The Chant of Savant

Saturday 22 February 2014

Mlevi kuanzisha jeshi la kupambana na Jinai

Seriously, nilikuwa nchini Mexico juzi ambapo nilialikwa na rais wa nchi hiyo kumpa ushauri kuhusiana na jinsi ya kuboresha jeshi lake la Sungusungu la kupambana na wauza bwimbwi. Je ni kwanini aliamua kuniita? Alisema ni kwa sababu baada ya kusoma mojawapo ya vitu vyangu alipata wazo la kunialika hasa baada ya kuambiwa na mmoja wa waanzilishi wa Sungusungu wa kupambana na wauza bwimbwi kusema alipata wazo hilo toka kwenye makala yangu mojawapo.
Huwezi kuamini kuwa nilikuwa nimeishasahau kutokana na kuwa na mitikasi mingi ya kufanya. Si unajua tena mashine kubwa lazima ifikiri na kuchemka kama haina akili nzuri. Hata hivyo, nilifarijika kugundua kuwa kuna watu wanafuatilia ushauri wangu hata kama walengwa wangu wa Bongolalaland wanasoma na kusonya huku wakiendelea na business ya kuuza bwimbwi as usual. Hata hivyo, wakae wakijua kuwa kiama chao kinakuja kama walevi watanielewa na kuamua kujikomboa.
Hali ilikuwa mbaya sana hasa katika jimbo la Michoacan ambako nilishuhudia wakuu wa magenge ya kijinai wakikamatwa na kunyotelewa roho mchana kweupe. Hata ndata waliokuwa wakila nao baada ya kugundua kuwa walevi wanaweza kuwachenchia kibao, walilazimika kujiunga na sungusungu hawa waliozaliwa na wazo langu. Maana kushuhudia watu wakiuawa kupigwa au kutozwa pesa ili kuendesha maisha yao ya kawaida kulikokuwa kukifanywa na magenge ya wauza unga ilikuwa jambo la kawaida. Baada ya wananchi kuchoshwa na uonevu na unyama huu, waliamua kufuata ushauri wangu. Hivyo, hata walevi kujikomboa kutokana na kutenzwa kinyama na magenge ya kiharifu kama vile ndata, wauza bwimbwi, sirikali na manyang’au wengine lazima kukomeshwa mara moja.
Baada ya kutoa muhtasari wa kwanini nataka kuanzisha Jeshi la Kupambana na Jinai kwa kikameruni Force Against Crimes in Tanzia (FACT). Tofauti na wenzetu wa Mexico, sisi tutapanua wigo na kupambana na wauza bwimbwi, mafisadi, walioghushi, wala rushwa, vyangudoa wa kila aina kuanzia wa kimaadili hadi wa siasa.
Kwa vile wanaouza bwimbwi, kupokea rushwa, mafisadi, walioghushi na hata wanaofanya usharmuta wa kila aina wanajulikana, FACT itakuwa ikivamia makazi yao na kuwakamata na kuwapa kichapo kabla ya kupitisha hukumu ya umma kama wanavyofanya kule Mexico.
Najua wengi wanaweza kuchukulia wazo hili kama la kilevi na lisilowezekana.  Kwa vile kwetu wameshindwa hivyo lazima tuwasaidie. Tuna hakika tutafanikiwa kwenye vita hii ya kuikomboa na kuigomboa kaya toka kwenye mikono ya waovu hata kama baadhi yao wana maulaji na mamlaka. Sisi hatutabakisha kitu. Tutapambana na yeyote kumuonyesha kuwa kaya hii ni ya walevi na si ya watenda jinai.
Je unajua ni kwanini watendaji wako wameshindwa? Rushwa rushwa ndugu zanguni. Mijitu imehongwa kiasi cha kukamatwa mateka. Hamkusikia wale waliojitapa kuwa wana orodha ya watenda jinai wote kuanzia wauza bwimbwi, mafisadi, wala rushwa na hata majambazi lakini wakashindwa kuwashughulikia? Sasa tunasema bila kumung’unya maneno kuwa naye tutamwendea atupe sababu nuzuhu za kutowashughulikia hao waharifu kama si wenzake. Hatutaangalia mtu usoni wala kujali cheo na hadhi ya mtu. Lazima kuikomboa kaya toka kwenye mikono michafu ya magenge ya kijambazi.
Najua mtauliza: Je wanafaidika vipi? Si wanakatiwa na kukatiana vitu na uchache huku wakiuacha umma wa walevi uteketee huku wao wakipeta na kuwa mabilionea bin vuu. Sasa muda wa kuendelea kutumiana, kulana na kuuza umekwisha. Lazima walevi wachukue hatua mujarabu.
Kwa vile wale walioaminiwa madaraka wameyachezea au kufanya kile ambacho wakameruni huita to sleep on the wheel, walevi kujichukua hatamu na kukomboa kaya yao. Lazima kuondoa huu wendawazimu ambapo kaya imechafuliwa kiasi cha kukosa hata maana. Hebu fikiria, kwa mfano, washenzi wanaua elimu kwa vile wanasomesha vitegemezi vyao nje na kujenga taifa la wajinga. Je namna hii tutafika? Heri walevi tuingilie kati maana ulevi ni bora kuliko ujinga ingawa na ulevi wenyewe unategemea. Hatuwezi kuendelea kushuhudia elimu yetu ikizama huku sirikali yetu ikijaa vihiyo walioghushi wanaotuuza kwa wachukuaji. Lazima tufanye kitu na kitu chenyewe ni kupitia harakati za FACT kuwanasa na kuwapatiliza wote walioleta balaa na zahma hii.
Hatuwezi kuvumilia kuona mijitu vihiyo mafala na majambazi ikitukoga kwa utajiri ambao ni matokeo ya jinai tena dhidi ya walevi. No. It can’t be us. We’ll fight too see to it that we emancipate ourselves so as to see true manumission of Bin-Adam even if we are boozers. In fact, FACT is there to bring about some real and desired changes in Danganyika. I promise. FACT’ll take thugs’ crown away just soon.
Hatuwezi kuacha mambo kuendelea kienyeji na kijambazi kama yalivyo. Hakuna kilichoniacha hoi kama juzi tu kikundi cha vitoto kiitwacho Mbwa Mwitu kuwatoa jasho. Tukio jingine ni lile la muuaji wa halaiki wa kule kwa akina Mura Mwita aliyenyotoa roho walevi zaidi ya kumi bila kudedishwa. Angekuwa amepambana na FACT angeishakuwa past tense zamani gani. Tunataka kuwaonyesha hawa wapuuzi wanaochezea ulaji jinsi warume tunavyofikiri na kutenda. Tunataka tuwaonyeshe tusivyofikiri kwa massaburi kama wao. Sisi ni vichwa wala si massaburi kama wao. We’ll show them what it means to be thinkers who use kanywaji to warm their brains up. Leo jamani tuvumiliane kwa kuongea sana ukameruni. Ni kutokana na hangover niliyoipata pale Heathrow wakati nikirejea zangu toka Mexico. Hamuoni wale wanaorejea na hangovers kutoka Jersey, Uswisi na nchi nyingine wanakoficha njuluku wanavyoiba zaidi na zaidi kiasi cha kaya kuanza kuwa na mabilionea wezi watupu? Hivi kweli mbunge Kwa mfano, anaweza kuwa bilionea bila kuiba kwa kutumia uishiwa wake? Waulize akina Roast Tamu La Aziz na Mooooo Dewiiiiji. Wanaitwa mabilionea wakati ukweli siyo bali wasanii wanaotumia mfumo wetu mbovu na uongozi mfu na uchwara ambao lazima FACT iukomeshe. Moody Madabidabi uko na utapeli wako wa kuuza ARvS feki?
Habari ndiyo hiyo washikaji.
Chanzo:Nipashe Jumamosi Feb., 22, 2014.

No comments: