Sunday, 29 December 2013

Mkwe wa Museveni na Mugabe wakumbwa na kashfa.


Tunafunga mwaka kwa kuzidi kuibuka kwa madudu ya watawala wetu. Nchini zimbabwe, mkwe wa rais Robert Mugabe, Adam Molai (Pichani juu) akikumbwa na kashfa ya  kuingiza sigara nchini Afrika Kusini kimagendo. Molai ni mume wa mpwa wa Mugabe aitwaye Sandra Mugabe. kwa taarifa zaidi BONYEZA HAPA.
Wakati kashfa hii ya magendo ikifichuka nchini Zimbabwe, nchini Uganda mkwe wa rais Yoweri Museveni aitwaye Odrek Rwambogo (Pichani chini) anatuhimiwa kutaka kumhonga mgombea wa upinzani jumla ya dola za kimarekani 630,000 ili ajitoke kwenye kinyang'anyiro kwenye eneo lillogunduliwa mafuta la Bunyoro.
Kwa taarifa zaidi BONYEZA HAPA.

No comments: