Monday, 16 December 2013

Sudan Kusini yazima jaribio la mapinduzi


Usiku wa kuamkia tarehe 16 Desemba hii ulishuhudia mapigano makali baina ya vikosi vya jeshi la serikali ya Sudan Kusini na vile vinavyoaminika kumtii makamu wa rais  wa zamani Dk Riek Machar aliyetimuliwa hivi karibuni na rais Salva Kiir Mayardit.
Inasikitisha kwa nchi changa kuliko zote duniani kuanza kuadamwa na jinamizi la uporaji wa madaraka unaotakana na hisia za kikabila na tamaa ya madaraka. Je mamlaka mjini Juba zitashughulikiaje kitisho hiki bila kukiuka haki za binadamu? Je kuna mkono wa mtu hasa Sudan Kaskazini ambayo imekuwa ikituhumiwa kuwaunga mkono waasi wanaopigana na serikali ya Juba yenye utajiri wa mafuta? Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.

2 comments:

Anonymous said...

Ndiyo uhuru waliokuwa wanapigania miaka yote wauwane kwa bunduki ili iweje!?

Afrika hatima yetu naona ni kifo tuu na siyo maendeleo wakati wote wa maisha yetu...Inasikitisha sana lakini ndiyo inatokea Afrika...

Maendeleo ni sawa ya hadithi kwenda mbinguni....!

Anonymous said...

Hakuna jipya chini ya jua. Hata kama ningekua mimi, sioni hasara kuua mbwa mmoja kichaa ili kuinusuru familia yangu dhidi yake. Naona sasa saa ya ukombozi kweli inatimia. Kama nisemavyo siku zote Mwl Mhango atakumbukwa daima katika ulimwengu wa wasomi, lakini lah! Si ulimwengu wa Kikwete na waramba viatu wake. Nimewahi kuandika katika blogu hii kuwa kiatu cha Mwl Mhango kinawezaa kuvaliwa na maraisi watatu wa Afrika akiwemo Jikwete. Sina nia mbaya na Nchi yangu hii maskini, ila hawa kenge na mbwamwitu watakwisha at no time!