Tuesday, 18 July 2017

Leo Tumetimiza miaka 19 ya NdoaKwa ndugu jamaa na marafiki, leo mimi na mke wangu Nesaa tumetimiza miaka 19 tangu tufunge ndoa. Katika kusherehekea siku hii  muhimu kwetu, pia huwa tunakumbuka kuwa ni siku ya kuzaliwa kwa shujaa wetu Nelson Mandela-ambaye kama angekuwa hai leo-angetimiza miaka 99. Tumefurahia keki na kadi tulizonunuliwa na watoto wetu kila mmoja akieleza anavyojihisi kuwa wazazi wake ukiachia mbali Nkwazi Jr na Nkuzi ambao hawajui kuandika. Kwetu ndoa si ndoana bali shule na pepo. Tunazidi kumshukuru na kumuomba Mungu aendelee kutupa na kutujalia amani upendo na utulivu tangu mwanzo wa safari yetu. Tunazidi kushukuru kuwa upendo wa kweli na wa ari si kiungo ambacho kiliwahi kupungua au kukosekana tangu mwanzo wa safari yetu. Si hayo tu, tunamshukuru Mungu kwa kutujalia wana na mabinti si haba ukiachia mbali furaha na kufaana visivyo vya kawaida. 


2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ama kweli mnastahili pongezi HONGERENI SANA. Maana ni kweli maisha ya ndoa ni kuvumiliana pia kusikilizanakwa dhati. Ila sasa kaka umechelewa kwa mwaliko:) Haya nawatakieni hii siku iwe ya AMANI NA FURAHA

NN Mhango said...

Da Yasinta tunakushukuru kwa salamu zako. Hata hivyo, hukuchelewa. Kwani hatukukaribisha mtu yeyote hasa ikizingatiwa kuwa hili ni suala binafsi. Nawe kadhalika, tunawatakieni kila la heri, upendo na mafanikio katika ndoa yenu.