Tuesday, 17 September 2013

Kikwete na watu wake na mambo yake

Kikwete anapomteua balozi wa heshima Ahmed Issa pichani na mkewe Julin wakati mtu mwenyewe hata hajulikani. Je ni kujuana, ukuadi, uzembe na ukosefu wa umakini, dili au vipi? Sitashangaa nikisikia siku moja amemteua Mohamed Gire wa Richmond kuwa balozi wa heshima. Huenda hawa marafiki wa Balali wana dili watakalolifanikisha la lala salama ya Kikwete.
Ni bahati mbaya kuwa bado Kikwete anakimbiza rekodi ya kuwa kiongozi wa kwanza duniani kuizunguka dunia bila kujali kuwa anaumiza walipa kodi. Hakika Kikwete hatakaa ajifunze ukiachia mbali kushabikia kuombaomba kunakomuwezesha kuzurura kila uchao.

2 comments:

Anonymous said...

Niliwahi kusema huko nyuma, mtu huyu anatumia sana mkasi (a.k.a. mikasi) kama kitendea kazi kikuu. Duh! Yeye full kuzindua kwa kwenda mbele.

NN Mhango said...

Anon hukukosea. Jamaa ni mgumu wa kujifunza na kubadilika. Tuombe muda wake uishe atokomee akiacha legacy chafu ya kuwa rais rahisi na kihiyo tuliyepata kuwa naye.