Monday, 1 November 2010

Je na hawa walichagua au CCM au mchakachuo?Picha kwa hisani ya Masangu Matondo Nuzulilima wa CHAKULA KITAMU.

Kwa matokeo yanavyotoka ni wazi kuwa uchakachuaji hasa kwenye kura za urais umefanyika. Kuna maswali mengi ya kujiuliza kuu likiwa ni kwanini matokeo yacheleweshe ukiachia mbali watu wengi (hasa wanaosadikiwa kuwa ngome ya upinzani kutokuta majina yao kwenye vituo)?
Japo CCM inaweza kujipa matumaini kuwa imshinda, imefungua pazia la kuporomoka na hatimaye kutoweka kwenye ramani ya Tanzania.
Je hao juu nao waliichagua CCM au Kivuitu Kiravu aliwachagulia?je hayo tuonayo ndiyo maisha bora aliyowaahidi Kikwete na akaahidi zaidi ya hapo? Je matawala anayechekelea na kuitumia hali hii kama mtaji wake si fisadi wa kiroho wa kutupwa? Tafakarini jamani.

2 comments:

SIMON KITURURU said...

Samahani natoka nje ya topiki!:-(

Nimepata kitabu chako Mkuu na naanza kukisoma leo jioni!:-)

Ni hilo tu Mkuu na AKSANTE SANA MKUU!!

NN Mhango said...

Ni furaha yangu kusikia hivyo. Lau nimetekeleza lile nililoahidi. Umeisikia SAA YA UKOMBOZI niliyotabiri ikianza kujiri huko nyumbani? Ubarikiwe na nategemea kusikia mchango wako tokana na kukibukua hicho kitabu.