The Chant of Savant

Monday 10 February 2014

Mkiti wa CCM kizimbani kwa kuuza dawa feki

Mkurugenzi wa mashtaka Jinai (DPP) ameamuru mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa mkoa wa Dar Es Salaam, Ramadhani Madabida (Pichani) wa kwanza kushoto kufunguliwa mashtaka matano mojawapo likiwa ni kusambaza madawa feki yenye thamani ya mamilioni ya kurefusha maisha kwa waathirika wa ukimwi.
Hatutajadili kesi iliyoko mahakamani. Hata hivyo ukiangalia mrorongo mzima wa kesi na visa vya Madabida kujihusisha na uuzaji na usambazaji madawa feki havikuanza jana.Hapa unaweza kuona uovu na roho mbaya vinavyotawala Tanzania. Zamani wakati wa awamu ya kwanza mtu mwenye kutia shaka kama huyu asingeweza kuchaguliwa kiongozi hata wa shina. Ukisikia mfumo wa kifisadi ndiyo huu. Mke wa mtuhumiwa huyu ni mbunge ambaye bila shaka anatumia ubunge wake kutafuta dili kwa ajili ya madawa feki. Na hii si mara ya kwanza kwa Madabida kukumbwa na kashfa ya kuuza madawa feki. Mara ya kwanza alituhumiwa na mambo yakaisha kimya kimya. Huyu ibn muthnaq Madabida simtofautishi na habithi Ditopile Mzuzuri. Bila shaka naye atakufa mapema kama ilivyotokea baada ya Mzuzuri kuua na kulindwa na jamaa yake Kikwete asijue Mungu hana rushwa wala kujuana. Maana ukiangalia umati wa waathirika anaowaibia na kuwaua unashindwa kuelewa hata kilichowapa ujasiri CCM kuendelea kumbakiza kwenye wenyekiti.

9 comments:

Anonymous said...

Watanzania wanapenda viongozi wa aina hii
Kwani watanzania kwa ufahari na kujionyesha hakuna
Angalia eti kiwanja bagamoyo kinauzwa dola million 6
Nyumba mbezi beach dola laki tatu,
Kweli tembo watapona, madini yatapona, na wimbo wa watanzania wawekezaji, tena wachina ambo wao hawakuwekeza kwenye maliasili kwao.
Rafiki yangu mzungu aliniuuliza hivi africa hana watu wanaondika historia?
Nikamuuliza kwanini, akasema tulipokuja afrika tulituma wapelelezi na mission miaka 1000 iliyopita , walipokuja waliwapa zawadi machifu, vioo, bunduki ,nk
Tukawatawala miaka kibao tuchachukuwa uchumi wote, leo bado ni yale yale viongozi wenu kweli buumbuwazi kabisa, kila kukicha wawekezaji
Norway ipogundua mafuta ilichukuwa miaka 10 kupata watalaam wao, leo kwetu mpaka miaka 1000 watakuwa hao wawekezaji, inashangaza kasi ya ujenzi wa bomba la gesi unavyokwenda kasi huwaamini,
Reli iliyojegwa na mjerumani inasubiburi wahisani
Kweli tuiete BoNGO

Jaribu said...

Ni kweli Anonymous, vitu kama reli ni teknolojia ya zamani sana, ya karne ya kumi na tisa. Haihitaji maarifa sana kutengeneza na kumaintain reli ile. Shida ni kwamba Watanzania tunapenda viongozi kama hao, wezi na mbumbumbu.

Hizo bei za ardhi huko ni maajabu, ni kama Ujapani enzi za miaka themanini na tisini, ingawa wenzetu uchumi wao ulikuwa ni mzuri. Lakini hata na hao hawakuweza kumudu huu uchumi wa "povu" kwa muda mrefu, sembuse nchi ambayo wananchi wao wengi ni masikini. Nilikuwa nakaa Texas na huko nyumba ya dola 300000 ni ya ghali, nyumba siyo kiwanja cha dola milioni sita ni sehemu za matajiri ambao ni mamilionea wa kweli, siyo wa wizi.

