mwalimu Mhango,
Ningependa kuchukua nafasi hii kwa kukupongeza na kukupa hongera kwa kuanza kuyavuna matunda haya ya awali ya kazi zako ukiwa wewe mwenyewe unashuhudia katika uhai wako.Naam,mimi ni katika wale ambao nilikua naamini kwwmba kazi zako hizi zitafaidisha kizazi kijacho zaidi kuliko kizazi hiki tulichokuwa sisi,hususa kwa vijana wa kiafrika ambao hawakujengewa utamaduni wa kujisomea ukiongezea na kupigwa na wimbi la short cut la social media ambalo linawafanya na kuona kujisomea ni kazi nzito.Naam,umelima shamba umepanda mbegu na mbegu zimeshaanza kuchipua na kumea iliyobaki ni kazi ya vijana kulilinda shamba hilo na kufaidika na matunda yake.Mwalimu Mhango kazi uifanayo ni kubwa hususa katika kupambana na ukoloni,ukoloni mambo leo na kuwaumbua daima viongozi wetu ambao wanaotetea masilahi yao na masilahi ya mabwana zao.
Pia ningependa kuipa pongezi familia yako kwa kutoa sapoti yao kubwa kwako kwa kukuwepesishia utekelezaji wa kazi zako, pia nawapa pongezi wale wote ambao wanasimama na wewe bega kwa bega kwa kuchangia mawazo yao na feedback zao kwako.Najua wazi kwamba safari ni ndefu lakini kila safari uanza kwa hatua moja njiani nawe hatua hiyo umeshaianza Menyezi Mungu azidi kukutilia wepesi na kukupa afya njema na uhai bora

NN Mhango said...

Anon,
Shukrani kwa pongezi na dua zako. Useamayo ni kweli. Kwani kazi za kisomi huchukua muda mrefu kukubalika na kutumika. Kimsingi, moja ya kazi yangu ilionekana kuchomoza hata kabla ya kuchapishwa haswa kitabu cha AFRICA REUNITE or PERISH. Profesa aliyekipitia alikipenda sana kiasi cha kuniarika tuandike kingine pamoja ambacho nimeishakabidhi upande wangu. Ni kweli. Vijana wetu -na si vijana tu bali watu wetu -hawasomi kiasi cha kupitwa na mengi. Hata hivyo, unategemea nini kama wanazaliwa na kutawaliwa na watawala wavivu wa kufikiri nikiazima maneno ya mvivu mmoja Mkapa wala hawaandiki? Sisi tuliosoma wakati wa mwl Nyerere tulionea fahari kusoma na kuandika. Sijui kama wanafunzi wa sasa wanaweza kwenda kutembea kwa jamaa zao wakaiba vitabu na majarida hasa Africa Now kama nilivyokuwa nikifanya na kuacha fedha.
Nashangaa kwa mfano hapa Kanada kuona vibabu vikipigana vikumbo maktaba ukiachia mbali watoto wa darasa la kwanza kushindanishwa kusoma vitabu vingi na kupewa zawadi. Binti yangu wa darasa la sita anasoma mitabu ya kurasa 500 kwenda juu hadi tungombana naye.
Nimalizie tena kwa kukushukuru kwa kunipa motisha na changamoto.
Asante sana ndugu yangu.