Friday, 19 November 2010

Simba anapogeuka mbwa!


Laiti wengi wangejua kuwa lengo la Maalim Seif Shariff Hamad ni kutafuta utukufu na ulaji binafsi, wasingemwanga damu zao kule Zanzibar. Sijui hii inajenga picha gani ambapo Seif amegeuka kiraka cha CCM nyongeza ya Augustine Mrema? Je ni wangapi watafuata matumbo yao na kutelekeza vichwa vyao ukiachia mbali nadhiri? Je kuna uuaji wa demokrasia wa kutisha kama huu? Kila wafanyapo dili zao wanasingizia amani na mshikamano. Je twaweza kuwa na amani na mshikamano vya kweli bila kutenda haki? Je amani na mshikamano vyaweza kushamiri sambamba na ufisadi wa wazi wazi na utawala wa kujuana,familia na kulipana fadhila? Je amani na mshikamano vyaweza kuletwa na watawala walioingia kwa uchakachuaji badala ya kura halali? Je kutanua au kulikwepa tatizo siyo kujipalia mkaa? Mbuni ana tabia moja ya kihayawani. Pindi amuonapo adui hufutika kichwa chake kwenye mabawa yake. Je hulka hii yamfaa mwanadamu tena aitwaye kiongozi? Tafakarini na jadilini.

2 comments:

Anonymous said...

Duh ni usaliti na usanii bab kubwa! Maskini wabongo tunaendelea kuliwa.

Fita Lutonja said...

Natamani kuihama nchi yangu Tanzania nningekuwa CUF ningemfukuza uanachama ili asitamb ulike na usariti wake