Saturday, 13 November 2010

Hongera maalim Seif na Lipumba kurejea CCM
Wengi wanajiuliza kama siyo kushuku. Je usuhuba na ushirika wa mwenyekiti wa CUF na katibu wake na CCM una tija kwa taifa kwa namna yoyote?. Je usuhuba huu utadumu? Je ushirika huu utaikuza au kuiua demokrasia nchini? Je kupewa kipande cha utawala visiwani kutalinufaisha taifa au kuliweka msambweni? Je CUF kama TLP ndiyo imerejeshwa CCM?

Kwanini serikali ya umoja wa kitaifa upande mmoja na si nchi nzima? Je ushikaji huu ni kwa maslahi binafsi au ya wanachama? Maswali ni mengi kuliko majibu.

5 comments:

Anonymous said...

Ni maswali mazuri ya kujiuliza mpayukaji, maana hata mie sielewi maana ya kuwa na makamu wa uraisi wawili! Aise Hebu fikiria yale madelegation yao kila wakisafiri, kama leo nimeona ITV Tanzania, Maalimu akiwa Buguruni, akiambatana na msururu wa mashangingi, wana usalama, polisi na wapambe! Hii nchi yetu, siasa kwa vyama vya upinzani ni kupigania ulaji wao tu na sio haki na huduma kwa mlalahoi.
Na ni mpaka hapo tutakapobadilisha haya mawazo yetu ndio ndipo tutakaposonga mbele kiamendeleo.
Maalimu kawauza wapemba na wanaunguja wachache kwa ajili ya cheo na ulaji tu!

Anonymous said...

Bila kupindisha huu ni usaliti usio na kifani. Maskini wanachama wa CUF wametumiwa hadi kuuawa kumbe ni mapambano kwa ajili ya mlo wa fisi wachache!

Ng'wanaMwamapalala said...

Ikumbukwe kuwa wakina Mandela Afrika ni wachache kama hawapo kabisa kwa sasa.
Maalim pia ameutekeleza ule msemo wa kiingeleza usemao. If you can't beat them, join them

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

mwenye macho haambiwi tazama Mpayukaji! Werevu na watu makini wanajua kuwa kuna kitu kinaendelea... Kuna usemi ulikuwa unaenda hapa Mjini Musoma kuwa Wagombea ubonge wa CCM na CUF walipokuwa wanajinadi walikuwa wakidai 'chagua ccm chagua mimi, usiponichagua mimi chagua mgombea wa CUF' and vice versa.

Mwisho wa siku wote walipigwa butwaa wa Chadema alipoibuka kidedea!

Tunayo safari ndefu umno ya kuhakikisha kuwa demokrasia ya ukweli inatamalaki Tz

NN Mhango said...

Wachangiaji wageni wangu mmenena vema. Umma umewasikia. Kazi kwake kujikomboa kutokana na utawala wa mafisi na mafisadi watokanao na uchakachuaji.