Shida nyingine ya Tanzania ni kuwapapatikia wageni, hata wakiwa wahalifu. Wachina wako wengi, na wenyewe hawajaliani, huwezi kutegemea watatujali sisi au mali yetu. Nakumbuka kuliko na stori za huko uchina ukitaka kiungo cha mwili, kama moho au maini, basi wewe unaweka oda jamaa wanaenda kumpiga risasi mfungwa kesho yake unapata fresh. Siyo watu wa kuwaendekeza.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon na Jaribu mmeniwahi. Niko naandika makala ya kiingereza iitwayo Mortgage, mirage or mintage? Nilishangaa nilipowasiliana na kampuni moja ya kihindi ya ujenzi wa majumba nikaambiwa nyumba ya bei nafuu eti ni dola laki na nusu. Nilipomuuliza mhusika kama alikuwa serious akasema wanauza nyumba hadi dola milioni moja. Kichekesho ni kwamba unalipa 20% kama kianzio na ndani ya mwezi au miezi mitatu eti unalipa zilizobakia.
Nadhani biashara hii inawafaa wauza bwimbwi, mafisadi na majambazi. Ila siku hizi bubbles zikipasuka wengi watajinyonga. Huwezi kuwa na nchi inayoongozwa na rais mzuraraji na kihiyo kama Jakaya ukategemea maendeleo. Laiti Benjamin Mkapa asingeingizwa majaribu na mkewe mama tamaa angeacha legacy ya kupigiwa mfano. Kuondokana na upuuzi huu heri tuchague upinzani ili wahusika waishie kunyea debe nchi isonge mbele. Umenikumbusha msomaji wangu mmoja mwenye usongo aliyewahi kutoa pendekezo la kupambana na wahalifu kama Madabida. Alisema eti dawa ni kuwakatakata vipande na kuwalisha mbwa kama wanavyofanya uchina ambapo huwanyonga. Eti hawapaswi hata kunyongwa maana watafaidi.

Anonymous said...

Duh!
MURDER-BIDDER au MURDER BREEDER kweli noma!!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Wow! Murderbidders siyo? Imetuliwa kweli kweli.

Anonymous said...

Mwl. Mhango,
nimeli-coin hilo jina mahususi huku nikiwa chini ya shinikizo kubwa mno la hasira na jazba jinsi tunavyouawa kila upande.

Ninasubiri kusikia jamaa akikaangwa kule kijiweni na akina Mipawa, Mpemba etc.,

Huwa ninapata elimu na burudani mno kuangalia mambo kwa jicho la tatu.

Tuwekee hawa "Murdebidders" kwenye kikaango pale kijiweni, tafadhali.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon,
P0lease please naomba nilitumie jina hili ndugu yangu.
Umenitangulia hatua tano mbele katika hili so to speak.
Kama ulikuwepo. Laima Dabida liwepo kijiweni likichambuliwa sambamba na majangili na washenzi wengine.

Anonymous said...

Mwl., ruksa kabisa kumkaanga huyo kwa jina hilo. Hofu yangu tu ni iwapo Mgosi na Mipawa wataweza kutamka sawia.

Sikuwa nimefahamu kuwa "singular form" yake ni Dabida. Umetisha.

Kumbe sasa "plural form" ya prezidaa ni "Viquette"

Jokes aside, mwl., niruhusu nikiri kuwa huwa ninapiga njiwa wawili kwa jiwe moja (si murder, right?) kila nipitapo kwenye uwanja wako huu. Elimu & Burudani.

Keep up the good work.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon,
Nami nafarijika kusikia kuwa kumbe uwanja wangu si majigambo na mipicha ya kuwaramba watu makalio bali kutoa dozi na ilm.
Endelea kunitembelea na kunichangia. Nashukuru hata mkuu na waramba makalio yake wake wanaujua uwanja huu kiasi cha hata kufikia kutupiga vijembe kuwa tuko ughaibuni tunakesha kwenye mablog na kuisema serkali yake vibaya asijue tunaibomoa taratibu.