Monday, 22 November 2010

Je mbunge wako ni mwizi?


Odongo Otto Mtunzi na mbunge wa Uganda

Wabunge wanatumia nafasi zao kinyume cha sheria kujilimbikizia utajiri. Hivi ndivyo kitabu kipya kilichotungwa na mbunge wa Aruu Odongo Otto kinavyodokeza.

Kitabu cha “Theory and Practice of Parliamentary Democracy (Dhana na utekelezaji wa demokrasia ya Bunge- tafsiri ni yangu, kinaonyesha jinsi wabunge walivyotelekeza wajibu wao na kukimbiza pesa.

“ Warsha zinafanyika kwenye mahoteli ya kitalii kujadili bajeti ya wizara, na ajabu warsha hizi hugharimiwa na wizara.” Hii haina tofauti na ujambazi unaofanyika Tanzania. Rejea warsha elekezi kule Ngurdoto iliyoishia kuzamisha pesa ya walipa kodi wetu maskini na kisifanyike kitu zaidi ya wakubwa kujazana mapesa.

Kitabu kinaendelea “Kawaida warsha hizi huanza ijumaa na kila Mbunge hurejea nyumbani na posho ya mafuta hata kama warsha yenyewe imefanyika jijini-eneo la kawaida la kazi la wahusika..”

Akizidua kitabu chake Bungeni ijumaa Otto alisema: “ Najua kitabu hiki kitakwenda sambamba na bunge. Lakini wananchi wana haki ya kujua nani anawaangusha katika mapambano dhidi ya ufisadi. Naweza kuitwa na kamati ya nidhamu lakini watu wanapaswa kujua ukweli.”

Naibu spika, Rebecca Kadaga, alisema kuwa atatoa maelezo yake baada ya kukisoma kitabu husika.

Kwa ufupi Otto anajenga hoja kuu ya msingi kuwa bunge lazima lijipambanue na ufisadi na kuonyesha kwa vitendo jinsi linavyopambana nao badala ya kuushiriki kama yalivyo mabunge yetu.
Tanzania inapaswa kusoma kitabu hiki kutokana na kuwa na wabunge wengi wafanyabiashara ya haki za umma ukiachia mbali kuongoza kwa kuingia mikataba ya kiwizi na kusababisha umaskini wa kunuka.
Je mbunge wako ni moja ya hawa? Tafakarini.

1 comment:

Anonymous said...

Mpayukaji huwa unazinusaje? Tazama mtoto wa Lowassa anachunguzwa huko Uingereza. Bado Ridhiwani na Salma.
Big up kwa saaaaaana!