Wednesday, 9 March 2016

Haya ni maombi au utapeli na ubangaizaji


Baada ya rais John Magufuli kustukia gea ya baadhi ya viongozi wa kiroho wenye uroho na hamu ya kuwa karibu na ulaji, amesusa kuhudhuria upuuzi unaoitwa kumuombea. Kwani hamuwezi kumuombea majumbani au kwenye nyumba zenu za ibada hadi iwe matangazo? Acheni njaa. Eti wanaiombea nchi! Kama si njaa na utapeli mlikuwa wapi wakati inageuzwa shamba la bibi? Naona aina fulani ya ushirikina licha ya uganganjaa na utapeli wa kutumia jina la Mungu.

No comments: