Saturday, 5 March 2016

Kwa wanandoa au watarajiwa


Hapa Agatha Murudzwa anawanasihi wanandoa kupendana huku akiwapongeza wawili waliofunga pingu za maisha kwa lugha yake ya Kishona.


Hongereni
Mungu awe nanyi
Mungu awalinde
umepata mume
mapenzi umpe
Hongereni
umpe upendo
Auone na kuuhisi

Wawili nyinyi
Mmetukusanya hapa
Mmesimama mbele ya Mungu
Hiki kinachofanyika
Ni mbele ya Mungu
Mungu awaunganishe
Mtangulizeni Mungu
Hongereni
Mungu awe nanyi
Mungu awalinde

Nawe baba ni mlinzi
Mtunze umpe upendo
Mpe upendo wa mume
Hongereni
Mungu awe nanyi
Mungu awalinde


ONYO
Ukisikia mukadzi usiseme ni Nkwazi
Hata ukisikia Ngwazi usidhani ni Nkwazi
Mukadzi ni mwanamke na Ngwazi ni mtemi wa watemi au simba

No comments: