Thursday, 25 November 2010

Nchimbi ni kihiyo au genius?

Maelezo yaliyochapishwa na gazeti la Mwananchi la Novemba 24 juu ya historia hasa elimu ya waziri Emanuel Nchimbi yanaacha maswali mengi kuliko majibu.
Ukiangalia hapa chini unagundua kuwa Nchimbi alisoma shahada mbili yaani ya uzamili na ya uzamivu kwa kipindi kimoja yaani mwaka 2001-2003!
Si hilo tu, hata hicho chuo anachodai kupatia shahada ya uzamivu ukikichunguza kinatia shaka. Kina wafanyakazi wasiozidi 30 na masharti yake ndiyo usiseme. Je umefika wakati wa kumfichua Nchimbi huku tukimbana Jakaya Kikwete ambaye amefumbia macho tuhuma za kughushi vyeti vya kitaaluma za Nchimbi na wenzake?
Je hakuna watanzania wengine wanaoweza kuwa mawaziri hadi rais ang'ang'anie vihiyo na watuhumiwa wa jinai? Na hii si mara ya kwanza kwa Kikwete kujionyesha kama mvunja sheria. Aliwapigia kampeni watuhumiwa wa EPA na Richmond ukiachia mbali naye kutajwa kwenye list of shame. Je huu ndiyo ushirika wa mafisadi ambao wapinzani wamekuwa wakiupigia kelele? Je kama jamii tunapaswa kuendelea kunyamazia jinai hii?
Tafakari.


Jina: Emmanuel John Nchimbi
Nafasi: Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo
Tarehe ya Kuzaliwa: 24 Desemba, 1971
Jimbo la Ubunge: Songea Mjini (2005-2010) na ametetea tena nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu

Nafasi nyinginea alizowahi kushika:
Naibu Waziri: Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (2008 – 2010), Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana (2006-2008) na Habari, Utamaduni na Michezo (Januari 2006 – Oktoba 2006).
Mkuu wa Wilaya: 2003 -2005
Afisa Tawala, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC, 1998 – 2003)

Elimu:
CommonWealth Open University PhD (Management) 2001 2003 PHD
Shahada ya uzamili katika masuala ya fedha na benki (MBA), Chuo Kikuu Mzumbe, (2001 -2003)
Stashahada ya Juu ya Uongozi, Chuo cha Uongozi wa Maendeleo Mzumbe (IDM) (1994- 1997).
Je Nchimbi ni kihiyo au jiniasi wa kawaida?

5 comments:

Anonymous said...

ONLY IN TANZANIA...INGEKUWA KWINGINE HUYU ANGEKUWA AMESHAACHIA NGAZI MUDA MREFU SANA.

KIHIYO MWINGINE NAONA ALITEMWA NA WAPIGA KURA - HUYU NI DIODORUS KAMALA.

HIZI PHD ZA KUNUNUA ZITATUMALIZA. HUYU JAMAA NI WAZI KABISA ANA VYETI VYA KUGHUSHI LAKINI BADO TU ANARUNDIKIWA MADARAKA...

Anonymous said...

Sio elimu yake tu hata uzoefu wake unatia mashaka sana......na ukiangalia madaraka anayopewa inashangaza sana........wakati kuna wataalamu wengi sana wenye upeo na wapo tayari kuzifanya hizi kazi lakini hawapewi nafasi.........hivi sisi (wadanganyika tuna nini?) au aliyeturoga amekufa?

Nchi za wenzetu kugushi vyeti ni kesi ya kukupeleka Segerea tena mvua nyingi tu........na ukitoka huko hata ukianza darasa la kwanza mpaka PhD. jamii haitakutambua wala kukupa nafasi.....

Anonymous said...

Yasiyowezekana kwingine duniani, bongo yanawezekana. Hiyo ni sifa kuu mojawapo ya jamii inayoitwa bongoland. Angalia, chuo kikuu cha Dodoma hakijatoa mhitimu hata mmoja wa PhD, lakini kimeishamtunuku JK PhD ya heshima! Mimi ninafikiri wangesubiri angaa kuzalisha PhD moja ya kweli kabla ya kukimbilia kumtunuku JK PhD ya usanii. Hata hiyo ya heshima inapata uzito iwapo chuo hicho kweli kinazalisha PhDs. Siasa zinatokomeza elimu bongolanda.

Anonymous said...

Msishangae Kikwete kuwarejesha vihiyo wenzake. Huoni anavyotapeliwa kwa kupewa PhD na chuo cha UDOM ambacho ni tawi la CCM pia ambacho hakijawahi kutoa hata mhitimu mmoja wa PhD?
Kikwete alichemsha chuoni ndiyo maana akakimbilia jeshini na chamani. Alipaswa kuwa polisi. Nchimbi, Mahanga Makongoro, Mary Nagu, William Lukuvi,na majuha wengine wote ni matapeli wa kawaida.

Anonymous said...

Hali hii ikiendelea Tanzania itatawaliwa na kina Mangungo mambo leo. Je kwanini umma unaridhia uchafu huu? Ina maana umma nao ni fisadi kiasi hiki?