Sunday, 23 July 2017

Wiki hii namkumbuka shujaa wangu Mahlathini

Sinon "Mahlathini" Nkabinde wiki hii anatimiza miaka 18 tangu atutokea kiroho ingawa kimwili daima atakuwa nasi kama si kupitia kwenye imani basi kwenye kazi yake. Tokana na kuwa mpenzi na shabiki mkubwa wa Mahlathini na Mahotela Queens huwa kila mwaka naadhimisha maisha ya nguli huyu wa muziki aliyetikisa anga la muziki hasa kwenye zama za ukaburu kiasi cha kuwa sehemu mojawapo ya ukombozi wa Afrika Kusini. Ni bahati mbaya kuwa ni mwezi huu wa Julai ambapo nguli mwingine David Masondo wa Soul Brothers alifariki ghafla miaka miwili iliyopita.

No comments: