Thursday, 13 July 2017

Kati ya wapinzani na Mkapa nani mpumbavu?

Image result for photos of mkapa and magufuli

Rais anayetuhumiwa kuiuza na kuihujumu Tanzania Benjamin Mkapa amerejea kwenye ulingo wa siasa kwa tabia ile ile ya kizamani. Akijikomba kwa rais John Magufuli mkoani Geita aliwaita wanaompinga Magufuli kuwa wapumbavu. Wengi wanadhani Mkapa hakusema hayo kwa kupenda bali kulazimika hasa ikizingatiwa alivyoondoka na kashfa lukuki hasa wakati huu wa utumbuaji majipu. Ukiangalia historia ya wizi wa kijinga na kipumbavu vilivyofanyika chini ya Mkapa unashangaa anapopata jeuri kiumbe huyu. Hivi Mkapa amesahau kuwa watanzania wanajua alivyojitwalila Machimbo ya Makaa ya Mawe ya Kiwira? Je Mkapa amesahau kuwa watanzania wanakumbuka alivyotumiwa na mke wake na mashemeji zake kuiua na kuiuza NBC? Je Mkapa amesahau kuwa watanzania wanakumbuka makampuni yake ya ANBEN, Tanpower, Fosnik na mengine? Je hapa upumbavu wa watanzania uko wapi au ni ile hali ya kuwaibia wakaendelea kunyamaza? Je kati watanzania na Mkapa mpumbavu ni yupi? Je Mkapa atafanikiwa kuendelea kuwatukana wananchi ili kumfurahisha Magufuli asimtumbue au wananchi wataliamsha dude na kutaka ashughulikiwe sawa na mafisadi wengine alioshirikaina nao kuuza taifa?

No comments: